GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
- Thread starter
- #21
Mambosasa mkuu lol
Huyu uliyemtaja hapa ni Mweupe ( Mchovu ) sana Kiongozi ukimlinganisha na Marehemu Nkama Sharp.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mambosasa mkuu lol
Na hakuishia tu kuwa na Mikwara kama ambavyo unamdhihaki hapa Kiongozi ila Jamaa ( Mrehemu Nkama Sharp ) pia alikuwa ni Mwana Karateka mzuri na mahiri sana tu. Vijana wengi wa miaka hii ya sasa mnajifanya mna Usela ila labda niwaambieni tu kuwa miaka yetu hiyo ambayo tulikuwa na akina Nkama Sharp ndiyo kulikuwa na Wahuni na Masela Wabobezi kabisa ila wote hao walikuwa wakikalishwa na Marehemu Nkama Sharp na wanatulia tuli. Ninaposema huyu Askari alikuwa si Mtu wa kawaida ndiyo namaanisha hivi.
Wewe kama tu Wavuta Bangi wa zamani Vijiweni wakipewa tu Signal kuwa Marehemu Nkama Sharp ameamka Kitini Kwake Ofisini na anaenda Kuvitembelea hivyo Vijiwe Kukamata Watu ndani ya Sekunde 7 au dakika 1 tu ulikuwa huoni Mtu Kijiweni bali unaona tu Vumbi huku kila Msela akilitafuta Boda la kwenda Kwao.
Nakumbuka kuna Siku moja Marehemu akiwa Full Mkoko kapigilia Kiaskari kabisa alitoka Baru / Mita ( alikimbizana ) na Mhalifu kutoka Kariakoo hadi maeneo ya Msasani jirani na ulipokuwa Uwanja wa Mpira wa Magunia na Yule Mhalifu kwa Kuchoka ilibidi asalimu Amri kwani alikuwa kila akikata Kona anamuona Mwanamume Nkama Sharp yuko Matakoni mwake.
Jamaa ( Mhalifu ) alipochoka na Kukaa chini Marehemu alikuja na kumuinua na Kumwambia waendelee na Marathon yao ambayo haikuwa rasmi na kilichotokea Yule Mhalifu sijajua kama alikuwa amechoka kweli au alikuwa anatafuta tu Huruma ambapo alijinyea / alikunya pale pale ndipo Afande Nkama Sharp nae akaamua Kuachana nae ili asije Kunuka Mimavi bure.
Kwa taarifa tu mtoto wake yupo ni askari ana cheo inspectaAlikuwa na mambo mengi na Vituko vingi tu ila binafsi nakumbuka kila alipokuwa akienda katika Vijiwe vya Masela wa enzi hizo wenyewe Masela walikuwa wanapiga Magoti na wanajisalimisha Kwake na ama Bangi walizokuwa nazo na Vitu vya Uwizi walivyoiba na walikuwa wakiongoza wenyewe Kituoni Polisi.
Marehemu Nkama Sharp ndiyo alikuwa Polisi pekee Jijini Dar es Salaam ambaye alikuwa hata akikukamata humbishii, unamtii na kweli hata Wewe mwenyewe unaamini kuwa ulikosea. Na alikuwa ni Polisi ambaye hana Uonevu na kuna muda alikuwa akiona unataabika au huna Msaada Kituoni basi anaweza Yeye kwa Huruma yake akakusaidia tena bila hata ya Kumpa Rushwa na ukatoka na hata ukitoka ulikuwa hurudii tena Makosa au Uhalifu.
Alikuwa na Uwezo wa Kipekee na Kipaji cha namna yake ambacho leo hii ni Nadra sana kukiona kwa Mapolisi wengi wa miaka hii ya sasa. Na nina uhakika kwa jinsi alivyokuwa Mweledi na ana Msimamo kama angekuwepo hadi miaka hii ya sasa kuna baadhi ya Maandamano ya Kisiasa wala asingekuwa anaiingilia au kuwasumbua Watu tofauti na Polisi wa sasa ambao kila Kukicha wao wanasema kuwa huwa wanatekeleza Maagizo kutoka Juu ( siyo Mbinguni kwa Mungu Baba )
Nashauri kama ikiwezekana Jeshi la Polisi nchini Tanzania litafute namna ya Kumuenzi huyu Marehemu Nkama Sharp ambaye Binafsi pia nakumbuka aliwahi kutufanya Mimi na baadhi ya Wenzangu tugawane Mitaa ile ya Jirani na Shule ya Muhimbili kwa Kumkimbia baada ya Kuambiwa kuwa tulikuwa tunafanya Fujo katika Mechi moja tuliyocheza na Wababe wa miaka hiyo Shule ya Tambaza na nakumbuka katika hali ya Kumkimbia niliweza Kupoteza Kiatu changu cha Mguu wa Kushoto na nilipofika Nyumbani nilipewa Kipigo cha maana ila nikashukuru kuwa ni bora nimepigwa na Wazazi kuliko ningeishia Mikononi mwa Marehemu Nkama Sharp.
Nasisitiza tena Marehemu Nkama Sharp aenziwe tafadhali na Mapolisi wa sasa hebu muigeni huyu Afande ili nanyi tuwapende.
Sio kukukamata unaongozana,aliua na uwezo wa kukuambia nikukute kituoni na masela wanatangulia wenyewe kituoni,mimi binafsi nilikutana naye osterbay polisi wakati huo ni staff sagent(major kipolisi),mbwembwe zake ni hizo hizo,maana nilivyokutana naye alimake sure najua kua kabeba bastora,RIP kamanda Mkama SharpMuelezee tu unavyomjua Wewe Kiongozi. Kila nikiikumbuka tu ile Mikogo yake hasa ya Kiutembeaji pamoja na ile Miwani yake, Ubabe wake huku akiwa na Mwili wake ule Mdogo nabaki Kucheka tu lakini nikijiuliza alikuwa na Kipaji gani au Uwezo gani kiasi kwamba kuna wakati alikuwa anamudu Kulikamata Kundi Kubwa tu la Masela na akaongozana nalo peke yake hadi Kituoni lakini hamna hata Mtu Mmoja anayekimbia.
Alikuwa na mambo mengi na Vituko vingi tu ila binafsi nakumbuka kila alipokuwa akienda katika Vijiwe vya Masela wa enzi hizo wenyewe Masela walikuwa wanapiga Magoti na wanajisalimisha Kwake na ama Bangi walizokuwa nazo na Vitu vya Uwizi walivyoiba na walikuwa wakiongoza wenyewe Kituoni Polisi.
Marehemu Nkama Sharp ndiyo alikuwa Polisi pekee Jijini Dar es Salaam ambaye alikuwa hata akikukamata humbishii, unamtii na kweli hata Wewe mwenyewe unaamini kuwa ulikosea. Na alikuwa ni Polisi ambaye hana Uonevu na kuna muda alikuwa akiona unataabika au huna Msaada Kituoni basi anaweza Yeye kwa Huruma yake akakusaidia tena bila hata ya Kumpa Rushwa na ukatoka na hata ukitoka ulikuwa hurudii tena Makosa au Uhalifu.
Alikuwa na Uwezo wa Kipekee na Kipaji cha namna yake ambacho leo hii ni Nadra sana kukiona kwa Mapolisi wengi wa miaka hii ya sasa. Na nina uhakika kwa jinsi alivyokuwa Mweledi na ana Msimamo kama angekuwepo hadi miaka hii ya sasa kuna baadhi ya Maandamano ya Kisiasa wala asingekuwa anaiingilia au kuwasumbua Watu tofauti na Polisi wa sasa ambao kila Kukicha wao wanasema kuwa huwa wanatekeleza Maagizo kutoka Juu ( siyo Mbinguni kwa Mungu Baba )
Nashauri kama ikiwezekana Jeshi la Polisi nchini Tanzania litafute namna ya Kumuenzi huyu Marehemu Nkama Sharp ambaye Binafsi pia nakumbuka aliwahi kutufanya Mimi na baadhi ya Wenzangu tugawane Mitaa ile ya Jirani na Shule ya Muhimbili kwa Kumkimbia baada ya Kuambiwa kuwa tulikuwa tunafanya Fujo katika Mechi moja tuliyocheza na Wababe wa miaka hiyo Shule ya Tambaza na nakumbuka katika hali ya Kumkimbia niliweza Kupoteza Kiatu changu cha Mguu wa Kushoto na nilipofika Nyumbani nilipewa Kipigo cha maana ila nikashukuru kuwa ni bora nimepigwa na Wazazi kuliko ningeishia Mikononi mwa Marehemu Nkama Sharp.
Nasisitiza tena Marehemu Nkama Sharp aenziwe tafadhali na Mapolisi wa sasa hebu muigeni huyu Afande ili nanyi tuwapende.
Alikuwa anajimix na masela, kilaji sanaMuelezee tu unavyomjua Wewe Kiongozi. Kila nikiikumbuka tu ile Mikogo yake hasa ya Kiutembeaji pamoja na ile Miwani yake, Ubabe wake huku akiwa na Mwili wake ule Mdogo nabaki Kucheka tu lakini nikijiuliza alikuwa na Kipaji gani au Uwezo gani kiasi kwamba kuna wakati alikuwa anamudu Kulikamata Kundi Kubwa tu la Masela na akaongozana nalo peke yake hadi Kituoni lakini hamna hata Mtu Mmoja anayekimbia.
Alikuwa muelewa sanaNilifanya nae kazi Oysterbay Police kabla ya umauti,huku mwishoni baada ya kutoka FFU na kuhamia CID hakuwa na makeke mengi,Apumzike kwa Amani
Wale wazee wa Ajax pressure wanamtambua zaidi[emoji23][emoji23][emoji23]Na hakuishia tu kuwa na Mikwara kama ambavyo unamdhihaki hapa Kiongozi ila Jamaa ( Mrehemu Nkama Sharp ) pia alikuwa ni Mwana Karateka mzuri na mahiri sana tu. Vijana wengi wa miaka hii ya sasa mnajifanya mna Usela ila labda niwaambieni tu kuwa miaka yetu hiyo ambayo tulikuwa na akina Nkama Sharp ndiyo kulikuwa na Wahuni na Masela Wabobezi kabisa ila wote hao walikuwa wakikalishwa na Marehemu Nkama Sharp na wanatulia tuli. Ninaposema huyu Askari alikuwa si Mtu wa kawaida ndiyo namaanisha hivi.
Wewe kama tu Wavuta Bangi wa zamani Vijiweni wakipewa tu Signal kuwa Marehemu Nkama Sharp ameamka Kitini Kwake Ofisini na anaenda Kuvitembelea hivyo Vijiwe Kukamata Watu ndani ya Sekunde 7 au dakika 1 tu ulikuwa huoni Mtu Kijiweni bali unaona tu Vumbi huku kila Msela akilitafuta Boda la kwenda Kwao.
Nakumbuka kuna Siku moja Marehemu akiwa Full Mkoko kapigilia Kiaskari kabisa alitoka Baru / Mita ( alikimbizana ) na Mhalifu kutoka Kariakoo hadi maeneo ya Msasani jirani na ulipokuwa Uwanja wa Mpira wa Magunia na Yule Mhalifu kwa Kuchoka ilibidi asalimu Amri kwani alikuwa kila akikata Kona anamuona Mwanamume Nkama Sharp yuko Matakoni mwake.
Jamaa ( Mhalifu ) alipochoka na Kukaa chini Marehemu alikuja na kumuinua na Kumwambia waendelee na Marathon yao ambayo haikuwa rasmi na kilichotokea Yule Mhalifu sijajua kama alikuwa amechoka kweli au alikuwa anatafuta tu Huruma ambapo alijinyea / alikunya pale pale ndipo Afande Nkama Sharp nae akaamua Kuachana nae ili asije Kunuka Mimavi bure.
kuna usemi "Simba ni mkali lakini watoto wake wananyonya" kwa mikwara hiyo ameshindwa kukalea kabinti kake katika maadili mazuri yule anajiita Tunda.Kwa kweli miaka ya 80s mpaka 90 kulikuwa Askari Polisi waliokuwa na mbinu za kusambaratisha vigenge vya wahalifu yaani kwa kupita tu kwenye mitaa, wale masela wa miaka hiyo waliokuwa wakivuta jani vijiweni walikuwa wakikimbia wenyewe.Nakumbuka pale Arusha kulikuwa na Polisi mmoja alikuwa anafahamika kwa jina la Kimaro maarufu sana kwa jina la "SABA SITA" huyu jamaa hakuwa tofauti na marehemu Mkama Sharp. Pale Arusha miaka hiyo hakuna mtu ambaye alikuwa hamjui "SABA SITA". Kiukweli huyu askari alikuwa very smart katika kazi yake kwanza alikuwa anaipenda. Nakumbuka pale Sheikh Amri Abeid Stadium kulikuwa na mechi ya ligi kuu kati ya Simba SC na Ndovu FC ya Arusha, kwa baadhi ya wapenzi wa soka walikuwa wakiruka ukuta kuingia uwanjani kwa kukosa kiingilio,sehemu nilipokuwa nimekaa wakaja kukaa jamaa watatu walioruka ukuta kumbe Saba Sita alikuwa amewaona akapotezea kama hajawaona, wale washkaji wakajisahau. Kumbe "7 6" alikuwa anawalia timing, Simba ilipata goli la kuongoza lililofungwa na marehemu Edward Chumila uwanja mzima ulizizima kwa kushangilia lile goli, muda huo sasa Saba Sita akiwa amevalia pama lake la FFU, pingu, kirungu na kiunoni akiwa na pistol iliyokuwa kwenye kasha lake alikuja mpaka pale nilipokuwa nimekaa akawachomoa wale jamaa watatu walioruka ukuta sio siri jamaa waliingia hofu kubwa, akaanza kuzunguka nao uwanja mzima akiwa amewafunga mashati yao kwa kuwaunganisha alipofika nao kwenye Defender la Polisi aliwaamuru wapande ndani na walale kifudi fudi, hiyo ndio ilikuwa adhabu yao hawakuwapiga hata kidogo mpira ulipokwisha aliwaachia. Baadae nasikia Saba Sita alihamishiwa Mererani kikazi na kisha alihamishiwa tena CCP kuwa Mkufunzi. Nowadays sijui alipo nadhani atakuwa amestaafu.Lakini niconclude kwa kusema Mkama Sharp na Saba Sita ni Polisi waliokuwa very professional katika kazi yao.
Kwa kweli miaka ya 80s mpaka 90 kulikuwa Askari Polisi waliokuwa na mbinu za kusambaratisha vigenge vya wahalifu yaani kwa kupita tu kwenye mitaa, wale masela wa miaka hiyo waliokuwa wakivuta jani vijiweni walikuwa wakikimbia wenyewe.Nakumbuka pale Arusha kulikuwa na Polisi mmoja alikuwa anafahamika kwa jina la Kimaro maarufu sana kwa jina la "SABA SITA" huyu jamaa hakuwa tofauti na marehemu Mkama Sharp. Pale Arusha miaka hiyo hakuna mtu ambaye alikuwa hamjui "SABA SITA". Kiukweli huyu askari alikuwa very smart katika kazi yake kwanza alikuwa anaipenda. Nakumbuka pale Sheikh Amri Abeid Stadium kulikuwa na mechi ya ligi kuu kati ya Simba SC na Ndovu FC ya Arusha, kwa baadhi ya wapenzi wa soka walikuwa wakiruka ukuta kuingia uwanjani kwa kukosa kiingilio,sehemu nilipokuwa nimekaa wakaja kukaa jamaa watatu walioruka ukuta kumbe Saba Sita alikuwa amewaona akapotezea kama hajawaona, wale washkaji wakajisahau. Kumbe "7 6" alikuwa anawalia timing, Simba ilipata goli la kuongoza lililofungwa na marehemu Edward Chumila uwanja mzima ulizizima kwa kushangilia lile goli, muda huo sasa Saba Sita akiwa amevalia pama lake la FFU, pingu, kirungu na kiunoni akiwa na pistol iliyokuwa kwenye kasha lake alikuja mpaka pale nilipokuwa nimekaa akawachomoa wale jamaa watatu walioruka ukuta sio siri jamaa waliingia hofu kubwa, akaanza kuzunguka nao uwanja mzima akiwa amewafunga mashati yao kwa kuwaunganisha alipofika nao kwenye Defender la Polisi aliwaamuru wapande ndani na walale kifudi fudi, hiyo ndio ilikuwa adhabu yao hawakuwapiga hata kidogo mpira ulipokwisha aliwaachia. Baadae nasikia Saba Sita alihamishiwa Mererani kikazi na kisha alihamishiwa tena CCP kuwa Mkufunzi. Nowadays sijui alipo nadhani atakuwa amestaafu.Lakini niconclude kwa kusema Mkama Sharp na Saba Sita ni Polisi waliokuwa very professional katika kazi yao.
Jamaa yupo kiteto,hajastaafu Bado.ni ocd nadhani.Kwa kweli miaka ya 80s mpaka 90 kulikuwa Askari Polisi waliokuwa na mbinu za kusambaratisha vigenge vya wahalifu yaani kwa kupita tu kwenye mitaa, wale masela wa miaka hiyo waliokuwa wakivuta jani vijiweni walikuwa wakikimbia wenyewe.Nakumbuka pale Arusha kulikuwa na Polisi mmoja alikuwa anafahamika kwa jina la Kimaro maarufu sana kwa jina la "SABA SITA" huyu jamaa hakuwa tofauti na marehemu Mkama Sharp. Pale Arusha miaka hiyo hakuna mtu ambaye alikuwa hamjui "SABA SITA". Kiukweli huyu askari alikuwa very smart katika kazi yake kwanza alikuwa anaipenda. Nakumbuka pale Sheikh Amri Abeid Stadium kulikuwa na mechi ya ligi kuu kati ya Simba SC na Ndovu FC ya Arusha, kwa baadhi ya wapenzi wa soka walikuwa wakiruka ukuta kuingia uwanjani kwa kukosa kiingilio,sehemu nilipokuwa nimekaa wakaja kukaa jamaa watatu walioruka ukuta kumbe Saba Sita alikuwa amewaona akapotezea kama hajawaona, wale washkaji wakajisahau. Kumbe "7 6" alikuwa anawalia timing, Simba ilipata goli la kuongoza lililofungwa na marehemu Edward Chumila uwanja mzima ulizizima kwa kushangilia lile goli, muda huo sasa Saba Sita akiwa amevalia pama lake la FFU, pingu, kirungu na kiunoni akiwa na pistol iliyokuwa kwenye kasha lake alikuja mpaka pale nilipokuwa nimekaa akawachomoa wale jamaa watatu walioruka ukuta sio siri jamaa waliingia hofu kubwa, akaanza kuzunguka nao uwanja mzima akiwa amewafunga mashati yao kwa kuwaunganisha alipofika nao kwenye Defender la Polisi aliwaamuru wapande ndani na walale kifudi fudi, hiyo ndio ilikuwa adhabu yao hawakuwapiga hata kidogo mpira ulipokwisha aliwaachia. Baadae nasikia Saba Sita alihamishiwa Mererani kikazi na kisha alihamishiwa tena CCP kuwa Mkufunzi. Nowadays sijui alipo nadhani atakuwa amestaafu.Lakini niconclude kwa kusema Mkama Sharp na Saba Sita ni Polisi waliokuwa very professional katika kazi yao.
tuliroga nae uchawini.Mliroga nae wapi labda?