Huyu ndiye Mwigulu Nchemba

Hakuna lolote, juzi tu alikuwa mtukanaji mzuri na ropokaji, leo tu kapewa madaraka tayari keshakuwa mwerevu, watanzania tunadanganyika kirahisi sana ndo maana tutaendelea kulia maisha yetu yote na nchi wataipukutisha.
 
Mwigulu ni taswira mpya yenye matumaini mapya 2015
 
Uongo ni dhambi kwa maracya kwanza nlikua na mwona kama mlevi ila kwa sasa na mwelewa vzr na ni jambo jema Watanzania tumuunge mkono na kuzd kumwombea make anatufaa
 
Hakuna lolote, juzi tu alikuwa mtukanaji mzuri na ropokaji, leo tu kapewa madaraka tayari keshakuwa mwerevu, watanzania tunadanganyika kirahisi sana ndo maana tutaendelea kulia maisha yetu yote na nchi wataipukutisha.

Mkuu umenena huyu mtu ni laghai la karne! Ni hatare, weka mbali na watoto!
 
Kwa Hisani ya Kalamu ya Marehemu Robert Lengeju

"Wakati ninyi mnaendeleza matusi kwenye mitandao, mnararuana mchana kweupe, mnaendeleza makundi na mipasuko ya kichawi, CCM wanaendela kutulia na kupanga mashambulizi kisayansi. Mwigulu Nchemba mliyezoea kumsikia akitoa shutuma za 'kujilipua' sasa anatumia muda mwingi kufungua matawi ya chama na kuimarisha yale ya zamani, vijijini. Katika mikutano yake anazungumzia changamoto za ajira, umuhimu wa vijana kujituma na kuzifuata fursa na kuwaomba watanzania waendelee kukiamini chama hiki kilicholeta uhuru . Wakati mawaziri vivuli wa Chadema wakiwa 'busy' na kutafuta risiti feki za kupakaziana posho hewa, mawaziri wa CCM wako bize kujenga barabara, kuchimba visima vya maji, kujenga madaraja, kujenga shule kila kata, kuboresha mazingira ya watu kujitegemea na kujitafutia kipato"

Mwigulu ni Taswira Mpya yenye Matumaini Mapya
Tunamuunga mkono
 
Wakati ninyi mnaendeleza matusi kwenye mitandao, mnararuana mchana kweupe, mnaendeleza makundi na mipasuko ya kichawi, CCM wanaendela kutulia na kupanga mashambulizi kisayansi. Mwigulu Nchemba mliyezoea kumsikia akitoa shutuma za 'kujilipua' sasa anatumia muda mwingi kufungua matawi ya chama na kuimarisha yale ya zamani, vijijini. Katika mikutano yake anazungumzia changamoto za ajira, umuhimu wa vijana kujituma na kuzifuata fursa na kuwaomba watanzania waendelee kukiamini chama hiki kilicholeta uhuru
 
MWIGULU NCHEMBA RAFIKI WA WALALA HOI, KIPENZI CHA VIJANA , ALAMA YA UZALENDO, UJASIRI NA UTHUBUTU
Kwa Mtanzania yoyote anaefuatilia siasa hili jina sio geni sana masikioni mwao, wapo waliolisikia jina hili kwa namna yoyote ile mbaya au nzuri leo nataka nimzungumzie Mwigulu Lameck Nchemba Mbunge wa Iramba Magharibi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM na Naibu Waziri wa fedha kwa namna ninavyomjua na harakati zake za kisiasa ninavyozitazama.

Alizaliwa tarehe 7 January 1975 katika kijiji cha Makunda Wilaya ya Iramba katika familia ya kimaskini kabisa ambayo baba alijishughulisha na ufugaji, huku mama akijushughulisha na kilimo. Maisha ya utotoni ya Mwigulu Nchemba yamegubikwa na tabu nyingi na mara nyingi amekuwa akikiri aliishi kwa uji kutwa nzima na kukutana na mlo mmoja tu jioni hasa kutokana na muda mwingi kutumia kuchunga ng’ombe.

Maisha haya ya kushinda na wanyama porini mda mwingi na kukabiliana na wanyama wa hatari, hali ya hewa mbovu kama mvua kali au jua kali yalimjenga katika ujasiri ambao hadi leo hii anao nitauelezea badae Katika makala hii. Kama ilivyo ada familia za kifugaji kulea watoto katika misingi ya heshima, Upendo adabu na utu, Mwigulu Nchemba alikuzwa hivyo kuheshimu watu, na kuthamini utu wa Mtu na kuwa na upendo kwa binadamu wenzake.
 
Jee kwenye tafiti za TWAWEZA kapewa asilimia ngapi? Au ndio kaangukia kwenye lile kundi la Others lenye asilimia 1.3 kwa ujumla wao?
Kumtaja Mwigulu na Urais ni sawa na ujuha uliopitiliza.
 
Ngoja na mimi nitafute skafu ya Tanzania. #MwiguluAnatosha

Alipata ufaulu mzuri na kujiunga Chuo Kikuu cha Dar es salamu UDSM mwaka 2001 - 2014. Katika maisha ya chuo hakujishughulisha na siasa za chuo kabisa waliosoma nae wanasema alikuwa mpole kupindukia, ambaye alikuwa na marafiki wachache sana wala hakufahamika. Jambo lililokuja kumfanya kuwa maarufu ni pale alipofaulu kwa kiwango cha juu na kuwaongozea wanafunzi wenzake wa kitivo cha uchumi. Hapa ndipo alipoanza kufahamika. Nilipopata bahati ya kumuuliza kwa nini hakupenda kufanya siasa chuo kikuu alinijibu kwa kifupi “ Kila jambo na wakati wake, niliona ninasoma kozi ngumu ya uchumi, mbele yangu niliona nina wajibu mkubwa wa kutumia elimu hii kulikomboa taifa langu kiuchumi hivyo sikuona haja ya kujihusisha na siasa za kitoto nikiwa chuo wakati wangu ulikuwa bado.”

Baada ya kumaliza masomo Chuo Kikuu Dar es salamu na kupata ufaulu mzuri alichukuliwa moja kwa moja na Bank kuu ya Tanzania inayotuhumiwa kulundika watoto wa wakubwa lakini yeye alikwenda kwa sifa tu. Hakumjua mtu yoyote na hapa ndipo Bahati yake na muujiza wake wa kwanza ulipoanza kujionyesha. Na kudhibitisha nyota yake ni mshale akilenga hakosi.
 
Mwigulu ndiye kiongozi pekee wenye taswira njema ya Urais wa Tz kwa utendaji wake ulio na uadilifu mkuu
Kweli anaweza kuwa mzuri, Sikatai, lakini yeyote atakaye ongoza hii nchi kutoka ccm hata awe muadilifu kama malaika hataweza kufanya mabadiliko yoyote, CCM imeoza. Anachofanya Mwigilu ni Siasa ya kujijenga lakini hana lolote zaidi ya wenzake. Kikwete aliingia na Nguvu ya ajabu, ahadi nyingi kubwa kubwa, watu walipata tumaini, mpaka hata wachungaji walikufuru kusema kuwa ni chaguo la Mungu, JE kikowapi sasa?

Watu walisubiri neema waliyoahidiwa bila mafanikio, watu wakakata tamaa, kuonyesha machungu yao angalia idadi ya wapiga kura 2010, walijua kuwa kwa mfumo wa ccm hawatakubali kiongozi wao aongoze kwa muhula mmoja, kwa maana ingekuwa katika historia, wananchi walijua kuwa kwa gharama zozote Kikwete angerudi kwa muhula wapili, wakaona haina maana ya kupoteza muda wa kupiga kura, Sote tunajua nini kilichotokea, nchi yenye wananchi karibu milioni 50, na wapigakura karibu milioni 30, lakini raisi anaapishwa kwa kura milioni tano na laki mbili na ushee, hiki ni kichekesho cha karne. Serikali na tume ya uchaguzi wakaona sawa tu kwa kujitokeza wapiga kura milioni nane na laki sita na ushee tu, Hapo ukiondoa kura feki karibuni lakini saba kisha angalia idadi ya waliopitisha serikali hii.
 
Jee kwenye tafiti za TWAWEZA kapewa asilimia ngapi? Au ndio kaangukia kwenye lile kundi la Others lenye asilimia 1.3 kwa ujumla wao?
Kumtaja Mwigulu na Urais ni sawa na ujuha uliopitiliza.

Twaweza waliwashindanisha wagombea wanna toka CCM kwa utashi wao na Mwigulu hakuwa si miongoni mwao
 
Mkuu umenena huyu mtu ni laghai la karne! Ni hatare, weka mbali na watoto!

Wakati ninyi mnaendeleza matusi kwenye mitandao, mnararuana mchana kweupe, mnaendeleza makundi na mipasuko ya kichawi, CCM wanaendela kutulia na kupanga mashambulizi kisayansi. Mwigulu Nchemba mliyezoea kumsikia akitoa shutuma za 'kujilipua' sasa anatumia muda mwingi kufungua matawi ya chama na kuimarisha yale ya zamani, vijijini. Katika mikutano yake anazungumzia changamoto za ajira, umuhimu wa vijana kujituma na kuzifuata fursa na kuwaomba watanzania waendelee kukiamini chama hiki kilicholeta uhuru
 
Utakuwa umetumwa na shetani!:evil:

Wakati ninyi mnaendeleza matusi kwenye mitandao, mnararuana mchana kweupe, mnaendeleza makundi na mipasuko ya kichawi, CCM wanaendela kutulia na kupanga mashambulizi kisayansi. Mwigulu Nchemba mliyezoea kumsikia akitoa shutuma za 'kujilipua' sasa anatumia muda mwingi kufungua matawi ya chama na kuimarisha yale ya zamani, vijijini. Katika mikutano yake anazungumzia changamoto za ajira, umuhimu wa vijana kujituma na kuzifuata fursa na kuwaomba watanzania waendelee kukiamini chama hiki kilicholeta uhuru wetu
 
Uongo ni dhambi kwa maracya kwanza nlikua na mwona kama mlevi ila kwa sasa na mwelewa vzr na ni jambo jema Watanzania tumuunge mkono na kuzd kumwombea make anatufaa
Wakati ninyi mnaendeleza matusi kwenye mitandao, mnararuana mchana kweupe, mnaendeleza makundi na mipasuko ya kichawi, CCM wanaendela kutulia na kupanga mashambulizi kisayansi. Mwigulu Nchemba mliyezoea kumsikia akitoa shutuma za 'kujilipua' sasa anatumia muda mwingi kufungua matawi ya chama na kuimarisha yale ya zamani, vijijini. Katika mikutano yake anazungumzia changamoto za ajira, umuhimu wa vijana kujituma na kuzifuata fursa na kuwaomba watanzania waendelee kukiamini chama hiki kilicholeta uhuru wa taifa letu
 
Nakumbuka miaka hiyo udsm alikua akijulikana kama CHIEF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…