Huyu ndiye Lee Byung Hun

Huyu ndiye Lee Byung Hun

Tea Party

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2019
Posts
658
Reaction score
1,133
HUYU NDIYE LEE BYUNG HUN

Kama umeangalia IRIS kipindi kile inaoneshwa ITV basi huyu jamaa utakuwa unamfahamu.

Kwenye IRIS alitumia jina la Kim Hyeonjun agent wa South Korea aliyesalitiwa na nchi yake baada ya kwenda kwenye mission ya hatari huko Budapest Hungary.

Pia kama umeangalia MR SUNSHINE pia utakuwa umemuona humo. Hivi hapa ni vitu kumi kutoka kwake ambavyo pengine utakuwa huvifahamu.

1. Cha kwanza kabisa ni kwamba mpaka sasa ana miaka 50. Pamoja na kwamba anaonekana mdogo lakini amezaliwa 1970 huko Gwangju, Gyeonggi Korea ya Kusini.

2. Kama ilivyo kwa waigizaji kutokea Korea Lee Byung Hun ni msomi alipata degree ya French Literature pale HANYANG UNIVERSITY. Akapumzika kidogo.

Baadae alingia CHUNG ANG UNIVERSITY na huko akasomea Theater and Cinematography.

3. Wakati anaigiza IRIS Byung Hun alikuwa analipwa Usd 90,000 kwa episode moja. Ikumbukwe pia kwamba IRIS ilikuwa na episodes 16.

Hivyo Byung Hun alilipwa zaidi ya dollar Million 1 alipokuwa anaigiza IRIS.

4. Lee Byung Hun ni mume wa mtu. Amemuoa muigizaji mwenzie aitwaye Lee Min Jung (aliigiza kwenye Once Again) mwaka August 10 mwaka 2013.

Harusi hiyo ilifanyika pale Grand Hyatt Hotel Seoul.

5. Mwaka 2009 aliingia kwenye soko la filamu la nchini marekani baada ya yeye kuigiza kama STORM SHADOW kwenye movie ya GI JOE : THE RISE OF COBRA.

Movie hii ilimpa umaarufu mkubwa sana huko nchi korea na kupelekea watu wegi kutokea nchini Marekani wamfahamu.

6.Lee Byung Hun ana uwezo wa kuongea Kiingereza, Kifaransa, Kichina na Kikorea.

7. Byung pia ana kampuni iitwayo BH ENTERTAINMENT ambayo juzi juzi tu hapa iliingia mkataba na KAKAO H ilikuikuza kampuni hiyo.
BH imewasain waigizaji kama Kim Go Eun, Kim Yong Ji, Lee Jin Wook na Han Ga In.

8.Lee Byung Hun ni mojawapo kati ya wasanii wachache kutokea nchini Korea ambao wameshinda tuzo zote za heshima kubwa sana nchini Korea.
Tuzo hizo ni BAEKSANG ART AWARDS, BLUE DRAGON AWARDS pamoja na GRAND BELL AWARDS. .

9. Ukiachana na series pia Lee Byung Hun ameigiza movie mbalimbali kama ASHFALL, FORTRESS na THE MAN STANDING NEXT.

10. Mwisho kabisa Lee ana uzito wa 72 Kg.


Uzi tayari!
MV5BMTcxMDA5Mzk1NF5BMl5BanBnXkFtZTcwMzI0MDg3Nw%40%40._V1_.jpg
lee-byung-hun.jpg
Cover_Final_ColourA.jpg
1586480363-20200409-leebyunghun.jpg
Lee-Byung-Hun-and-Lee-Min-Jung.jpg
 
Hee huko Korea wanakula nn jaman mtu anamiaka 50 lakn muonekano Kama janki tu wa miaka 24 hivii

Mwamba alitisha Sana kwenye ile Iris 1 kam yeye ana 50 vpi BAEK SON atakuwa na umri gan?
 
Jamaa namuelewa sana hana movie mbaya
 
Kumbe huyu ndo aliegiza kama White Ninja kwenye GI Joe, nilipenda bifu lake na Snake Eye (Black Ninja) na jinsi walivokuja kua pamoja kwenye Part Two.
 
Moja ya Korean Drama ambazo niliwahi kuzikubali, basi ni hii ya IRIS! Sema tu ilinikera sana 😞 pale jamaa alipo tunguliwa na risasi wakati yupo njiani aki drive kwenda kuonana na yule mpenzi wake, aliyekuwa akimsubiria kwenye ule mnara.
 
Aisee ile movie ni kali sana, nilipenda kupata zile soundtrack zote audio lakini sijapata
 
Hee huko Korea wanakula nn jaman mtu anamiaka 50 lakn muonekano Kama janki tu wa miaka 24 hivii

Mwamba alitisha Sana kwenye ile Iris 1 kam yeye ana 50 vpi BAEK SON atakuwa na umri gan?
Wanakula kimchi hao,ukitaka kujua utofauti wa misosi yao nenda pale the Goong masaki ni korean restraurant ukajionee mambo,wali kidogo side dishes kibaooo
 
Wanakula kimchi hao,ukitaka kujua utofauti wa misosi yao nenda pale the Goong masaki ni korean restraurant ukajionee mambo,wali kidogo side dishes kibaooo
Yaah pamoja na BIBIMBAP na GOLGI

hyo kimchi n mchanganyiko wa mbogaza majan na wanakula zikiwa za motooo
 
Back
Top Bottom