Kwa kweli miaka ya 80s mpaka 90 kulikuwa Askari Polisi waliokuwa na mbinu za kusambaratisha vigenge vya wahalifu yaani kwa kupita tu kwenye mitaa, wale masela wa miaka hiyo waliokuwa wakivuta jani vijiweni walikuwa wakikimbia wenyewe.Nakumbuka pale Arusha kulikuwa na Polisi mmoja alikuwa anafahamika kwa jina la Kimaro maarufu sana kwa jina la "SABA SITA" huyu jamaa hakuwa tofauti na marehemu Mkama Sharp. Pale Arusha miaka hiyo hakuna mtu ambaye alikuwa hamjui "SABA SITA". Kiukweli huyu askari alikuwa very smart katika kazi yake kwanza alikuwa anaipenda. Nakumbuka pale Sheikh Amri Abeid Stadium kulikuwa na mechi ya ligi kuu kati ya Simba SC na Ndovu FC ya Arusha, kwa baadhi ya wapenzi wa soka walikuwa wakiruka ukuta kuingia uwanjani kwa kukosa kiingilio,sehemu nilipokuwa nimekaa wakaja kukaa jamaa watatu walioruka ukuta kumbe Saba Sita alikuwa amewaona akapotezea kama hajawaona, wale washkaji wakajisahau. Kumbe "7 6" alikuwa anawalia timing, Simba ilipata goli la kuongoza lililofungwa na marehemu Edward Chumila uwanja mzima ulizizima kwa kushangilia lile goli, muda huo sasa Saba Sita akiwa amevalia pama lake la FFU, pingu, kirungu na kiunoni akiwa na pistol iliyokuwa kwenye kasha lake alikuja mpaka pale nilipokuwa nimekaa akawachomoa wale jamaa watatu walioruka ukuta sio siri jamaa waliingia hofu kubwa, akaanza kuzunguka nao uwanja mzima akiwa amewafunga mashati yao kwa kuwaunganisha alipofika nao kwenye Defender la Polisi aliwaamuru wapande ndani na walale kifudi fudi, hiyo ndio ilikuwa adhabu yao hawakuwapiga hata kidogo mpira ulipokwisha aliwaachia. Baadae nasikia Saba Sita alihamishiwa Mererani kikazi na kisha alihamishiwa tena CCP kuwa Mkufunzi. Nowadays sijui alipo nadhani atakuwa amestaafu.Lakini niconclude kwa kusema Mkama Sharp na Saba Sita ni Polisi waliokuwa very professional katika kazi yao.