Wasifu wa rais ajaye huu hapa
1. Ni mzawa halisi wa kitanzania kutokana na wazazi wake wote ni watanzania wakiwemo babu zake
2. Amesoma elimu ya msingi na sekondari katika shule zetu za kitanzania
3. Amelitumikia jeshi la wananchi watanzania, ambapo aliweka historia kwa kuongoza kikosi cha mizinga wakati wa mafunzo jkt
Huu ni ujasiri na uzalendo wa juu kwa nchi yake.
4. Amepewa cheo cha FIELD MASHO na amefanikiwa kufanya mafunzo muhimu ya kiulinzi na kiusalama toka vyuo bora vya kijeshi duniani katka nchi za Urusi, Cuba, USA, na UK. Mbali na mambo mengine ni kachero wa kimataifa.
5. Amefanikiwa kupata shahada yake ya kwanza na ya pili toka TANZANIA
6. Amepata makuzi yaliyojaa uadilifu kwani mbali na kutoka familia yenye legacy ni mtu wa kawaida sana kwani hana ardhi zaidi ya ile ya kurithi, anatembelea gari aina ya Noah, na hana miradi ya kibepari, anamiliki nyumba moja yenye vyumba 4
7. Ni rafiki mkubwa wa aliyekuwa rais wa Venezuela mwanamapinduzi Hugo Chavez, Fiedel Castro wa Cuba, Vladmir Putin wa Urusi, Familia ya F.Kenedy wa USA.
8. Katika Afrika ni swahiba wa Robert Mugabe, Yoweri Museveni, Thabo Mbeki n.k
9. Ameombwa na kushawishiwa sana kuwania nafasi hii kubwa kabisa ndani ya JMT kupitia viongozi wakubwa wastaafu, viongozi waadilifu wa kidini, na wanazuoni mahiri bado hajajibu mpaka sasa
10. Anabebwa na uadilifu/usafi kuliko yeyote mwenye ndoto na nafasi hii.
11. Anao ujasiri wa kukemea uovu ikiwemo rushwa na ufisadi ambavyo vimekuwa kansa ya uwajibikaji ndani ya serikali nchini.
12. Anajua vipaumbele vya watanzania.
13. Kiafya na kiumri anatosha kuliko mgombea yeyote ndio maana atafanya vipimo na kuomba watanzia wajulishwe.
14. Ni mtu wa maamuzi sahihi na kwa wakati yenye manufaa kwa taifa.
NB: Atafanya mhadhara Nkurumah UDSM akisindikizwa na Mzalendo na mwanamapinduzi Robert Mugabe, Wahadhiri nguli nchini, mawaziri wakuu wastaafu, marais wastaafu JMT na SMZ, Viongozi wa dini n.k.
Kuwa mzalendo, kataa kurubuniwa kwa fedha, kwani TANZANIA NI YAKO!!!!!!!!!!!!