acer
JF-Expert Member
- Apr 4, 2012
- 1,595
- 142
Maoni yangu juu ya 'kura ya maoni' juu ya uongozi wa Kisiasa iliyotolewa na Twaweza: Jana niliandika kwenye twitter handle yangu kuwa ni ngumu kuita hii kitu ya Twaweza inayojulikana kama Sauti za Wananchi 'Utafiti', at best would call it 'opinion polls'. Nadhani sikueleweka. Kisayansi 'utafiti' ule unapungukiwa vigezo vingi sana kiasi cha kuzua maswali mengi kwa msomaji makini kufikia kuhoji uhalali na nguvu ya kitakwimu (statistical power) ya matokeo yake. Wengi hawakunielewa zaidi niliposema kuwa matokeo yake ni mazuri kwangu kwa kila hali, kama nikitazama 'utafiti' ule kwa 'ubinafsi' wangu. Nadhani nawajibika kutoa maelezo zaidi ili nisieleweke vibaya na kwa lengo la kuweka kumbukumbu sahihi.Jee kwenye tafiti za TWAWEZA kapewa asilimia ngapi? Au ndio kaangukia kwenye lile kundi la Others lenye asilimia 1.3 kwa ujumla wao?
Kumtaja Mwigulu na Urais ni sawa na ujuha uliopitiliza.
1. Kwanza ni kuwapongeza Twaweza kwa kuwa wabunifu katika kazi zao na kuamka kutumia njia za kisasa za kiteknolojia za kukusanya maoni ya wananchi kwa gharama nafuu na kwa haraka.
2. Kwa uelewa wangu utafiti una mapungufu makubwa kwenye namna watoa maoni wanavyopatikana kwenye tafiti hizi za twaweza zijulikanazo kama 'Sauti za wananchi'. Wamechaguliwa watu 2000 wakapewa simu bure na solar charger bure, halafu kila utafiti, kwenye kila issue huwa wanapigiwa hao hao kutoa maoni yao. Kwa utafiti huu waliotoa maoni ni 1445 kati ya walio katika mpango huu. Kuwapa hivyo vifaa kuna introduce ethical issues kwenye utafiti. Pia watafiti hawaelezi wanapataje watu 1445 kama ndiyo wawakilishi wa watanzania takriban milioni 45? Sampling frame ya 2000 ina sifa zipi na wanadhibiti vipi coverage bias na selection bias?
3. Pamoja na kwamba maoni ya hawa watu 1445 waliohojiwa hayakidhi vigezo vya kitakwimu vya kuwa generalizable kwa population yote, yanatoa mwangaza kuwa watanzania bado wana imani na CCM (chama changu), yanatoa picha kuwa kuna fursa pana kwa viongozi wa kizazi cha mabadiliko kuwania nafasi yoyote ile na kushinda kwa sababu, pamoja na umaarufu wa viongozi wa kizazi cha analogia, pamoja na kuwemo kwenye domain za umma kwa zaidi ya miaka 35, bado hawajaweza kuwashawishi watanzania kwa kiasi kikubwa! Kuna wengi kati yao hawajaamua wampe nani kura zao za Urais. Pia inatoa mwangaza kwamba kutakuwa na fursa pana kwa watu wapya kuingia majimboni na kutuamsha tuliopo sasa kukaa vizuri zaidi.
Japokuwa matokeo yanatupa moyo viongozi wapya kuendelea kujipanga, sitaki kutia wingu la 'ubinafsi' wangu kwenye maoni yangu kisayansi.
4. Ushauri kwa Twaweza: boresheni sampling technique ili ku-eliminate design biases na kuongeza authenticity, validity, reality na generalizability ya matokeo ya hizi tafiti zenu. Mkifanya hivyo mtakuwa mna tool nzuri sana ya utafiti wa kwenye jamii ambayo itasaidia sana kutupa taarifa wananchi na pia kuwezesha informed decision making.
Ahsanteni,
Dr. Hamisi Kigwangalla
Novemba 13, 2014.
Maoni yangu juu ya 'kura ya maoni' juu ya uongozi wa Kisiasa iliyotolewa na Twaweza: Jana niliandika kwenye twitter handle yangu kuwa ni ngumu kuita hii kitu ya Twaweza inayojulikana kama Sauti za Wananchi 'Utafiti', at best would call it 'opinion polls'. Nadhani sikueleweka. Kisayansi 'utafiti' ule unapungukiwa vigezo vingi sana kiasi cha kuzua maswali mengi kwa msomaji makini kufikia kuhoji uhalali na nguvu ya kitakwimu (statistical power) ya matokeo yake. Wengi hawakunielewa zaidi niliposema kuwa matokeo yake ni mazuri kwangu kwa kila hali, kama nikitazama 'utafiti' ule kwa 'ubinafsi' wangu. Nadhani nawajibika kutoa maelezo zaidi ili nisieleweke vibaya na kwa lengo la kuweka kumbukumbu sahihi.