Huyu ndo msanii bora wa Tanzania mwaka 2016

Huyu ndo msanii bora wa Tanzania mwaka 2016

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Tukiangalia mwaka 2016 katika wasanii wa bongo fleva nani aliefanikiwa katika muziki wake na kuingiza pato kubwa mwaka 2016
Diamond platnumz huyu ndo msanii aliepata mafanikio zaidi Tanzania
Hizi ndio facts

- Mwezi wa kwanza Diamond alishinda tuzo kubwa nchini Nigeria za the Headies kama msanii bora wa mwaka non Nigerian

- Mwezi wa 2 diamond alishinda tuzo 2 za Hipipo nchini Uganda kama msanii bora wa Africa mashariki na wimbo bora wa africa mashariki kupitia wimbo wa Nana


- Kuanzia mwezi wa 3 hadi wa 5 diamond alifanya tour ya music wake US na Uerope akafanya shows zaidi ya 37 na kuingiza zaidi ya milioni 600
1481032811734.jpg


- Mwezi wa 5 diamond alichaguliwa kuingia kwenye tuzo za BET

- Mwezi wa 6 diamond aliingia mkataba na Vodacom wa kuwa balazo wao na kutengenenea matangazo yao. Diamond alilipwa zaidi ya milioni 600 na vodacom

- Mwezi wa 7 Diamond aliingia mkataba na Tomato Gold source na kulipwa zaidi ya milioni 160 na kutengeneza tangazo pia

-Mwezi wa 8 diamond aliingia mkataba na cocacola kutengeneza tangazo la Onja msisimko na kulipwa zaidi ya milioni 70

- Mwezi wa 9 diamond alifanya show nchini kenya kwa mwaliko wa chama cha ODM na kulipwa zaidi ya milioni 87

- Mwezi wa 10 diamond alishinda tuzo zaidi 7 kuanzia afrimma na eau usa

- Mwezi wa 11 diamond alianza kufanya ziara yake Africa kuanza nigria, malawi , mayotte pia alishinda tuzo 3 za afrima

- Mwezi 12 diamond alitangaza kulipwa zaidi ya bilioni 2 na lebal ya Universal music group na kuingia nao partnership ya kusambaza music wa WCB duniani
 
Ni mafanikio ya hali ya juu ukilinganisha na wanamuziki au wasanii wenzake hapa Tz na pengine East Africa. HONGERA ZAKE
AKAZE BUTI maana watu wana uchu wa kuona akianguka kimuziki.
 
Wasanii wengine wanakazi kubwa kumfikia huyu jamaa
 
Diamond hana mpinzani kwa Tanzania, kulinganishwa na wasanii wengine, nikutaka kusumbua akili tu kwa ubishi
 
ni mafanikio ya hali ya juu ukilinganisha na wanamuziki au wasanii wenzake hapa Tz na pengine East Africa. HONGERA ZAKE
AKAZE BUTI maana watu wana uchu wa kuona akianguka kimuziki.

Arudi tandale
 
Akitokea mtu anamtukuna mleta mada badala ya kujibu hizo facts atakua hajamtendea haki asee.
 
[emoji23] [emoji23] nimeuona ila nimejikaushaaaa.
Sitaki kutia neno hapa,naona vijana wake wa JF mmeamua kumuandalia tuzo yenu.
Hongereni[emoji6]
Nifah mgumu kukubali ukweli hasa ukiwa upande wa wcb [emoji1] [emoji1]
 
Back
Top Bottom