Huyu Pasta Dominiki 'Nabii Kiboko ya Wachawi' ni nani? Nguvu yake ni ya Kweli? Siyo Msanii kama wa Kawe na Kimara Temboni?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kwa Nyomi Kubwa alilonalo sasa na Nyota yake inavyoanza Kungaa huku Akipendwa na Kukubalika zaidi kwakuwa huwa Habahatishi kwa Kukutajia Mbaya wako (hata kama ni Mzazi au Nduguyo) huku Akiwaumbua na Kukutajia Wachawi wako na akikuombea na kufanikiwa hawa wa Kawe na Kimara Temboni wasipomkalia Kikao cha Dharura anaenda Kuwapokonya Waumini Wao wote.

Yuko (Anapatikana) Buza kwa Lulenge na siyo kule Buza kwa Mpalange ambako wengi tunakupenda na tunakujua kwakuwa 95% ya Warembo (Mademu) wa huko Wewe Mwanaume usipopita nao na Gari lako Vumbi / Rough Road watakudharau na kukucheka mno huku wakiona ni Mshamba (Mgaigai) mtupu tu.

Haya Kazi Kwenu sasa Kufunguka!
 
Nipo Ethiopia naelekea Nigeria........
Subiri nirudi bongo,nitawakalisha wote na kuwapora watoa sadaka wao!!
 
Kadri Injili inavyohubiriwa kwa kweli na kwa hira, ndivyo tunavyouendea mwisho wa dunia. Yesu alipoulizwa dalili za nyakati za mwisho ni zipi? Moja ya dalili alisema Injili itahubiriwa kwa kila kiumbe.

Nafikiri kila Mkristo anapaswa kusoma vizuri neno la Mungu kisha kumruhusu Roho amfafanulie neno na kuomba neema ya Mungu ya kumfanya abadilike kupitie hilo neno. Ni wakati sasa kila wakati kuomba rehema mbele za Mungu kila wakati.
 

Anawakimbiza wote hapa mjini jamaa kuponya ni Dk zero

USSR
 
Genta huyu nabii nimekutana na msafara wake siku chache zilizopita wakigawa maji kwa watu njiani. Anatembea na coaster iliyojaa wasaidizi wake (warembo pisi kali) na akiambatana na canter ya wazi iliyosheheni katoni za maji. wanafika sehemu wanasimama dk 5 hivi wanagawa maji kisha wanasepa. Gari ya bombastic sound huwa ni sehemu ya msafara

Watu wengi sana wametokea kumuamini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…