Huyu Polisi wa zamani Marehemu Mkama Sharp alikuwa na Kipaji gani ambacho Polisi wengi wa sasa hawana?

Huyu Polisi wa zamani Marehemu Mkama Sharp alikuwa na Kipaji gani ambacho Polisi wengi wa sasa hawana?

Arusha alikuwepo SABASITA KIMARO. Niliwahi kumuona alfajiri miaka ya 90 amedhibiti vibaka wasiopungua kumi pale around about kaloleni vibaka wanapelekwa kituoni kwa kwata na amri za kufa mtu huku wote wajaa vumbi hawafai tena!
 
Kuna Siku moja nikiwa pale pale Shamba la Bibi ( Taifa ) huku nikiwa bado ni Mdogo kabisa Kipindi kile Katibu Mkuu wa Simba SC alikuwa Mzee Mmoja Mbabe sana ( sasa Marehemu ) Priva Mtema niliwahi Kuona Mbwa wa Mkama Sharp akiondoka na Kipande cha Nyama cha Tako la Kushoto la Mhalifu na sina uhakika kama alipona ile Siku au alikufa baadae.
Daaah nimecheka utafikiria mazuri
 
Aisee! kumbe Tunda ni mtoto wa Kimaro a.k.a "SABA SITA" mbona sasa binti machepele sana mzee ameshindwa kum-discipline ?
Si ndio hapo yaani kabinti ni kama kamempiga bao msure wake.
Any way labda Ni mapenzi ya kupitiliza kwa watoto. Au mama yake binti ndio tatizo.
Changamoto Sana sifa zote za mdingi zinaweza kuharibiwa na mtoto
 
Si ndio hapo yaani kabinti ni kama kamempiga bao msure wake.
Any way labda Ni mapenzi ya kupitiliza kwa watoto. Au mama yake binti ndio tatizo.
Changamoto Sana sifa zote za mdingi zinaweza kuharibiwa na mtoto
Acha tu, dingi na undava wote lakini kashindwa kudhibiti kale kabinti.
 
Acha tu, dingi na undava wote lakini kashindwa kudhibiti kale kabinti.

Watoto wa Kike wana Changamoto zao Kiongozi na ukijifanya unamfuatilia sana utaishia kuambiwa ama unatembea nae au uko mbioni kutembea nae.
 
MSITAJE SANA WATOTO
KUNA WATOTO WENGINE AWAJAJULIKANA RASMI JAMAN KWENYE NDOA ZA WAZAZI WAOO MTAVUNJA ALTARE ..KAMA UNAHAKIKA ANAISHI KWA WAZAZI RUKSA ..ILA KAMA AMNA UHAKIKA MTAVUNJA MADHABAHAU WAPENDWA WENGINE TUMEWEKA SIRI MPAKA SASA INGAWA NDUGU WANAJUA...
TUWASITIRI
 
Sharp na mbwa wake (mbwa wa polisi).

Si mara 1 au mara 2 niliwahi kumwona Sharp akiwa na mbwa. Kuna wakati angemwacha mbwa karibu na geti la kuingia kwenye Uwanja wa Taifa wa zamani (shamba la bibi) bila kumfunga popote.Angemwamrisha "tulia hapa hadi nikukute, usiondoke!" na mbwa angatulia hapo. Hata akikuona unajipenyeza getini kiwizi wizi au unajaribu kuruka ukuta mbwa huyo asingekuwa na time na wewe.

Ila ole wako aamrishwe kukukamata ndo utaisoma namba.Afande Sharp angemwelekeza mbwa wake " unamwona yule jamaa aliyevaa kofia ya blue, t-shirt nyeupe na jeans ya blue?nenda kamkamate!" Ni hivi mbwa angekusonga wewe tu aliyeelekezwa akukamate (hata kama uko kwenye kundi la watu wengi, na angekukamata).

Iliwahi kutokea afande Sharp alimsakizia mbwa msela mmoja aliyekuwa anajaribu kupita chini ya geti, jamaa alivyoona atadakwa ikabidi akimbilie kwenye kambi ya jeshi ya Abdallah Twalipo (almaarufu 'Ngome') iliyo jirani kabisa na Uwanja wa Taifa na kituo cha mafuta. Jamaa alivyoingia kambini, wazee wa JWTZ waliokuwa zamu walimlinda na kumwambia asiwe na hofu, walichofanya ni kumsubiri mbwa aingie kambini kisha wamfanyie mambo ya Samson na Simba wa Wafilisti. Ila yule mbwa alikuwa na akili bhana, alifunga breki getini na kurudi kwa boss. Wajeda wakamwambia Sharp "huyo mbwa wako na wewe mwenyewe leo tulitaka tuwafundishe adabu.Rudia tena uone". Sharp hakujibu neno.

Ila huyu Pot alikuwa tishio kwa wahuni kwakweli.Kuna mtoto yupi wa mjini ambaye hakumfahamu?
kwaiyo dog akajua nikiingia hum wazee wa kaz watanifanya ndivyo sivyo dah ejikuta nacheka sana
 
Back
Top Bottom