Huyu Sallam kumbe ndio kila kitu kwa Diamond

Acha porojo mjomba ukisikia team work ndio hiyo, hawa watu wanakabidhiana majukumu, sababu sallam yupo vizuri sana kimataifa ni rahisi kwake ku deal na huko, but talle na fella pia wanafanya vyema majukumu yao, ona madee is doing good, yamoto, chege na temba even diamond himself anawakubari kiutendaji, hata nature ni fella aliyemsaidia, diamond angeona udhaifu wao asingeendelea kufanya nao kazi, hata huyo sallam amezungumza vyema sana kuhusu utendaji wao, acha kukashifu wenzako kijana!
 
Siri kuu ya mafanikio ya diamond ni hela, kama alivyosema sallam, yaani diamond haogopi kutumia pesa pale anapohitaji pesa, ndio maana analipa managers, body guard na dancers, lkn wasanii wengine utakuta yeye ndio dancer, manager, body guard, pia hata kubeba begi,tutumie pesa inapostahili
 
Mkuu hiyo point nimeikubali sana!!
Sio kwenye mziki pekee, hata kwenye business nyingine, unaingiza bidhaa sokoni, lazima kuweka nguvu ya ziada kuuza!!
 
teh teh kumbe ndio kazi za babu tale na fella hizo?
 
Huyu Sallam namwelewa sanaa ni mtu asiependa uswahili mtu asiependa umaarufu uchwara! Kiufupi jamaa yupo smart sana kuanzia kichwani hadi kuishi na watu! Jamaa siyo wa mchangani n wakimataifa zaidi!
 
Huyo ndio Jorge Mendez wa Bongo fleva.Tungekuwa na watu 10 kama Sallam bongo fleva ingetesa sana kimataifa
Ni kweli kabisa jamaa mkali na amenifurahisha pale alipotafuta upenyo wa MTV Nigeria kuacha figisufigisu za kibongo ambazo hazina maana.
 

Mkuu kila kitu kinaumuhimu wake..

Deals za ubalozi TZ huwa anasimamia Babu Tale, unajuwa zinaingiza pesa kiasi gani kwa Diamond?

Collable ya Neyo na Diamond Babutale ndio alifanya maongezi kilakitu mpaka kufikia maelewano licha ya Diamond kukubalika na Neyo kabla ya hapo..

Afu ukija kwa Fela huyu jamaa analijua game vizuri sana. Watu huwa wanazungumzia "FITNA" kijuujuu lakini ni kitu muhimu sana kwenye management ikiwemo timing ya utoaji nyimbo, nyimbo ipi, kutafuta wadau wa kufadhili promotions (kama Dr. Mwaka alivyotoa milioni 50 tangazo lake likae kwenye video ya utanipenda), shows za ndani bongo na hta nchi karibu, kuwa karibu na watu wa media n.k...

Kila mmoja anaumuhimu wake..!!!
 
Jamaa muwazi sana na ana busara pia maanake hiyo issue ya Kiba alivyoielezea...

Naimani wigo wa kazi zake utakua zaidi kila uchwao,sasa basi aachane na hiyo mikataba aliyoiita ya kiimani.
 
of course kila mtu ana umuhimu wake, ndio maana babu tale na fella wakamwambia jamaa waungane ili wapige kazi, kitu ambacho ni kizuri
 
Ni kweli inabidi atajwe ili aache tabia za kishamba,unambania mtu ili iweje ?
Ukimbania kijana unaumiza watu wengi sana nyuma yake, wazazi, kizazi chake kijacho, wadogo zake na hata taifa! Leo hii diamond kwenye chain yake wengi wametoka hata bwana wa antiezekiel anategemea kwa mond! Umaskini wetu unatokana na tabia zetu za ajabu ajabu
 
Kuna sehemu diamond anaimba anayepanga ni rabana ila anayeficha ni confidential ukisali sali sana mumeo nisije kuwa kichekesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…