komanyahenry
JF-Expert Member
- Sep 15, 2017
- 903
- 1,361
Saba Sita
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alikuwa na mambo mengi na Vituko vingi tu ila binafsi nakumbuka kila alipokuwa akienda katika Vijiwe vya Masela wa enzi hizo wenyewe Masela walikuwa wanapiga Magoti na wanajisalimisha Kwake na ama Bangi walizokuwa nazo na Vitu vya Uwizi walivyoiba na walikuwa wakiongoza wenyewe Kituoni Polisi.
Marehemu Nkama Sharp ndiyo alikuwa Polisi pekee Jijini Dar es Salaam ambaye alikuwa hata akikukamata humbishii, unamtii na kweli hata Wewe mwenyewe unaamini kuwa ulikosea. Na alikuwa ni Polisi ambaye hana Uonevu na kuna muda alikuwa akiona unataabika au huna Msaada Kituoni basi anaweza Yeye kwa Huruma yake akakusaidia tena bila hata ya Kumpa Rushwa na ukatoka na hata ukitoka ulikuwa hurudii tena Makosa au Uhalifu.
Alikuwa na Uwezo wa Kipekee na Kipaji cha namna yake ambacho leo hii ni Nadra sana kukiona kwa Mapolisi wengi wa miaka hii ya sasa. Na nina uhakika kwa jinsi alivyokuwa Mweledi na ana Msimamo kama angekuwepo hadi miaka hii ya sasa kuna baadhi ya Maandamano ya Kisiasa wala asingekuwa anaiingilia au kuwasumbua Watu tofauti na Polisi wa sasa ambao kila Kukicha wao wanasema kuwa huwa wanatekeleza Maagizo kutoka Juu ( siyo Mbinguni kwa Mungu Baba )
Nashauri kama ikiwezekana Jeshi la Polisi nchini Tanzania litafute namna ya Kumuenzi huyu Marehemu Nkama Sharp ambaye Binafsi pia nakumbuka aliwahi kutufanya Mimi na baadhi ya Wenzangu tugawane Mitaa ile ya Jirani na Shule ya Muhimbili kwa Kumkimbia baada ya Kuambiwa kuwa tulikuwa tunafanya Fujo katika Mechi moja tuliyocheza na Wababe wa miaka hiyo Shule ya Tambaza na nakumbuka katika hali ya Kumkimbia niliweza Kupoteza Kiatu changu cha Mguu wa Kushoto na nilipofika Nyumbani nilipewa Kipigo cha maana ila nikashukuru kuwa ni bora nimepigwa na Wazazi kuliko ningeishia Mikononi mwa Marehemu Nkama Sharp.
Nasisitiza tena Marehemu Nkama Sharp aenziwe tafadhali na Mapolisi wa sasa hebu muigeni huyu Afande ili nanyi tuwapende.
mwananyamala sioHiyo miaka 90 hakuna kilicho dumu baada ya hapo..
huyu nasikia aliwakimbiza sana waarifu mjini moro,sijui yuwapi sasa
tuache utani kwa mwili huo mtu kama mwarabu fighter au Arafat ngumi jiwe huyu anauwezo wa kuwatuliza kweli kipindi hicho kulikuwa hakuna mbavu.Mkama SharpView attachment 1186331
Usahihi ni Mkama SharpKwa nini wewe kila unapomtaja jina unaandika Nkama Sharp ila wengine wanaandika Mkama Sharp? Usahihi ni upi?
Alikuwa na mambo mengi na Vituko vingi tu ila binafsi nakumbuka kila alipokuwa akienda katika Vijiwe vya Masela wa enzi hizo wenyewe Masela walikuwa wanapiga Magoti na wanajisalimisha Kwake na ama Bangi walizokuwa nazo na Vitu vya Uwizi walivyoiba na walikuwa wakiongoza wenyewe Kituoni Polisi.
Marehemu Nkama Sharp ndiyo alikuwa Polisi pekee Jijini Dar es Salaam ambaye alikuwa hata akikukamata humbishii, unamtii na kweli hata Wewe mwenyewe unaamini kuwa ulikosea. Na alikuwa ni Polisi ambaye hana Uonevu na kuna muda alikuwa akiona unataabika au huna Msaada Kituoni basi anaweza Yeye kwa Huruma yake akakusaidia tena bila hata ya Kumpa Rushwa na ukatoka na hata ukitoka ulikuwa hurudii tena Makosa au Uhalifu.
Alikuwa na Uwezo wa Kipekee na Kipaji cha namna yake ambacho leo hii ni Nadra sana kukiona kwa Mapolisi wengi wa miaka hii ya sasa. Na nina uhakika kwa jinsi alivyokuwa Mweledi na ana Msimamo kama angekuwepo hadi miaka hii ya sasa kuna baadhi ya Maandamano ya Kisiasa wala asingekuwa anaiingilia au kuwasumbua Watu tofauti na Polisi wa sasa ambao kila Kukicha wao wanasema kuwa huwa wanatekeleza Maagizo kutoka Juu ( siyo Mbinguni kwa Mungu Baba )
Nashauri kama ikiwezekana Jeshi la Polisi nchini Tanzania litafute namna ya Kumuenzi huyu Marehemu Nkama Sharp ambaye Binafsi pia nakumbuka aliwahi kutufanya Mimi na baadhi ya Wenzangu tugawane Mitaa ile ya Jirani na Shule ya Muhimbili kwa Kumkimbia baada ya Kuambiwa kuwa tulikuwa tunafanya Fujo katika Mechi moja tuliyocheza na Wababe wa miaka hiyo Shule ya Tambaza na nakumbuka katika hali ya Kumkimbia niliweza Kupoteza Kiatu changu cha Mguu wa Kushoto na nilipofika Nyumbani nilipewa Kipigo cha maana ila nikashukuru kuwa ni bora nimepigwa na Wazazi kuliko ningeishia Mikononi mwa Marehemu Nkama Sharp.
Nasisitiza tena Marehemu Nkama Sharp aenziwe tafadhali na Mapolisi wa sasa hebu muigeni huyu Afande ili nanyi tuwapende.
Huyu mangi ni proffesional killerKwa kweli miaka ya 80s mpaka 90 kulikuwa Askari Polisi waliokuwa na mbinu za kusambaratisha vigenge vya wahalifu yaani kwa kupita tu kwenye mitaa, wale masela wa miaka hiyo waliokuwa wakivuta jani vijiweni walikuwa wakikimbia wenyewe.Nakumbuka pale Arusha kulikuwa na Polisi mmoja alikuwa anafahamika kwa jina la Kimaro maarufu sana kwa jina la "SABA SITA" huyu jamaa hakuwa tofauti na marehemu Mkama Sharp. Pale Arusha miaka hiyo hakuna mtu ambaye alikuwa hamjui "SABA SITA". Kiukweli huyu askari alikuwa very smart katika kazi yake kwanza alikuwa anaipenda. Nakumbuka pale Sheikh Amri Abeid Stadium kulikuwa na mechi ya ligi kuu kati ya Simba SC na Ndovu FC ya Arusha, kwa baadhi ya wapenzi wa soka walikuwa wakiruka ukuta kuingia uwanjani kwa kukosa kiingilio,sehemu nilipokuwa nimekaa wakaja kukaa jamaa watatu walioruka ukuta kumbe Saba Sita alikuwa amewaona akapotezea kama hajawaona, wale washkaji wakajisahau. Kumbe "7 6" alikuwa anawalia timing, Simba ilipata goli la kuongoza lililofungwa na marehemu Edward Chumila uwanja mzima ulizizima kwa kushangilia lile goli, muda huo sasa Saba Sita akiwa amevalia pama lake la FFU, pingu, kirungu na kiunoni akiwa na pistol iliyokuwa kwenye kasha lake alikuja mpaka pale nilipokuwa nimekaa akawachomoa wale jamaa watatu walioruka ukuta sio siri jamaa waliingia hofu kubwa, akaanza kuzunguka nao uwanja mzima akiwa amewafunga mashati yao kwa kuwaunganisha alipofika nao kwenye Defender la Polisi aliwaamuru wapande ndani na walale kifudi fudi, hiyo ndio ilikuwa adhabu yao hawakuwapiga hata kidogo mpira ulipokwisha aliwaachia. Baadae nasikia Saba Sita alihamishiwa Mererani kikazi na kisha alihamishiwa tena CCP kuwa Mkufunzi. Nowadays sijui alipo nadhani atakuwa amestaafu.Lakini niconclude kwa kusema Mkama Sharp na Saba Sita ni Polisi waliokuwa very professional katika kazi yao.
DuhSABASITA ndie Baba Mzazi wa haka kabinti kanakoitwa TUNDA,yupo Dar nadhani bado hajastaafu
Huwez pewa vyote...Siku hizi kajichokea tu ni ocd huku manyara kituo nimesahau jina,ujanja wote kashindwa kumdhibiti mwanae kawa mdangaji sugu utafikiria sio mtoto wa sabasita
Aiseee nilikuwa nadhani ni mimi tu ndo namkumbuka yule Pot kwa members wote wa Jf, kumbe tupo wengi tunaomkumbuka!
Kiukweli, kwa mtu ambaye hakuwahi kumuona au kuingia kwenye 18 za huyu njagu anaweza akadhani jamaa tunampamba bure au tunazungumzia story ya abunuasi.
Nilikuwa namuona sana pale Uwanja wa Taifa wa zamani (shamba la bibi). Na mimi kama mrukaji ukuta maarufu enzi hizo nilishanusurika mara kadhaa kuingia mikononi mwake. Nakumbuka sometimes jamaa alikuwa na mbwa, na mbwa huyu alikuwa anafata maelekezo ya afande Sharp kwa namna ya kushangaza sana.
Hivi wewe unawajua polisi vizuri eti Mwarabu fighter asitulizwe.tuache utani kwa mwili huo mtu kama mwarabu fighter au Arafat ngumi jiwe huyu anauwezo wa kuwatuliza kweli kipindi hicho kulikuwa hakuna mbavu.
Huyu 7 6 ana mtoto wake wa kike anajiita tunda [emoji23][emoji23][emoji23]Kwa kweli miaka ya 80s mpaka 90 kulikuwa Askari Polisi waliokuwa na mbinu za kusambaratisha vigenge vya wahalifu yaani kwa kupita tu kwenye mitaa, wale masela wa miaka hiyo waliokuwa wakivuta jani vijiweni walikuwa wakikimbia wenyewe.Nakumbuka pale Arusha kulikuwa na Polisi mmoja alikuwa anafahamika kwa jina la Kimaro maarufu sana kwa jina la "SABA SITA" huyu jamaa hakuwa tofauti na marehemu Mkama Sharp. Pale Arusha miaka hiyo hakuna mtu ambaye alikuwa hamjui "SABA SITA". Kiukweli huyu askari alikuwa very smart katika kazi yake kwanza alikuwa anaipenda. Nakumbuka pale Sheikh Amri Abeid Stadium kulikuwa na mechi ya ligi kuu kati ya Simba SC na Ndovu FC ya Arusha, kwa baadhi ya wapenzi wa soka walikuwa wakiruka ukuta kuingia uwanjani kwa kukosa kiingilio,sehemu nilipokuwa nimekaa wakaja kukaa jamaa watatu walioruka ukuta kumbe Saba Sita alikuwa amewaona akapotezea kama hajawaona, wale washkaji wakajisahau. Kumbe "7 6" alikuwa anawalia timing, Simba ilipata goli la kuongoza lililofungwa na marehemu Edward Chumila uwanja mzima ulizizima kwa kushangilia lile goli, muda huo sasa Saba Sita akiwa amevalia pama lake la FFU, pingu, kirungu na kiunoni akiwa na pistol iliyokuwa kwenye kasha lake alikuja mpaka pale nilipokuwa nimekaa akawachomoa wale jamaa watatu walioruka ukuta sio siri jamaa waliingia hofu kubwa, akaanza kuzunguka nao uwanja mzima akiwa amewafunga mashati yao kwa kuwaunganisha alipofika nao kwenye Defender la Polisi aliwaamuru wapande ndani na walale kifudi fudi, hiyo ndio ilikuwa adhabu yao hawakuwapiga hata kidogo mpira ulipokwisha aliwaachia. Baadae nasikia Saba Sita alihamishiwa Mererani kikazi na kisha alihamishiwa tena CCP kuwa Mkufunzi. Nowadays sijui alipo nadhani atakuwa amestaafu.Lakini niconclude kwa kusema Mkama Sharp na Saba Sita ni Polisi waliokuwa very professional katika kazi yao.
Saba sita alikua anawafunga mashati watuhumiwa 6 wanatangulia kituoni yeye anawafuata kwa nyuma na mayenu yake kama papaa chemendee.SABASITA ndie Baba Mzazi wa haka kabinti kanakoitwa TUNDA,yupo Dar nadhani bado hajastaafu
wamekupa rangi zake zote mkuu.nyeupe na nyeusi yake.Hata mimi namkumbuka. Ila kwangu naona ni kama chongo kwenye kundi la vipofu. Nadhani ushamba wetu hasa enzi zile za zamani ndizo zilimkuza zaidi. Naomba nieleweke kuwa sisemi kuwa alikuwa ''mzuri'' wa kazi yake lakini nasema tu ''uzuri'' wake ulipaishwa na ushamba na woga wetu.
Aiseee nilikuwa nadhani ni mimi tu ndo namkumbuka yule Pot kwa members wote wa Jf, kumbe tupo wengi tunaomkumbuka!
Kiukweli, kwa mtu ambaye hakuwahi kumuona au kuingia kwenye 18 za huyu njagu anaweza akadhani jamaa tunampamba bure au tunazungumzia story ya abunuasi.
Nilikuwa namuona sana pale Uwanja wa Taifa wa zamani (shamba la bibi). Na mimi kama mrukaji ukuta maarufu enzi hizo nilishanusurika mara kadhaa kuingia mikononi mwake. Nakumbuka sometimes jamaa alikuwa na mbwa, na mbwa huyu alikuwa anafata maelekezo ya afande Sharp kwa namna ya kushangaza sana.
mbwa alijua atapigwa risasi.Sharp na mbwa wake (mbwa wa polisi).
Si mara 1 au mara 2 niliwahi kumwona Sharp akiwa na mbwa. Kuna wakati angemwacha mbwa karibu na geti la kuingia kwenye Uwanja wa Taifa wa zamani (shamba la bibi) bila kumfunga popote.Angemwamrisha "tulia hapa hadi nikukute, usiondoke!" na mbwa angatulia hapo. Hata akikuona unajipenyeza getini kiwizi wizi au unajaribu kuruka ukuta mbwa huyo asingekuwa na time na wewe.
Ila ole wako aamrishwe kukukamata ndo utaisoma namba.Afande Sharp angemwelekeza mbwa wake " unamwona yule jamaa aliyevaa kofia ya blue, t-shirt nyeupe na jeans ya blue?nenda kamkamate!" Ni hivi mbwa angekusonga wewe tu aliyeelekezwa akukamate (hata kama uko kwenye kundi la watu wengi, na angekukamata).
Iliwahi kutokea afande Sharp alimsakizia mbwa msela mmoja aliyekuwa anajaribu kupita chini ya geti, jamaa alivyoona atadakwa ikabidi akimbilie kwenye kambi ya jeshi ya Abdallah Twalipo (almaarufu 'Ngome') iliyo jirani kabisa na Uwanja wa Taifa na kituo cha mafuta. Jamaa alivyoingia kambini, wazee wa JWTZ waliokuwa zamu walimlinda na kumwambia asiwe na hofu, walichofanya ni kumsubiri mbwa aingie kambini kisha wamfanyie mambo ya Samson na Simba wa Wafilisti. Ila yule mbwa alikuwa na akili bhana, alifunga breki getini na kurudi kwa boss. Wajeda wakamwambia Sharp "huyo mbwa wako na wewe mwenyewe leo tulitaka tuwafundishe adabu.Rudia tena uone". Sharp hakujibu neno.
Ila huyu Pot alikuwa tishio kwa wahuni kwakweli.Kuna mtoto yupi wa mjini ambaye hakumfahamu?