Huyu ni mwanaume mkweli?

Huyu ni mwanaume mkweli?

AUNT HAPPY

Member
Joined
Mar 29, 2013
Posts
10
Reaction score
1
Habari zenu ndg wanajf napenda kuwapongeza hii ni mara ya kwanza kuandika huku naomben ushauri.mm n dada wa miaka 31 nimeajiriwa.niliolewa na kupata mtt bahat mbaya mume wangu hakuwa riziki kwan alipoteza uhai kwa ajali ya gari alipokuwa safarini 2009. Baada ya hapo niliamua kutulia mwenyewe.mwaka jana 2011 nilipata mwanaume ambae nae alikuwa ametengana na mkewe kwa muda. Nae alinieleza mambo mengi nami tukakubaliana kuishi pamoja. Sasa tumekaa kwa muda wote huo tukiwa wapenzi lkn kinachonishangaza huyu kaka anaishi na dada yake.na chumba cha huyu kaka huwa hafungi mlango wake wa chumban na dada yake huwa anaingia chumban humo kama kwake na huwa anakifanyia usafi chumba cha kaka yake huyo na wakati mwingine huwa kama kaka yake hayupo huwa analala ktk kitanda hicho.sasa nikimueleza mwanaume huyu yy ananiambia nimueleze na mm namuogopa maana huwa siishi hapo.kingine huwa nasoma evening class sasa mwanaume huyu anataka pale nitokapo class anataka nikishatumia vyombo nijiyahid niwe naviosha.na hapo niamkapo niwe najitahid kufanya usafi ndani ndio niende kazini najikuta nafanya ila wakati mwingine najikuta nachelewa kulala hivyo inabidi nimuombe dada yake anisaidie maana yy yupo nyumban tu.sasa kinachonipa hofu kila nikimuuliza kuuhus mpango wa kwenda kujitambulisha home yy anadai bado muda na sasa tumeshakuwa wapenz kwa muda miez saba lkn yy anadai tusomane kwanza je huyu mwanaume ananifaa
 
Kuwa mpole tu dada Furaha, mapenzi hayana formula inayofanana unaweza kusema miezi 7 ni mingi kumbe kwenye mazingira mengine ni michache sana. Umeeleza kwa urefu ila sijaelewa kama kwa sasa mnaishi pamoja au kila mtu kwake? Mnaishi pamoja na huyo dada ya mume mtarajiwa kwa sasa au mume anaishi na dada na wewe upo kwako? Anyway, take your time dada yangu, kama ni wako atakuwa wako tu la muhimu wewe play your part, kama kwa kumuheshimu, huo usafi anaotaka, mapenzi ya kweli na kadhalika. Kama unampenda na unadhani anafaa kuwa mume stahiki huna haja ya ku-rush, tekeleza wajibu wako.
 
kuishi mmm bado naishi kwangu ila wakati mwingine ndio huwa naenda hapo kwake na yy huwa anakuja kwangu na huyo kaka yy ndie anaishi na dada yake huyo
 
hapo unagegedwa tuu....alafu chunguza kama kweli huyo ni sista.
 
kweli wanaume hawafai...
dada wa watu kazunguka na maneno wee,kumbe shida ni kutokujua ni lini na yeye atakua tena mke wa fulani? mnh

ukiendelea ku nag ndio kabisaa utaonekana desperate,uchune tu huyu anakupotezea muda,kama unataka mume omba kwa mungu,kisha jichanganye kwenye mikutano na sehemu nyingine za kukutana utampata tu mtu.....huyo wa sasa hana msimamo .......
kuwa na msimamo usiwe door mat,jua unataka nini kwa mwanaume,jiamini and go for it,hapo umesema hajali saa nyingine umechoka pamoja na shule yako hii inaonyesha alivyo selfish ila kwa upande mwingine labda ana hofu umemzidi kila kitu wanaume bwana soo unpredictable ila mie hapo ningepaacha fasta:A S 39:
 
Nashukurun sana kwa ushaur. kwanza ni mtu ambae hana hata chembe ya shukran kwasababu yy huwa anampa huyo dada pesa za matumiz hapo nyumban ili aweze kununua vitu vya kumaliza mwez lkn utajikuta siku ya siku vile vitu alivyonunua dada yake havimalizi mwezi na hukuta ananipigia cm kuwa vitu ndani vimeisha lkn kwa kuwa na mm nina huruma huwa nawanunulia vitu hivyo ili wakamilishe mwez lkn yy hanaga asante hata siku moja hata ya kudanganyia tu.ukweli hata mm nimechoka na huyu baba
 
Nashukurun sana kwa ushaur. kwanza ni mtu ambae hana hata chembe ya shukran kwasababu yy huwa anampa huyo dada pesa za matumiz hapo nyumban ili aweze kununua vitu vya kumaliza mwez lkn utajikuta siku ya siku vile vitu alivyonunua dada yake havimalizi mwezi na hukuta ananipigia cm kuwa vitu ndani vimeisha lkn kwa kuwa na mm nina huruma huwa nawanunulia vitu hivyo ili wakamilishe mwez lkn yy hanaga asante hata siku moja hata ya kudanganyia tu.ukweli hata mm nimechoka na huyu baba

mwanzo nilishindwa kuchangia,ila kwa sasa umeongeza haya maelezo,nakuambia HAKUFAI! nakushauri soma kwa bidiii,mimi naamini uliyeandikiwa na mungu atakuja siku ambayo umepangiwa ila omba mungu
 
Back
Top Bottom