Huyu ni mmoja tu; hebu fikiria Watanzania 10 wangefanya hivi ni wawekezaji au wafanyabishara wangapi tungewavuta kuja hapa nchini?

Huyu ni mmoja tu; hebu fikiria Watanzania 10 wangefanya hivi ni wawekezaji au wafanyabishara wangapi tungewavuta kuja hapa nchini?

nashukuru siko tz.
mambo ya nchi yangu yalinichosha. kabla ya serikali watz wenyewe ni wana utapeli wa kishamba na uchawiuchawi
Ka upo USA nqsikoa watanzania bao wanapumilia mashine. Nina brother anatamani arudi. USA waanaoenda hatuoni wakiwa hata levo ya Manji.
 
Habari zenu wanajamii forum. Huku niliko, mimi ni mzima wa afya, na natumaini huko mlipo ni wazima pia kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Leo, katika pita pita mtandaoni, nikakutana na post ya bwana James ambayo kwa namna moja imenivutia sana na kunifanya nije hapa kuianzishia uzi, pengine tukapata lolote la kujifunza toka kwake kuhusu namna ya kutumia mitandao ya kijamii katika kulitangaza taifa letu la Tanzania.

Bwana James ameieleza Afrika na dunia juu ya kile kinachofanywa na jirani yetu, Kenya. Amesema kuwa, "Kenya imekuwa ikirangua parachichi kutoka Tanzania na kuyasafirisha nje ya Afrika, hali inayopelekea taifa hilo kutambulika kama wazalishaji na wasafirishaji wakubwa wa parachichi barani Afrika na duniani kwa ujumla. Hili limekuwa likifanyika pia katika uzalishaji wa nyama na maziwa."

Baada ya kupitia maelezo haya, nilishuka moja kwa moja sehemu ya maoni na nilifarijika sana na maoni ya mfanyabiashara mmoja wa parachichi kutoka Afrika Kusini ambaye alishukuru sana kwa taarifa hii, akidai kuwa imemfungua macho. Alikuwa akirangua parachichi kutoka Kenya na kuziingiza nchini Afrika Kusini, hali iliyompelekea kuingia gharama kubwa sana, ila sasa anatizamia kuanza kuzirangua kutoka Tanzania.

Ombi langu ni hili: Wote tumeona jinsi mtu mmoja alivyoweza kumvuta mfanyabiashara mmoja kuja nchini kwetu. Je, kila Mtanzania akitumia nafasi yake kufanya hivi, tungeweza kuvutia wawekezaji au wafanyabiashara wangapi?

Pia, kizazi cha Z, kizazi cha taarifa, kizazi cha sayansi na teknolojia, kizazi cha mitandao ya kijamii, badala ya kuingia huko na kufuatilia habari za WCB, Mwijaku na wengine, jamani tumieni nafasi hiyo pia kuandika chochote juu ya mazuri ya nchi yetu. Kama inakuwa ngumu, basi tumeni hata picha za Mlima Kilimanjaro. Kwa namna moja au nyingine, tutakuwa tumeitangaza nchi yetu na siyo kuiachia serikali pekee.

Asanteni.

View attachment 3043355
Haiwezi kusaidia wakati taasisi zimelala.
Usione wanahubiri exportation ukianza tafuta vibali huo mlolongo utakoma.
 
Tatizo mnapenda kulaumu tu serikali fahamu kuhusu mfumo wa capitalism unafanya kaz vipi? sis wananch ndo tunatakiwa tuanze serikali ije itusaidie..
 
Tatizo mnapenda kulaumu tu serikali fahamu kuhusu mfumo wa capitalism unafanya kaz vipi? sis wananch ndo tunatakiwa tuanze serikali ije itusaidie..
Sijaelewa,,, yani unamaana ya kuwa mfumo wa capitalism ndiyo unaruhusu exports za bidhaa ?? Huku wa kwetu ukikataaa ???

Yani ,,, mfumo wetu unashida gani labda ??
 
Us yupo top3 country zinazo produce crude oil. ila hawachimbi mafuta... wewe mwenyew unaweza kwenda kenya ukatafuta bidhaa yoyote ukapeleka nch yoyote na ukaitambulisha tz kwamba ndo wazalishaji. unakua middle man kama kenya... au kama USA learn to play game smart.. stop complain.
 
Serikali imewekeza kwenye kununua chawa wa kusifia viongozi badala ya kutangaza nchi kupitia ushawishi walionao mitandaoni, mimi nijitutumue kuelezea mazuri ya nchi ambayo muwekezaji akipatikana kodi zinarudishwa kufadhili chawa. Haya ni maajabu, kila mtu ashinde mechi zake, tule kulingana na urefu wa kamba zetu
Aaaah! Mkuu noma sana bongo hakuna siasa
 
Sina ila nimeishi nao hao wakulima. Mie nimelima viazi mviringo msharage nk. Naamini horticulture zinafanana. Mdudu anetisha sana ni kantangaze. Mvua nyingi na ukungu.
Mkuu nina mpango nilime nyanya za kifuku nina mpango nipande miche 50000 mtaji sio shida kwangu ila shida ni uzoefu na vijana wa kazi,vipi wapi naweza kuwapata vijana wa kazi wenye uzoefu na wachapa kazi nakilimo cha nyanya?mimi nipo mtwara
 
Uyo anae taka kuja Tanganyika aje lakini awacliane na wale wa India walio kujaga kununua korosho kisha wakakuta nn ndani ya magunia yao. All the best






KAZI ni kipimo cha UTU
Sasa huo ni udhaifu wa wizara na bodi ya korosho ambao wanatakiwa kuhakiki ubora kabla ya kupeleka nje hizo korosho. Now kuna vyama vya wakulima, ndiko ambako mnunuzi anatakiwa akanunue mazao, sio kwa walanguzi wa mtaani ambao ni wapigaji. Hata parachichi ni hivyo hivyo, inatakiwa zinunuliwe toka kwenye vyama vya wazalishaji vilivyosajiliwa.
 
Huwa sielewi shida yetu ni nini, Nchi yetu idadi ya wasomi inaongezeka kila Leo lakini ujinga hauiishi. Sisi tuna mazao ya biashara mengi sana lakini hatujui wapi tumekwama na serikali haijali.
Tatizo uoga wetu unawapa mileage watawala ,kivip?
Mkulima wa kawaida akitaka kutoa mazao nje ya nchi anakutana na msururu wa vibali na ukiritimba ambayo vinapitishwa na wale matapeli pale bungeni,ila sisi hatuwezi kunyanyua mdomo Wala mkono kupinga ujinga huo
Ni rahisi mkenya kuingiza mazao toka kwetu IL ni ngumu sana Kwa mtanzania kutoa mazao toka katavi kwenda Kenya.
Watu wachache wamejimilikisha kila kitu nchi hii huku wengi tukibakia hoi.
 
Usiwalaumu Kenya, sisi tumelala kwa sababu ya utawala mbovu na viongozi wetu si wabunifu wa lolote, wao wanakariri kila kitu kama ilivyo elimu yetu. Nchi yetu inachafuliwa sana kwa kuwa na viongozi useless kwenye idara nyeti, hawana msaada wowote kwa Mh. rais zaidi ya kuliibia taifa tu.
 
Makampuni kama ( tanzanice, eatfresh, avoafrica, avogroup, wintech.) yote yananunua parachichi na kuexport kupitia mgongo wa wakenya humo ndani huwezi kukuta mtanzania akiwa manager. Kibaya zaidi bei wanajipangia mfano mwaka huu walianza kwa kununua 1700tsh/kg mpaka 800tsh/kg. Watanzania yatupasa kuamka.
 
Mkuu nina mpango nilime nyanya za kifuku nina mpango nipande miche 50000 mtaji sio shida kwangu ila shida ni uzoefu na vijana wa kazi,vipi wapi naweza kuwapata vijana wa kazi wenye uzoefu na wachapa kazi nakilimo cha nyanya?mimi nipo mtwara
Kupata vijana ni changamoto kubwa. Mi nipo Njombe ila vijana wa hapa ni waswahili. Angalau upate wa Mbeya .
Ila vijana wa mbeya hawana utamaduni wa kukaa muda mrefu kwa Boss wanaogopa kugeuzwa ndondocha. Ukipata mundali>mmalila>mnyiha>msafwa>mnyakyusa. ujue umepata mtu wa kazi, zingatua hio alama > Fanya juu chini tafuta mundali. Ishu kubwa ni malipo.
Wandali huwa wanamalengo hawaji tuu.
Weka hesabu atalima kwa sh. ngapi, atapanda jwa sh.ngapi, atapskilia kwa sh.ngapi atahudumia kwa sh. Ngapi.
Mundali.
Ninayo vonnectoon na wandali ils sitaki waje wanilaumu, unatakiwa uwe serious wale watu ni watu wa kazi sio masihara ya kazi.
Hihuo ikiweka hesabu chini nainus simu ndani ya wiki utawapata. Kazi kwako.
lakini nasikia wagogo ba watu wa singida wanadumu kwenye nao wanaweza kazi ika sijaoata kuwaona.
Jirani ya shamba hapa kuna kijana wa kichaga, yeye anafanya kazi kwa ndugu yake. Nadhani sijawahi ona mchaga anafanya kazi kama huyu dogo, amewahi taka kunifanyia connection kwa mwenzake.
Unaweza pata hawa watu ika uwe serious na usiwe na mkono wa birika kwenye malipo na huduma. Watu wa Mbeya lazima uwape Chakula cha kutosha sio cha mawazo kwao kuna chakula hivyo usiwabanie kula.
Pm kwa taarifa zaidi.
 
Mkuu nina mpango nilime nyanya za kifuku nina mpango nipande miche 50000 mtaji sio shida kwangu ila shida ni uzoefu na vijana wa kazi,vipi wapi naweza kuwapata vijana wa kazi wenye uzoefu na wachapa kazi nakilimo cha nyanya?mimi nipo mtwara
Uzoefu di hata humu watu wameandika sana. Taarifa za wengine ni uzoefu tosha. Hakuna maajabu kwenye kilimo chochote ndio maana drs 7 akifeli anaenda kulima.
Jiunge magroup ya wakulima.
Kilimo kigumu cha nyanya kipo huku kwa sababu mvua ni nyingi mno, huko mtwara uta enjoy.
Huku miezi hii kuna Ukungu mtwara hamna. Kwa hio jipange tu andaa mazingira. Project yako mshirikishe bwana shamba akupe ushautri, usisahau wakulima wa karibu.
Zingatia :
Mbegu
Mbolea
Sumu za wadudu
Wanyama wezi kama ngedere
Wezi binadamu
Wachawi
Rutuba ya shamba japo inaweza boreshwa
Maji.
Umbali wa shamba lilipo
Wanunuzu wako ni kina nani.
Ubora wa nyanya. Mfano Njombe na Iringa ndio ze ye ardhi bora ya nyanya ikifuatia Mbeya, je nyanya yako itaweza shindaba na ya Njombe sokoni ?.
Zingatia muda wa kuanza kulima.
Unapoamua kulima kifuku ujipanga sio kitoto, na hasa kwa mazao ya bustani.
Ukitaka zaidi naweza kuku connect na wakulima wenye uzoefu. Vile vile tutashare ideas maana nami nawatika mbegu kuanzia wanane kwenda mbele.
Jdmbo lingine weka segment or portion usisie mbegu zote kwa mpigo. Sia awamu tatu ili kukwepa RISK .
Kingine kama maeneo yatakuwa tofauti itapendeza, hii nimejifunza kwenye viazi mviringo.Usiweke project yako kwenye eneo moja ikitokea dhoruba unapoteza mazima.
 
Ni soko huria. Hata nyie wabongo hamkatazwi kuuza bidhaa nje ya nchi tatizo lenu kila mtu anawaza fremu tu auze nguo, viatu na mikoba.
 
Back
Top Bottom