.
Bahati mzuri Tanzania bado hatuna cyber law, ndio maana hata yule Mzee wa Ze Uta.. hata angekamatwa Tanzania, sijui tungemshitaki kwa sheria ipi.
Mambo ya Internet yamegusiwa kwenye sheria mpya za Anti Money Laundering na Terrorism Act huku hatuna any basic legistlation kuhusu internet. Hivyo kitanzania kosa ni kutukana kwa sauti na watu wasikie, kuchapisha print na watu wa wasome, au kubroadcast matangazo watu wasikie, hili la kubandika humu sio kosa kisheria.
Ila pia nakubaliana na wewe, ustaarabu ni kitu muhimu kwa heshima ya JF, baadhi ya wachangia muhimu hufikia wakati wakaidharau JF na kuachana nayo, japo naamini bado wanaingia kama guest.
Toka kufungwa kwa ile Ze Uta.., members wa JF wameongezeka kwa kasi na kunawakati unafungua unatafuta topic ya maana, unakosa, unaishia kufunga.
Kwa vile hili ni jukwaa huru, tunawajibika kuheshimu mawazo ya kila mtu, ila pia tunaweza kuweka code of ethics on 'right to privacy' ili JF isitumiwe kama tool ya 'character Assasination' at the moment, there is nothing JF can do for now, just go on to 'take the bitter with the sweet' ila naamini huko mbele, we can do something.
JF Idumu.