Huyu trafiki kumkaribia hivi Rais sio hatari?

Iweke tena hiyo clip mkuu
 
Nina hakika yule trafiki hajui wapi anatakiwa apite na wapi hatakiwi apite.

Nilishuhudia tukio moja nilikuwa kwenye hafla fulani hivi sehemu wakaja viongozi,kuna askari wameshika bunduki ati wamekaa wanamtizama yule kiongozi wakati mimi ninachofahamu mlinzi kama mlinzi unatakiwa uwaangalie watu na sio unamuangalia kiongozi.
 
Usiongee sana kuna wauza magenge humu wao wanajiaminisha tuko salama watakuja kukupinga. Tangu ile ziara ya kutoka nchini Kenya tulianza kupiga kelele wale wafanyakazi wa airport waliokuwa wanazubaa nyuma ya ndege wakiwa wamevaa reflectors wakati rais anashuka usiku ule. Na ile style ADC wake na delegates wanavyoshuka ovyo bila mpangilio.

Ule uzi uliweka hiyo video siukumbuki waliokuwa wanapinga waje na hapa wapinge. Maeneo mengi anaonekana ulinzi wake ni wa kawaida sijui wasimamizi ndio wale St. Yohana evening class, yani Konde Boy anaweza jichanga akaweka ulinzi wa kuzuga machoni kihunihuni na tukashindwa kuukosoa kuliko hawa wapokea posho.
 
Naona urefu umemsaidia pia
Ndiyo sifa ya walinzi, sasa kwa mama wamejazana walinzi wafupi halafu ni goigoi kweli sijui ni nani anawaruhusu watu wa namna hii kutengeneza safu ya ulinzi wa mama, hawa walinzi wenye kimo kifupi wakafanye kazi nyingine za kulinda mageti na si kuwa katika safu ya ulinzi wa kiongozi mkuu.

Ulinzi wa mama unapaswa kuwa na watu wenye miraba minne na wakakamavu hivi huyu kiongozi wa hiki kikosi cha ulinzi hajifunzi kwenye mataifa yaliyo endelea? Aone ni sifa zipi zinahitajika kwa walinzi hasa hao escort team ambao wako na mama muda wote ameshindwa kufanya copy and paste kutoka kwa wale walinzi waliokuwa wanatembea na Hayati John Magufuli.
 
Mbona anaonekana kama amepiga TUNGI? Na lengo lake lilikuwa nini na kwanini asipite nyuma ya gari badala ya mbele?
 
Polisi inahitaji reform kuanzia recruitment hadi mental drills.
You can see kisaikolojia huyo trafiki hapo anaonekana ni mpenda sifa haswa.Na alipokumbushwa limits zake na walinzi wa Rais you can see the way he reacted bila utulivu mpaka alipomwona kamanda wake mbele ndio akili ikamtulia.Kakumbuka kumpigia saluti polisi mwenzie lakini yule kanali aliyemfurusha pale alimkimbia tuu na cde anayelindwa kampita tuu.Huyu akarushwe kichura kidogo aisee!
 
Rais nae n binadam Tu Kama Sisi
Kiufupi hawajiamin ndo maana
Walikua na walinz mda wote
 
Kweli kuna yeyote duniani anaweza kumdhuru mama yetu? Kuna yeyote ana uthubutu wa kunyanyua mkono na kumdhuru mama? Hamna kabisa
Wewe diaspora nakuuliza wakati John F. Kennedy anapigwa risasi kuna kenge yeyote alikuwa anapendwa pale States kuliko yeye?
Wakati Ronald Reagan anapigwa risasi pale Hilton Hotel kuna mtu alikuwa anakubalika hata kumkaribia?
 
Naona wale kina mama walikuwa wanashangaa tu na barakoa zao no reaction kabisa labda kidogo yule npambe wa raisi nimeona akishusha mikono kuelejea kiunoni labda kujiandaaa kutoa silaha yoyote (kama kweli alikuwa nayo)
 
alikua ana mkwepa mwanaume mwenyewe silaha
 
Mfumo wa hiyo video. Wengine kwetu haifunguki.. tuambieni ni katika mkutano upi ikibidi tuingie you tube
 
Naona wale kina mama walikuwa wanashangaa tu na barakoa zao no reaction kabisa
Wapo kuuza sura kuna mmoja ni mlinzi naona kavaa kiofisi na katupia kabisa high heels utafikiri yupo kwenye maonesho ya u- miss, mkuu wao ajaribu kuliangalia hili kwa upana zaidi aweke watu walio makini na kazi yao maana wengi wao wanakula posho za bure na kazi hawataki kufanya.
 
Wapo kuuza sura kuna mmoja ni mlinzi naona kavaa kiofisi utafikiri yupo kwenye maonesho ya u- miss mkuu wao ajaribu kuliangalia hili kwa upana zaidi.
Mkuu naomba uniambia tofauti ya huyo mama namna alivyovyaa na hao wengine waliovaa suti kuna tofauti gani mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…