Naam enhee..?
Yaani hiyo ni uthibitisho kwamba furaha hapo kwenye vitu ambavyo tunatarajia vitupe furaha.
Kama umepata furaha kwa sababu umeoa,au umenunua gari au nyumba basi tambua kwamba hiyo furaha uliyonayo sio kwa sababu ya hivyo vitu ulivyovipata bali ni kwa sababu ya wewe umeamua kufurahi kupitia hivyo vitu.
Kama ingelikuwa ni kweli kwamba furaha inatokana na vitu basi mtu huyo angekuwa na furaha muda wote ambao yuko na hicho kitu,lakini hali inakuwa tofauti hiyo ina maana ya kwmaba hivyo gitu VIMESHINDWA KULETA FURAHA KWAKE YEYE.
Kwanza anatakiwa afahamu kwamba furaha yake ni jukumu lake,na wala furaha yake sio jukumu la ndoa,au nyumba,au utajiri.
Utajiri,ndoa,mwenza,nyumba,pesa n.k hayo yote usiyabebeshe majukumu ya kukupa furaha,hayo yako neutral wala hayahusiki na furaha yake.
Bali yeye sasa ndio anatakiwa ajifurahishe kwa vitu ambavyo yuko navyo na sio kujifurahisha kwa vitu ambavyo angetamani avipate.
Anajifurahisha vipi ? Tutaona huko chini ila kwa ufupi ni KUSHUKURU au gratitude pamoja na tafakuri ya neema hizo.
Yaani pia hiyo ni uthibitisho kwamba pesa haileti furaha,bali wewe mwenyewe namna ulivyo ndio unaleta furaha.
Kama hauna pesa unaweza kudhani kwamba ukizipata utakuwa na furaha,ila cha ajabu ukishazipata tu baada ya siku kadhaa unaanza kuona ni jambo la kawaida sana,taratibu utaanza kuona ni jambo la kawaida,hiyo itafanya urudi katika system ya zamani na utaanza kuwa bored na maisha.
Mtu atatakiwa achague kuishi katika hali ambayo yuko nayo wakati huo kwa sababu sote tunaishi sasa hivi.
SOte tunaishi sasa hivi ndio maana tunavuta pumzi sasa hivi ili tuendelee kusihi.
HIvyo hata furaha ni makosa kuisubirisha wakati ujao ukipata jambo fulani wakati furaha unatakiwa uiishi sasa hivi na sio baada ya kupata jambo hilo.
Mtu mzima anaweza ku experience furaha.
Mtu mlemavu wa macho anaweza ku experience furaha.
Mtoto mdogo anaweza kuexperience furaha.
kIjana na mzee wanaweza ku experience furaha.
Mwanaume anaweza ku experience furaha
Mwanamke anaweza ku experience furaha.
NINI MAANA YANGU ?
maana yangu ni kwamba kila mtu hapo juu ni tofauti na mwingine na utakuta alichonacho huyu mwingine hana lakini je KWA NINI WOTE WANAWEZA KU EXPERIENCE FURAHA LICHA YA TOFAUTI ZAO ?
jawabu ni kwamba wataexperience furaha pale ambapo wataanza ksuhukuru na kuona umuhimu wa vile vitu au hali ambazo WAKO NAZO KWA WAKATI HUO,na sio kwa vitu au hali ambazo wanazitamani za baadae.
Ya kuandika ni mengi sana ila tuanze hapo tu mkuu kama kuna swali sehemu naomba uulize mkuu..