Huyu ndiye Mwigulu Nchemba

Sophia Andrew

Senior Member
Joined
Sep 19, 2014
Posts
114
Reaction score
7
Baada ya kumalizika kwa Kamati kuu ya chama iliyoketi kwa siku mbili hapa Dodoma, Kamati kuu ilimpongeza mh Mwigulu Nchemba kwa jitihada zake za dhati katika kupambana na kuisaidia serikali hasa katika Kukusanya kodi toka bilion300 hadi bilion 800 kwa mwezi pia kwa kutatua kero nyingi za walimu Nchini.

Nikimnukuu kuhusu yeye kuwa rais anayependekezwa mh Mwigulu anasema
"CHAMA chetu ni chama cha utaratibu na mimi ndiye msimamizi mkuu ndani ya chama, kundi langu ni CCM, wana CCM wana matumaini makubwa na mimi ya kuwavusha katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu".

Mwigulu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba.

Katika kipindi kifupi tangu kuteuliwa kwake katika nafasi ya Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu ameonesha ni kwa kiasi gani alivyo na uwezo mkubwa katika uongozi na kusimamia ustawi wa nchi na watu wake.

Tumeweza kushuhudia hofu ya Mwigulu pale aliposimama bungeni katika Bunge Maalumu la Katiba kutoa tahadhari kuhusiana na fedha za walipa kodi.

Akiwa miongoni mwa viongozi tulionao nchini, aliweza kupatwa hofu ya fedha za walipa kodi kutumika ndivyo sivyo.

Hili si jambo la kupuuzia hata kidogo, bali ni jambo la kujivunia kuwa na kiongozi mwenye uthubutu katika kipindi hiki ambacho Watanzania wanasumbuliwa na misigino ya kisiasa.

Katika mchango wake alionesha hofu yake ya kuendelea na majadiliano kwa siku 84 na hatimaye kushindwa kupata theluthi mbili za Tanzania Bara na theluthi mbili za Tanzania Visiwani ili kupitisha Rasimu tayari kwa kupigiwa kura ya maoni na Watanzania.

Mwigulu alifikia hatua ya kumtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba afanye hesabu na kujiridhisha juu ya kupatikana kwa takwa hilo la Kikatiba.

Hii ilikuwa ni hofu kuu. Ni hofu iliyotoka rohoni, isiyokuwa na chembe ya shaka. Aliweza kuona dalili za kulazimisha visivyolazimishwa.

Hofu inayolenga kuponya fedha za walipakodi wa nchi hii zinazoweza kutafunwa kwa siku 84 bila ya kupelekewa Rasimu ya Katiba kuipigia kura.

Ni hofu ya wengi, wachambuzi na wachokonozi wa kisiasa waliiona kauli ya Mwigulu kama kuanza kushtuka kwa CCM na viongozi wake.

Mwenyekiti wa Bunge hilo hakuweza kuiona hofu ya Mwigulu, hakuufanyia kazi ushauri wa mjumbe wake, lakini naamini ya kuwa nafsi ya Mwigulu ilikuwa huru baada ya kutoa dukuduku lake.

Kutokana na wadhifa wake ndani ya chama na Serikali Mwigulu amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha anasimamia fedha za walipa kodi wa nchi hii zisitumike vibaya bali kwa maslahi ya wote.

Tumeshuhudia ni kwa kiasi gani amesimamia fedha zilizokuwa zikiibwa kupitia mishahara hewa na kutoa angalizo kuhusiana na fedha hizo.

Nchi inao viongozi wengi, lakini viongozi aina ya Mwigulu ni wa kuhesabu kama si kutafuta. Tunalo jukumu la pamoja kuhakikisha viongozi wetu wanatekeleza majukumu yao kama afanyavyo huyu ambaye ameonesha njia.

Tunalo jukumu kumhakikishia ya kuwa tunamuunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yake na katika kulitumikia taifa letu na sio kumbeza kama ambavyo wengine wanafanya.

Pamoja na Mwigulu kuwa Naibu Katibu Mkuu CCM amekuwa akitimiza majukumu yake ya Naibu Waziri wa Fedha bila ubaguzi jambo ambalo limekuwa adimu katika kipindi hili.

Tanzania yangu ya sasa inahitaji viongozi walio na utayari wa kuwatumikia wananchi wake, walio na uchungu na mali na raslimali za nchi na si vinginevyo.

"Mimi sio matokeo ya jitihada za kundi lolote kufika hapa nilipo, niligombea ubunge nikiwa sijulikani na kundi lolote na wala sikutengenezwa na kundi lolote.
Hata nilipokwenda kugombea sikuwa hata na baiskeli, pikipiki wala gari. Mimi sina kundi na wala sitokani na makundi yanayokinzana, sina kundi lolote ndani ya chama wala siegemei kundi lolote."

"Lililo jema ni kutokuwa na chuki wala ugomvi na wanaCCM wenzangu. Sina sababu na wala sioni faida ya kuingia kwenye makundi katika ngazi hii na muda huu." anasema.

Hii ni miongoni mwa kauli zilizowahi kutolewa na Mwigulu, kauli inayopashwa kutolewa na kiongozi anayesimamia kile anachokiamini katika utekelezaji wa majukumu yake bila kuegemea upande wowote ule.

Tanzania ya kizazi hiki inahitaji viongozi wenye maono, wenye uthubutu wa kusema hapana sasa imetosha, viongozi walio na uchungu na ndugu zao kutokana na maisha wanayoyaishi.

Mwigulu Nchemba ni miongoni mwa viongozi walioonesha msimamo wao katika kutetea kile wanachoamini kuwa ni kwa ajili ya Watanzania wote na kwa faida ya wote.

Ni vyema tukasimama na kumuunga mkono yeye pamoja na viongozi watakao kuwa tayari kutimiza wajibu wao kama afanyavyo Mwigulu.

Tunalo jukumu la kusimama pamoja na Mwigulu kuhakikisha ya kuwa yale anayoyabainisha anayatetea bila hofu kwa faida yetu sote.

CHANZO: DIRA YA MTANZANIA
 
Mwigulu Nchemba ndio Rais 2015 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana ni Mwadilifu, Mzalendo na Mwajibikaji katika Uongozi.
 
Mwigulu Nchemba:Kitu ambacho watanzania wajue ni kuwa wanahitaji kiongozi mwenye mtazamo mpya na anayeamini kuwa mabadiliko ni vitendo na si kiongozi anayehitaji kutimiza ndoto zake za kuwa rais tu.Tunaimani na Mwigulu Nchemba.
 
Hata vijana tunamkubali huyu jamaa ndo mzalendo wa kweli
 
Acheni siasa maji taka. Huyo bado hajakomaa kiutendaji kabsa.
 
Mwigulu anakubalika na wananchi walio wengi
 
Mwigulu Nchemba ndio Rais 2015 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana ni Mwadilifu, Mzalendo na Mwajibikaji katika Uongozi.

Ni nani kakuruhusu uwe msemaji wangu?

Ama ni nani amekuruhusu kuwasemea watanzania?

Na ni nani amekupa huo umungu wa kupanga yajayo?

Raisi wangu ni EL baaaaasi usithubutu kunisemea tena
 

Nani amekuruhusu kuwa msemaji wa wsTz???
 
Acheni siasa maji taka. Huyo bado hajakomaa kiutendaji kabsa.

Waliokomaa na kuijua vizuri system ndio wanaotuibia na wametuletea wakina EPA na Richmond hadi Dowans
 
Nanyie ma ccm mna2changanya ma lowasa acheni zenu hata mwigilu hana lolote
 


SIFA ZA KIJINGA BANA! iv unajuwa wakati MKAPA anaachia madaraka serikali ilikuwa inakusanya sh. ngapi kwa mwezi? mwigulu amekuja juzi unatuambia ametoa bilion 300 hadi 800. naendelea kugundua kuwa tatizo letu ni kubwa kuliko tunavyolijua, wazungu wanasema tunawaza vizuri zaidi kwenye masuala ya ngono kuliko mambo ya jamii na maendeleo.
 
Kwanini asifiwe Naibu badala ya Waziri mwenyewe?
 
mmepewa pesa ili mumpigie debe huyo mpuuzi mwenzenu nn? eti nchema nchemba haaaaa! hafai kabisa na kama amewahonga ili mumsaidie mwambieni ukweli kwamba hakubaliki hata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…