Tangantika
JF-Expert Member
- Aug 12, 2018
- 5,586
- 7,087
Ka upo USA nqsikoa watanzania bao wanapumilia mashine. Nina brother anatamani arudi. USA waanaoenda hatuoni wakiwa hata levo ya Manji.nashukuru siko tz.
mambo ya nchi yangu yalinichosha. kabla ya serikali watz wenyewe ni wana utapeli wa kishamba na uchawiuchawi
Haiwezi kusaidia wakati taasisi zimelala.Habari zenu wanajamii forum. Huku niliko, mimi ni mzima wa afya, na natumaini huko mlipo ni wazima pia kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.
Leo, katika pita pita mtandaoni, nikakutana na post ya bwana James ambayo kwa namna moja imenivutia sana na kunifanya nije hapa kuianzishia uzi, pengine tukapata lolote la kujifunza toka kwake kuhusu namna ya kutumia mitandao ya kijamii katika kulitangaza taifa letu la Tanzania.
Bwana James ameieleza Afrika na dunia juu ya kile kinachofanywa na jirani yetu, Kenya. Amesema kuwa, "Kenya imekuwa ikirangua parachichi kutoka Tanzania na kuyasafirisha nje ya Afrika, hali inayopelekea taifa hilo kutambulika kama wazalishaji na wasafirishaji wakubwa wa parachichi barani Afrika na duniani kwa ujumla. Hili limekuwa likifanyika pia katika uzalishaji wa nyama na maziwa."
Baada ya kupitia maelezo haya, nilishuka moja kwa moja sehemu ya maoni na nilifarijika sana na maoni ya mfanyabiashara mmoja wa parachichi kutoka Afrika Kusini ambaye alishukuru sana kwa taarifa hii, akidai kuwa imemfungua macho. Alikuwa akirangua parachichi kutoka Kenya na kuziingiza nchini Afrika Kusini, hali iliyompelekea kuingia gharama kubwa sana, ila sasa anatizamia kuanza kuzirangua kutoka Tanzania.
Ombi langu ni hili: Wote tumeona jinsi mtu mmoja alivyoweza kumvuta mfanyabiashara mmoja kuja nchini kwetu. Je, kila Mtanzania akitumia nafasi yake kufanya hivi, tungeweza kuvutia wawekezaji au wafanyabiashara wangapi?
Pia, kizazi cha Z, kizazi cha taarifa, kizazi cha sayansi na teknolojia, kizazi cha mitandao ya kijamii, badala ya kuingia huko na kufuatilia habari za WCB, Mwijaku na wengine, jamani tumieni nafasi hiyo pia kuandika chochote juu ya mazuri ya nchi yetu. Kama inakuwa ngumu, basi tumeni hata picha za Mlima Kilimanjaro. Kwa namna moja au nyingine, tutakuwa tumeitangaza nchi yetu na siyo kuiachia serikali pekee.
Asanteni.
View attachment 3043355
sipo US wala sitaki kupasikia.Ka upo USA nqsikoa watanzania bao wanapumilia mashine. Nina brother anatamani arudi. USA waanaoenda hatuoni wakiwa hata levo ya Manji.
Sijaelewa,,, yani unamaana ya kuwa mfumo wa capitalism ndiyo unaruhusu exports za bidhaa ?? Huku wa kwetu ukikataaa ???Tatizo mnapenda kulaumu tu serikali fahamu kuhusu mfumo wa capitalism unafanya kaz vipi? sis wananch ndo tunatakiwa tuanze serikali ije itusaidie..
Aaaah! Mkuu noma sana bongo hakuna siasaSerikali imewekeza kwenye kununua chawa wa kusifia viongozi badala ya kutangaza nchi kupitia ushawishi walionao mitandaoni, mimi nijitutumue kuelezea mazuri ya nchi ambayo muwekezaji akipatikana kodi zinarudishwa kufadhili chawa. Haya ni maajabu, kila mtu ashinde mechi zake, tule kulingana na urefu wa kamba zetu
Mkuu nina mpango nilime nyanya za kifuku nina mpango nipande miche 50000 mtaji sio shida kwangu ila shida ni uzoefu na vijana wa kazi,vipi wapi naweza kuwapata vijana wa kazi wenye uzoefu na wachapa kazi nakilimo cha nyanya?mimi nipo mtwaraSina ila nimeishi nao hao wakulima. Mie nimelima viazi mviringo msharage nk. Naamini horticulture zinafanana. Mdudu anetisha sana ni kantangaze. Mvua nyingi na ukungu.
Sasa huo ni udhaifu wa wizara na bodi ya korosho ambao wanatakiwa kuhakiki ubora kabla ya kupeleka nje hizo korosho. Now kuna vyama vya wakulima, ndiko ambako mnunuzi anatakiwa akanunue mazao, sio kwa walanguzi wa mtaani ambao ni wapigaji. Hata parachichi ni hivyo hivyo, inatakiwa zinunuliwe toka kwenye vyama vya wazalishaji vilivyosajiliwa.Uyo anae taka kuja Tanganyika aje lakini awacliane na wale wa India walio kujaga kununua korosho kisha wakakuta nn ndani ya magunia yao. All the best
KAZI ni kipimo cha UTU
Tatizo uoga wetu unawapa mileage watawala ,kivip?Huwa sielewi shida yetu ni nini, Nchi yetu idadi ya wasomi inaongezeka kila Leo lakini ujinga hauiishi. Sisi tuna mazao ya biashara mengi sana lakini hatujui wapi tumekwama na serikali haijali.
Kupata vijana ni changamoto kubwa. Mi nipo Njombe ila vijana wa hapa ni waswahili. Angalau upate wa Mbeya .Mkuu nina mpango nilime nyanya za kifuku nina mpango nipande miche 50000 mtaji sio shida kwangu ila shida ni uzoefu na vijana wa kazi,vipi wapi naweza kuwapata vijana wa kazi wenye uzoefu na wachapa kazi nakilimo cha nyanya?mimi nipo mtwara
Uzoefu di hata humu watu wameandika sana. Taarifa za wengine ni uzoefu tosha. Hakuna maajabu kwenye kilimo chochote ndio maana drs 7 akifeli anaenda kulima.Mkuu nina mpango nilime nyanya za kifuku nina mpango nipande miche 50000 mtaji sio shida kwangu ila shida ni uzoefu na vijana wa kazi,vipi wapi naweza kuwapata vijana wa kazi wenye uzoefu na wachapa kazi nakilimo cha nyanya?mimi nipo mtwara