Huzuni/furaha tunazitengeneza sisi katika haya maisha, kila unachodhani kitakupa furaha kipo neutral + SULUHISHO LAKE

Atafute namna nyingi za kupata furaha, asitegemee moja tu
 
Furaha ni hisia nzuri juu ya Jambo au Hali fulani. Furaha ni huja Kwa muda then utoweka. Hi hisia na vile vichocheo vya mwili vinakufanya ujisikie vizuri.

Kwenye maisha jambo la mhimu ni amani na sio furaha. Amani ni Hali ya akili kuamini Iko sababu njema ya wewe kuwa vile ulivyo. Kutafuta sababu chanya kwenye Hali zote na kubaki na tumaini.

Heshima Sheria za asili ili kuipata amani .
 
Mkuu uko sahihi ila mimi huwa naona hakuna haja ya kupima furaha ya mtu fulani kwa kutumia mtu mwingine, yani mfano mtu anasema yeye atakuwa na furaha akiwa na ndoa au mali nyingi hakuna haja ya kumuambia eti kuna mtu anavyo hivyo vyote na hana furaha, na hapo ndipo inapokuja ile kauli ya happiness is subjective sababu tunatofautiana jambo linalomletea au linalomnyima furaha fulani si lazima limletee au limnyime furaha mwingine
 
Umegusia kitu cha msingi sana ambacho ilitakiwa nikizungumze.

ILitakiwa tuweke mjadala wa ni nini furaha,furaha ni nini,hiyo furaha tunayoizungumzia ni nini ?

Binafsi naungana na wewe kwamba ile furaha tunayoexperience katika matukio mazuri ile mimi siiiti furaha naweza kuiita kama stress nzuri.

Furaha kwangu mimi ni ile amani,utulivu wa nafsi na akili inakuwa imetulia kabisa kila kitu unaona kinaenda powa katika ulimwengu.
 
Uchaguzi ni mmoja tu mkuu!

Acha nihuzunike ndani ya DISCOVERY 3 kuliko kuhuzunika kwenye daladala!!
 
Ndio hapo Sasa ukiwa na malengo ya basic life hizo billions utazisikia tu.

Hapo hapo Kwa kipato unachokipata wewe Kuna mtu anasema akiwa na Hali kama Yako amemaliza biashara, anaacha dhambi zote, kazi yake inakua ibada tu.
Atakuwa amelogwa basi 🤣 maana mie mwenyewe kipato hicho hakintoshi. Ukitamani maisha ya juu sana ndio unarisk marinda yako ama maisha kabisa toka kwa mawakala wa kuzimu walioko maeneo mbali mbali nchini.
 
Yeah tunaendelea ku keep it low key. Afterall ku flash maisha huwa sipendagi hizo tabia.
 
Atakuwa amelogwa basi 🤣 maana mie mwenyewe kipato hicho hakintoshi. Ukitamani maisha ya juu sana ndio unarisk marinda yako ama maisha kabisa toka kwa mawakala wa kuzimu walioko maeneo mbali mbali nchini.


Naelewa unachokisema lakini ndio Kuna watu ni maombi Yao Kila siku wawe na maisha kama Yako.
 
hahahahah kweli sikatai ila kwa mtu mwenye familia hawezi ombea kipato kidogo.

Kwa uzoefu wangu, uhalisia wa mambo uko tofauti sana na vitu vinavyoonekana Kwa nje.

Ndio maana mleta uzi kasema itengeneze furaha Yako mwenyewe, ikiwezekana isitegemee vitu au hali.

Unapokuwa shule, furaha Yako ni kufaulu, ukisha faulu unaona si chochote.

Ukiwa kwenye masomo, unatamani upate kazi, ukisha pata kazi unafurahia siku za mwanzo Kisha inakua kawaida.

Hapo unatamani upate usafiri, nyumba, familia n.k

Vyote hivyo vinakupa furaha ya muda mfupi sana Kisha unaona kawaida huku ukiwa na kitu ya kitu kingine unachofikiri kirakupa furaha.

Hapo wale ambao hawana kazi, wanatamani hata ipatikane sehem ya kujitolea tu.

Kuna watu hawana wenza, wanafikiri walipata italeta furaha lakini walio na wenza wengine wanatamani wabaki bila wenza.

Ukiweza kuridhika na kufurahia Kila hatua unayopiga, unawezakuwa mtu mwenye furaha zaidi hata kama hauna vitu vingi.

Haya maisha Hadi unaingia kaburini unakua Bado Kuna vitu unafukuzia vikupe furaha.
 
Yan haya maisha bhana,ukioa mwanamke mweusi utahisi labda ungeoa mweupe ungeinjoy zaidi yan unatamani kujua mweupe ana ladha gani
 
Mkuu umefafanua vizuri sana.

Kuna mama yangu mmoja yeye alikuw a akiona toleo la simu nzuri huwa anatamani aipate na hujisemea kabisa "yaani nikiipata simu ile nitafurahi sana"

Matokeo yake akishaimiliki ile simu baada ya mwezi anatangaza kuiuza keshaichoka,so nilikuwa najiuliza nini shida tena..

Nikaja kugundua hicho kitu kwamba uhalisia wa furaha ni tofauti na vile tunavyofikiria.

Binafsi nimekuwa mtu ambaye ninaweza kujishift pale ninapopitia katika changamoto.

Naweza kuamka asubuhi nikaa nikaanza tu kushukuru Mungu kwa kuwa na ulimi ambao hauna vidonda na naanza kuwaza tabu zinazopatikana mtu akiwa na ulimi wa vidonda,baada ya hapo najisemea asante sana Allah,kisha nahamia kwenye kitu kingine kushukuru na kutafakari,nikipata vitu vuangu 10 tu vinanitisha basi najikuta nina amani na maisha.
 
Yan haya maisha bhana,ukioa mwanamke mweusi utahisi labda ungeoa mweupe ungeinjoy zaidi yan unatamani kujua mweupe ana ladha gani
😄😄.

Yani mkuu ni kuridhika na kile ulichonacho tu.

Na ili uridhike inabidi uone umuhimu wa kile ambacho uko nacho.

Na unaonaje umuhimu ? Utaona umuhimu kwa kushukuru.

Na unashukuru vipi ? Unashukuru kwa kutafakari umuhimu wa kitu hicho.
 
Kuwa na pesa, gari, nyumba sio chanzo Cha FURAHA!
Hata ujekuwa na mabilions of money bado hutaweza kywa na FURAHA ya kudumu!
FURAHA pekee ni Ile inayoletwa na Mungu katika shida na raha bado inakaa nawewe!
Wafilipi 4:4 “Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.”

Warumi 12:12 “kwa tumaini, mkifurahi katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;
 
Utajuwaje kupata bila kukosa?
 
Angalau umenitia moyo kidogo mkuu.

Nilitamani kupata kazi nzuri thanks God kwa kiwangochangu nimeipata.

Pesa ya mboga na mambo mengine ya kimaendeleo vyote sio tatizo tena kwa kipindi chote nitakacho kuwa hapa.

Lakini silali nawaza familia, leave rotation yangu ni kila baada ya miezi minne then na rudi kwa uyo mamaenu mwezi mmoja.

Hapa ninamastres zakutosha hasa inapofika usiku.

Ninamke mzuri lakini simfaidi hukuniliko mawazo chungu kizima hahaa Duuh.
 
Haha si ndio kuna watu wanasema hivyo kwamba kuwa tajiri siyo kuwa na furaha, unaweza ukawa na hivyo yote na bado ukawa na huzuni, sasa ndio watuambie huyu mtu anatakiwa afanyaje
Huo Msemo kujifariji tu pesa inaleta furaha mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…