Huyu ndiyo Bruce Lee

Huyu ndiyo Bruce Lee

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Bruce Lee aliweka rekodi ya dunia baada ya kupiga 'push up' 200 kwa kutumia vidole viwili vya mkono moja na kurusha punje ya mchele hewani na kuidaka kwa kutumia kijiti chembamba cha kulia chakula (chop stick).

Bruce Lee alizaliwa tarehe 27 november 1940 California, Marekani na alifariki tarehe 20 July 1973 Hong Kong akiwa na miaka 32.

Bruce Lee nguvu ya ngumi yake (punching force) ilikuwa na kilo 158 sawa na Mohammed Ali, lakini maajabu Bruce Lee alikuwa na kilo 58 na Mohammed ali kilo 117.

Bruce Lee alikuwa na uwezo wa kupiga ngumi tisa kwa sekunde moja, na ngumi yake ya inchi moja (one inch punch) ilikuwa na uwezo wa kumrudisha nyuma mita 5-6 mwanaume mwenye kilo 68.

Alikuwa na uwezo wa kupiga mateke tisa kwa sekunde moja, alipiga teke kiroba cha mchanga chenye kilo 135 na kuruka urefu wa futi tano kwenda juu. Alikuwa na uwezo wa kufungua kizibo cha soda kwa kutumia vidole viwili.

Aliweka rekodi ya dunia kwa kupiga 'push up' 1500 kwa mikono miwili bila kupumzika, 'push up' 400 kwa mkono moja, 'push up' 200 kwa kutumia vidole viwili vya mkono moja, na 'push up' 100 kwa kidole gumba cha mkono moja.

Bruce Lee alikuwa mchina wa kwanza kurekodi filamu Hollywood Marekani katika sanaa ya kupigana (martial arts). Bruce Lee pekee ndiye alievunja rekodi ya dunia mara kumi ndani ya miaka 2 tu.

FB_IMG_1668087683074.jpg
 
Chukuwa na hii Bruce Lee kwenye movie zake director kwenye production alilazimika kuziwekea slow motion kidogo kwa sababu ya speed ya Bruce Lee ingekuwa si rahisi kwa watanzamaji kuenjoy movie zake maana ingekuwa hazina tofauti na za Charlie Chaplin.

Bruce alifariki Hong Kong akazikwa Marekani, kaburi la Bruce Lee lipo Marekani.
 
Kwann hakuzikwa Hong Kong?
 
Back
Top Bottom