GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Alikuwa na mambo mengi na Vituko vingi tu ila binafsi nakumbuka kila alipokuwa akienda katika Vijiwe vya Masela wa enzi hizo wenyewe Masela walikuwa wanapiga Magoti na wanajisalimisha Kwake na ama Bangi walizokuwa nazo na Vitu vya Uwizi walivyoiba na walikuwa wakiongoza wenyewe Kituoni Polisi.
Marehemu Nkama Sharp ndiyo alikuwa Polisi pekee Jijini Dar es Salaam ambaye alikuwa hata akikukamata humbishii, unamtii na kweli hata Wewe mwenyewe unaamini kuwa ulikosea. Na alikuwa ni Polisi ambaye hana Uonevu na kuna muda alikuwa akiona unataabika au huna Msaada Kituoni basi anaweza Yeye kwa Huruma yake akakusaidia tena bila hata ya Kumpa Rushwa na ukatoka na hata ukitoka ulikuwa hurudii tena Makosa au Uhalifu.
Alikuwa na Uwezo wa Kipekee na Kipaji cha namna yake ambacho leo hii ni Nadra sana kukiona kwa Mapolisi wengi wa miaka hii ya sasa. Na nina uhakika kwa jinsi alivyokuwa Mweledi na ana Msimamo kama angekuwepo hadi miaka hii ya sasa kuna baadhi ya Maandamano ya Kisiasa wala asingekuwa anaiingilia au kuwasumbua Watu tofauti na Polisi wa sasa ambao kila Kukicha wao wanasema kuwa huwa wanatekeleza Maagizo kutoka Juu ( siyo Mbinguni kwa Mungu Baba )
Nashauri kama ikiwezekana Jeshi la Polisi nchini Tanzania litafute namna ya Kumuenzi huyu Marehemu Nkama Sharp ambaye Binafsi pia nakumbuka aliwahi kutufanya Mimi na baadhi ya Wenzangu tugawane Mitaa ile ya Jirani na Shule ya Muhimbili kwa Kumkimbia baada ya Kuambiwa kuwa tulikuwa tunafanya Fujo katika Mechi moja tuliyocheza na Wababe wa miaka hiyo Shule ya Tambaza na nakumbuka katika hali ya Kumkimbia niliweza Kupoteza Kiatu changu cha Mguu wa Kushoto na nilipofika Nyumbani nilipewa Kipigo cha maana ila nikashukuru kuwa ni bora nimepigwa na Wazazi kuliko ningeishia Mikononi mwa Marehemu Nkama Sharp.
Nasisitiza tena Marehemu Nkama Sharp aenziwe tafadhali na Mapolisi wa sasa hebu muigeni huyu Afande ili nanyi tuwapende.