Huyu Salah anastahili Ballon d'or.

Point yangu ni kwamba KUBEBA MAKOMBE hakujawahi kuwa kigezo cha messi na ronaldo kupewa ballon d'or sababu kila msimu huwa kuna timu zinachukua Treble ulaya yaani LIGI, FA cup na champions league ila hazijawahi kutoa player of the year kivipi leo ndio mtumie hiki kma kigezo cha kumnyima salah???

Salah anastahili kwa mchango wake kwa club haijalishi mchango umezaa kombe au lah ila tukisema kombe ndio iwe kigezo ronaldo na messi wangezisikia ballon d'or kwenye bomba
 
Kwahiyo unataka kuniambia Bingwa wa Hispania 2009-2010 alikua nani?
Ingekuwa criteria ni lazima uwe umeshinda kombe tu basi list ya wachezaji mpaka 23 ili wapigiwe kura ya nini? si wangetoa majina ya wachezaji tu walioshinda makombe list ndefu ya nini. mfano Salah kawa mchezaji bora EPL lakini hajachukuwa kombe wako wachezaji wa city wamechukuwa kombe lakini hakupata. sitaki kufananisha ila point yangu kuna tofauti ya team bora na mchezaji bora. kawaida mchezaji bora duniani hawatizami kuchukuwa vikombe maana hata kina Gerald walishawahi kuwa on short list japo hawakuwa na vikombe. Hoja je Salah baada ya mchango wake mwaka huu anastahili au hapana, kwangu mimi anastahili na sio kusaidia Liverpool tu pia team ya Egypt kwenda W.C baada ya miaka mingi. Tumpe stahili yake.
 
Sasa mm nauliza swali huu msimu CR7,Mess na Mohamed nani mkali katka kuzifumania nyavu? kwa maana ya kubadilisha matokeo mda wowote na club inajua bila yeye basi wamekwisha.Naomba jibu
 
ndio habari ya mujini duniani kote. Allah ampe wepes

Inshallah..mzima swahiba? Hayo mambo sijui ya kiatu yatafuata baadae na mavigezo yao ila kwa sie hatuhitaji kuambiwa na mtu kwamba nani anatisha kwa sasa. Hata mtoto wa miaka miwili anamuelewa jamaa kwamba anakamua ndimu na anazirushia nyavuni ipasavyo.
 
Mo Salah anastahili kuchukua mwaka huu ila tatizo watu wameshajiandaa kwa Christiano kuchukua tena
 
Hahah!! Mkuu unakosea kusema hivyo huwa wanaangalia timu yako umeisaidia vipi kupata mafanikio na mafanikio yenyewe ndio makombe, ingekua kama hivyo unavyosema wewe Mess angekua anachukua kila mwaka
2010 messi alichukua kombe gani?
 
Salah bado hata hajafikia uchezaji wa Morata avute mguu kwanza.
Morata huyu anaebadilishana na Giroud?
Morata anaezidiwa magoli na Okwi au yupi?
Morata ambae hata italy hajawahi kuwa bora au top score.. Au morata anaekosa magoli yupo na nyavu?
We nae uko upande wa wazungu... Yaani Salah anamtoa kwenye reli mtu kama Kane.. Aguero na De bruyne halafu wewe unataja mtu anaezidiwa na Dele Ali na Sane.

Acha bac jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…