Huyu ndiye msanii mwenye mafanikio makubwa kuliko yeyote Tanzania nzima

Huyu ndiye msanii mwenye mafanikio makubwa kuliko yeyote Tanzania nzima

Anaitwa AMBWENE YESSAYA AKA AY ni mmoja wa wasanii ambaye ana mafanikio makubwa sana kimuziki kuliko msanii yeyote yule hapa nchini Tanzania, vile vile yeye ndiye msanii wa kwanza Tanzania kuipeperusha bendera ya Tanzania katika anga za kimataifa mpaka ulaya. Historia yake ya muziki ilianzia miaka 1998

-Pesa yake ya kwanza kurekodi ngoma studio alipewa na mama yake Tshs 20000/=
-Ni mkulima (ana mashamba ya mpunga zaidi ya heka 100 huko ifakara Morogoro
-Ni mjasiriamali mwenye biashara nyingi ikiwemo duka la nguo
-Ni mmiliki wa vipindi vya TV vya MKASI na NGAZI KWA NGAZI vinavyorushwa EAST AFRICA TV

-Anamiliki kampuni ya UNITY ENTERTAINMENT inayojihusisha na uwakala wa kazi za sanaa, matangazo na kuunganisha wasanii, pia kuleta wasanii wa nje


CONCLUSION:
HAYO NI MACHACHE KUHUSIANA NA SUPER LEGEND AY MZEE WA COMERCIAL
Mbona hakuna cha maana ulichoandika hapo
 
Yani kuna watu wana majibu humu, unaweza ukakimbia hata na uzi wako uliouanzisha
 
YALE YALE YA ZAMANI ETI OOOH JUMA NATURE ANA PESA KUFURU,HALAFU HAWANA DATA.NIMEJIONEA KWA MACHO NATURE ANA NYUMBA ZA KAWAIDA MBILI AU TATU HIVI NA GARI ALIYONAYO NI ALTEZA.KAMA UNABISHA NJOO MBAGARA RANGI 3 KISHA CHUKUA BODABODA WAAMBIE WAKULETE MABANDA KWA NATURE.

Nimesema yote hayo kuonesha namna watanzania wanavyoweza pika storh bila kua na data husika.Je huyo AY kwa assests gan alizonazo,kwa matasha gani anayofanya au kwa show gani anazozifanya na kwa mikataba ipi MIKUBWA ya matangazo aliyonayo zaidi ya Samsung!!!!
 
Anamiliki kampuni ya Unity Entertainment...wakati in the same time nasikiwa kasaini na sijui na kampuni ya Babu Tale,or somebody else,ila kasaini kwa mtu tena recently tu...

Therefore kwenye medani ya biashara za ku-manage wasanii na biashara ya muziki kwa jumla hajafaulu...unaendaje kusainiwa kama msanii kampuni ya mwingine yako unamwachia nani?

Na pia,hizi taarifa za mali na mafanikio ya biashara kwa wasanii hua siamini takwimu,kiasili wasanii wote wanakuza vitu mara tatu zaidi ya ukweli just kujenga taswira ya showbiz,nothing more.

Hizo takwimu mi zitakua halisi kwangu kama nikizichukua na kugawanya kwa 3....

Na pia niweke wazi mrengo wangu,AY na MwanaFA nawachukia tu,sijui kwanini,I can not stand these guys...mi sio mnafiki,I hate these ni.ggaz for the sake of it....unajua kuna watu tu hua unawachukia bila sababu,basi kwangu mimi ni hawa jamaa,...basi tu,na sitaki ushauri [emoji37][emoji37][emoji37][emoji37]
Mm FA sitaki hata kumsikia anamajivuno ndio maana mziki wake unakuwa kama bablish
 
Hujakosea mkuu, ila ungemtaja msanii mwngine tofaut na yeye ningekupiga penga..
 
hivi inakuaje hawa wasanii wakubwa walioibukia kuanzia 2008 mpaka sasa wanashindwa kabisa kutengeneza pesa na kuwa atleast mentioned kwny list ya wasanii wenye mkwanja........ukitoa diamond wengne cjui wanakwama wp mana kila siku naskia wale wale.......prof j, diamond, jay dee, and AY
 
Back
Top Bottom