Chumchang Changchum
JF-Expert Member
- Nov 1, 2013
- 5,988
- 6,226
Mkuu jiwe limekupata..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
"SABA SITA" kwa sasa yuko wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara kama (OCD).Huyu jamaa miaka ya nyuma alinyoosha vibaka na majambazi waliokuwa wanasumbua Arusha, alikuwa yeye na Kachero mmoja aliyekuwa anaitwa Robert Bro mmoja alikuwa anapenda sana kupiga cheni kubwa kubwa na kupush ndinga za hatari, kiasi kwamba unaweza kujua ni msela flani kumbe Kachero. Huyo Robert naye sijui siku hizi yuko wapi.Moro kulikuwa na afande saba sita sijui yupo wapi
Huyu Nkama Sharp kafa muda tu alizaliwa na pacha mwenzie huwezi kuwatofautisha ukiwaona
kabla hajaamia manzese kwenye nyumba yake aliishi
mtaa wa kibambawe namba 16 sisi tulikuwa na nyumba namba 14
night star waliimba kimbia mbio mbio mkama sharp anakuja
kafa kwenye 2008 zaidi ya miaka 10
Tena alikumbana na kashfa ya wizi akaswekwagwa ndani nakumbukaHuyu Nkama Sharp kafa muda tu alizaliwa na pacha mwenzie huwezi kuwatofautisha ukiwaona
kabla hajaamia manzese kwenye nyumba yake aliishi
mtaa wa kibambawe namba 16 sisi tulikuwa na nyumba namba 14
night star waliimba kimbia mbio mbio mkama sharp anakuja
kafa kwenye 2008 zaidi ya miaka 10
Nakumbuka enzi tunacheza disco Mbowe na YMCA kulikuwa na magangwe wa mjiniNa hakuishia tu kuwa na Mikwara kama ambavyo unamdhihaki hapa Kiongozi ila Jamaa ( Mrehemu Nkama Sharp ) pia alikuwa ni Mwana Karateka mzuri na mahiri sana tu. Vijana wengi wa miaka hii ya sasa mnajifanya mna Usela ila labda niwaambieni tu kuwa miaka yetu hiyo ambayo tulikuwa na akina Nkama Sharp ndiyo kulikuwa na Wahuni na Masela Wabobezi kabisa ila wote hao walikuwa wakikalishwa na Marehemu Nkama Sharp na wanatulia tuli. Ninaposema huyu Askari alikuwa si Mtu wa kawaida ndiyo namaanisha hivi.
Wewe kama tu Wavuta Bangi wa zamani Vijiweni wakipewa tu Signal kuwa Marehemu Nkama Sharp ameamka Kitini Kwake Ofisini na anaenda Kuvitembelea hivyo Vijiwe Kukamata Watu ndani ya Sekunde 7 au dakika 1 tu ulikuwa huoni Mtu Kijiweni bali unaona tu Vumbi huku kila Msela akilitafuta Boda la kwenda Kwao.
Nakumbuka kuna Siku moja Marehemu akiwa Full Mkoko kapigilia Kiaskari kabisa alitoka Baru / Mita ( alikimbizana ) na Mhalifu kutoka Kariakoo hadi maeneo ya Msasani jirani na ulipokuwa Uwanja wa Mpira wa Magunia na Yule Mhalifu kwa Kuchoka ilibidi asalimu Amri kwani alikuwa kila akikata Kona anamuona Mwanamume Nkama Sharp yuko Matakoni mwake.
Jamaa ( Mhalifu ) alipochoka na Kukaa chini Marehemu alikuja na kumuinua na Kumwambia waendelee na Marathon yao ambayo haikuwa rasmi na kilichotokea Yule Mhalifu sijajua kama alikuwa amechoka kweli au alikuwa anatafuta tu Huruma ambapo alijinyea / alikunya pale pale ndipo Afande Nkama Sharp nae akaamua Kuachana nae ili asije Kunuka Mimavi bure.
Mimi huyu Sajent Sharp nilikua nakutana nae mipirani miaka hiyo, hasa inapocheza Timu za Simba na Yanga. Pia pale Karume Stadium kulikua na Derby ingine ya BOOM v/s ASHANT ndo alikuwepo huyu Mwamba.Uko sahihi Mkuu na ukiwa Mtoto wa Mjini kweli hasa wa Dar es Salaam ni lazima tu utamjua Marehemu Nkama Sharp. Nahisi Jeshi la Polisi nchini Tanzania halijamuenzi vile ipasavyo hivyo siwalazimishi na sina huo Uwezo ila Siku Moja nitakuwa ni mwenye Furaha Kubwa pale nikisikia ameenziwa kwa namna yoyote ile au basi hata Mkewe ( kama yupo hai nae ) au Watoto wake wamekumbukwa kwa Heshima Kubwa ya Marehemu Baba yao hapa nchini hasa hasa kwa Mkoa wetu huu wa Dar es Salaam.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Na hakuishia tu kuwa na Mikwara kama ambavyo unamdhihaki hapa Kiongozi ila Jamaa ( Mrehemu Nkama Sharp ) pia alikuwa ni Mwana Karateka mzuri na mahiri sana tu. Vijana wengi wa miaka hii ya sasa mnajifanya mna Usela ila labda niwaambieni tu kuwa miaka yetu hiyo ambayo tulikuwa na akina Nkama Sharp ndiyo kulikuwa na Wahuni na Masela Wabobezi kabisa ila wote hao walikuwa wakikalishwa na Marehemu Nkama Sharp na wanatulia tuli. Ninaposema huyu Askari alikuwa si Mtu wa kawaida ndiyo namaanisha hivi.
Wewe kama tu Wavuta Bangi wa zamani Vijiweni wakipewa tu Signal kuwa Marehemu Nkama Sharp ameamka Kitini Kwake Ofisini na anaenda Kuvitembelea hivyo Vijiwe Kukamata Watu ndani ya Sekunde 7 au dakika 1 tu ulikuwa huoni Mtu Kijiweni bali unaona tu Vumbi huku kila Msela akilitafuta Boda la kwenda Kwao.
Nakumbuka kuna Siku moja Marehemu akiwa Full Mkoko kapigilia Kiaskari kabisa alitoka Baru / Mita ( alikimbizana ) na Mhalifu kutoka Kariakoo hadi maeneo ya Msasani jirani na ulipokuwa Uwanja wa Mpira wa Magunia na Yule Mhalifu kwa Kuchoka ilibidi asalimu Amri kwani alikuwa kila akikata Kona anamuona Mwanamume Nkama Sharp yuko Matakoni mwake.
Jamaa ( Mhalifu ) alipochoka na Kukaa chini Marehemu alikuja na kumuinua na Kumwambia waendelee na Marathon yao ambayo haikuwa rasmi na kilichotokea Yule Mhalifu sijajua kama alikuwa amechoka kweli au alikuwa anatafuta tu Huruma ambapo alijinyea / alikunya pale pale ndipo Afande Nkama Sharp nae akaamua Kuachana nae ili asije Kunuka Mimavi bure.
Duu one in millionHuu uzi ni wa mda mrefu sana ila nami naomba niseme jambo kidogo,
Baada ya kusoma uzi huu wa uzalendo wa askari na kubakia na lawama kubwa kwa maaskari wa sasa, nikweli kabisa kwa sasa kukutana na askari mwadilifu ni ngumu mno, naomba nami kumshukuru afande mmoja japo nimejitahidi kumtafuta kwa sasa japo nipate jina lake na hata kumpa mkono wa shukrani na pia ajue hata mimi leo ni nani na ajue kuwa maisha ni duara katika dunia hii.
Ilikuwa mwaka 2011 wakati nimehitimu shahada yangu ya kwanza nikaenda Mwanza kutafuta maisha, maisha nayo yakawa magumu kweli hadi nikaingia kwenye utapel wa kuuza viwanja vya watu kwa kutumia mihuri bandia na kugushi nyakaraka nyingi za serikali.
Siku moja nikanasa kwa mjanja mmoja ambae nilitaka nimpige zaidi ya milion 7 hivi ila akashtukia dakika za mwishoni kabisa wananzego wakanikamata na kukuchora vibao kadhaa na baadae kunipeleka kituo cha Police, baada ya kufikishwa police nimetoa maelezo bila kupindisha chochote pale nikaingizwa ndani na nililala na siku ya pili alikuja kuniita na kumbe kesi yangu alipewa yeye baada kunipeleka chumba cha mahojiano huku akinichukua maelezo, bila kusita nami niliongea ukweli mtupu bila kuficha jambo lolote.
Baada ya maelezo hayo kumalizika akaniambia kaka mbona elimu yako nzuri tu kwa nini unajiingiza huku kwenye kifo na huku unajuwa majuto yake? Nilimjibu tu kuwa kiukweli hapa mimi ni mjinga na shetani katumia nafasi hii kutaka kuniangamiza.
Baada ya kumpa majibu yale alikaa kimya mda mrefu sana, kaniuliza una ndugu wa kukuwekea dhamana nikamjibu sina ,je rafiki yeyote ambae mnafanya hizi Dili ?,nikamjibu hizi dili napiga mwenyewe sina rafiki, je nyumbani kwenu hakuna mtu wa kuja huku Mwanza?, nikamjibu naogopa kuwaambia nitaficha wapi sura yangu?
Baada ya maswali hayo kaanza kunifungulia vifungu vya sheria ambavyo nitatiwa hatia navyo na vile nitaitumikia adhabu yangu, machozi yalinitoka ghafla, akaniambia usilie najuwa umefanya jambo bila kujuwa madhara yake.
Baadae akampigia jamaa simu alienikamatisha jamaa akaja kituoni akamsomea vifungu vya sheria na kumuomba anisamehe na ujinga wangu umenifanya nifanye kitu bila kujuwa madhara yake, jamaa nae bila hiana alicheka kidogo akasema mie huyu kijana kwanza nimempenda kuongea ukweli wake ni kweli kajutia kosa lake hivyo namsamehe lakini kulingana na elimu yake aliyonayo basi naenda kumtafutia ajira na naahidi atakuwa mtu mwema na atakuwa rafiki yangu.
Ndipo yule afande alisimama akaniambia Mungu akutunze na naomba uchukue kila kitu chako uondoke hapa, ukweli machozi yalinitoka tena na kumshukuru tena na tena yule afande.
Ukweli ni kwamba bado wapo watu wenye utu japo ni wachache sana ila ukweli bado wapo.
Mungu akubariki afande mahali ulipo japo sikuoni natamani nikuone nikusaidie hata ada ya mwanao kwa upendo tu wa kawaida japo najuwa ungekutana nami leo na kunifahamu sijui kama ungeongea na mimi najua ungekuwa unaniogopa na kufikiri vingine Mungu wa mbinguni akutunze
Ahsante Mchungaji DR.Jacob Mutashi Mungu akutunze umalizie uzee mwema ulichokifanya kwangu ni zaidi ya kufanya jambo.
Kuna elimu baada elimu mkuu nilijifunza kituDuu one in million
Ulikutana na Binaadamu kweli na siyo Mtu, katika Maisha siku zote omba Mungu ukutane na Wanadamu na siyo Watu!!Kuna elimu baada elimu mkuu nilijifunza kitu
Ukweli mkuu hapo ndipo nilijua kuwa kuna binadamu na watuUlikutana na Binaadamu kweli na siyo Mtu, katika Maisha siku zote omba Mungu ukutane na Wanadamu na siyo Watu!!
Dah safi sana, maafande wa dizaini ya akina Mkama wapo wengi tu nimekutana nao, nimeishi nao, yaan mpaka unashangaa kweli maaskari wa namna hii bado wapo kweli? 😳 ILA WAPO KABISAAHuu uzi ni wa mda mrefu sana ila nami naomba niseme jambo kidogo,
Baada ya kusoma uzi huu wa uzalendo wa askari na kubakia na lawama kubwa kwa maaskari wa sasa, nikweli kabisa kwa sasa kukutana na askari mwadilifu ni ngumu mno, naomba nami kumshukuru afande mmoja japo nimejitahidi kumtafuta kwa sasa japo nipate jina lake na hata kumpa mkono wa shukrani na pia ajue hata mimi leo ni nani na ajue kuwa maisha ni duara katika dunia hii.
Ilikuwa mwaka 2011 wakati nimehitimu shahada yangu ya kwanza nikaenda Mwanza kutafuta maisha, maisha nayo yakawa magumu kweli hadi nikaingia kwenye utapel wa kuuza viwanja vya watu kwa kutumia mihuri bandia na kugushi nyakaraka nyingi za serikali.
Siku moja nikanasa kwa mjanja mmoja ambae nilitaka nimpige zaidi ya milion 7 hivi ila akashtukia dakika za mwishoni kabisa wananzego wakanikamata na kukuchora vibao kadhaa na baadae kunipeleka kituo cha Police, baada ya kufikishwa police nimetoa maelezo bila kupindisha chochote pale nikaingizwa ndani na nililala na siku ya pili alikuja kuniita na kumbe kesi yangu alipewa yeye baada kunipeleka chumba cha mahojiano huku akinichukua maelezo, bila kusita nami niliongea ukweli mtupu bila kuficha jambo lolote.
Baada ya maelezo hayo kumalizika akaniambia kaka mbona elimu yako nzuri tu kwa nini unajiingiza huku kwenye kifo na huku unajuwa majuto yake? Nilimjibu tu kuwa kiukweli hapa mimi ni mjinga na shetani katumia nafasi hii kutaka kuniangamiza.
Baada ya kumpa majibu yale alikaa kimya mda mrefu sana, kaniuliza una ndugu wa kukuwekea dhamana nikamjibu sina ,je rafiki yeyote ambae mnafanya hizi Dili ?,nikamjibu hizi dili napiga mwenyewe sina rafiki, je nyumbani kwenu hakuna mtu wa kuja huku Mwanza?, nikamjibu naogopa kuwaambia nitaficha wapi sura yangu?
Baada ya maswali hayo kaanza kunifungulia vifungu vya sheria ambavyo nitatiwa hatia navyo na vile nitaitumikia adhabu yangu, machozi yalinitoka ghafla, akaniambia usilie najuwa umefanya jambo bila kujuwa madhara yake.
Baadae akampigia jamaa simu alienikamatisha jamaa akaja kituoni akamsomea vifungu vya sheria na kumuomba anisamehe na ujinga wangu umenifanya nifanye kitu bila kujuwa madhara yake, jamaa nae bila hiana alicheka kidogo akasema mie huyu kijana kwanza nimempenda kuongea ukweli wake ni kweli kajutia kosa lake hivyo namsamehe lakini kulingana na elimu yake aliyonayo basi naenda kumtafutia ajira na naahidi atakuwa mtu mwema na atakuwa rafiki yangu.
Ndipo yule afande alisimama akaniambia Mungu akutunze na naomba uchukue kila kitu chako uondoke hapa, ukweli machozi yalinitoka tena na kumshukuru tena na tena yule afande.
Ukweli ni kwamba bado wapo watu wenye utu japo ni wachache sana ila ukweli bado wapo.
Mungu akubariki afande mahali ulipo japo sikuoni natamani nikuone nikusaidie hata ada ya mwanao kwa upendo tu wa kawaida japo najuwa ungekutana nami leo na kunifahamu sijui kama ungeongea na mimi najua ungekuwa unaniogopa na kufikiri vingine Mungu wa mbinguni akutunze
Ahsante Mchungaji DR.Jacob Mutashi Mungu akutunze umalizie uzee mwema ulichokifanya kwangu ni zaidi ya kufanya jambo.
Bado wapo japo ni wachache sana mkuuDah safi sana, maafande wa dizaini ya akina Mkama wapo wengi tu nimekutana nao, nimeishi nao, yaan mpaka unashangaa kweli maaskari wa namna hii bado wapo kweli? 😳 ILA WAPO KABISAA