Huzuni/furaha tunazitengeneza sisi katika haya maisha, kila unachodhani kitakupa furaha kipo neutral + SULUHISHO LAKE

Huzuni/furaha tunazitengeneza sisi katika haya maisha, kila unachodhani kitakupa furaha kipo neutral + SULUHISHO LAKE

Ulyaani wewe mkuu nilichogundua unataka uwe na 13B katika akaunti alafu life lako liwe hilo hilo unafanya unachotaka au siyo mkuu ?
Eeh maisha siyabadilishi kwa maana level. Naishi maisha ya kawaida tu ila niwe sikosi chochote nachokitaka kwa wakati. Mi ni mpenzi wa magari na tech.

Sasa ntashindwaje kumiliki gari ya million 25-30 hapo? Inakuwa ni uhakika.
 
Eeh maisha siyabadilishi kwa maana level. Naishi maisha ya kawaida tu ila niwe sikosi chochote nachokitaka kwa wakati.
Una ndoto kama zangu kaka.

Yaani account inasoma billions lakini kama ulikuwx na kawaida ya kukaa kijiweni kwenye kahawa bado unaendelea,kama ulikuwa una kawaida ya kucheza mpira jioni unacheza,kama ulikuwa na kawaida ya kukamua ng'ombe wako maziwa unaendelea yaani harakati ni zilezile huku mpunga ukiwa mrefu.

Nina ndoto ya kuwa na maisha hayo na ninaamini Mungu hana roho mbaya atatupa tu mkuu.
 
Maisha haya haya tu kibongo bongo
Sasa hapo je wewe ukipata nyingi na washikaji zako wa sasa watapata nyingi ? Yaani hizo bata bado itakuwa weekend peke yake au wiki nzima.., na kama wiki nzima je nao watamudu hizo costs au wewe itabidi uwe unatoa offer na ukitoa offer bado watabakia kuwa marafiki zako (real)au watabadilika kuwa machawa wanafanya unachotaka wafanye na kupigana majungu..., na kama hautaweza kuwabeba kila siku kwenye bata je itabidi ubadilishe wadau ambao ukipiga simu mkutane viwanja hawataleta habari za mtoto kukosa karo ?!!!

Kwahio utaona kwamba sometimes more money comes with more problems na huenda associates wako wa sasa wasiwe associates wa baadae kwahio whatever makes you happy now kupata pesa ni ku-assist hio pursue yako of happiness, ingawa huenda kuna watu utafutaji ndio furaha yao hata wakipata ngapi bado ule utafutaji (Adrenalin rush ndio mpango mzima) ila kama nilivyosema awali furaha itakuja pale mtu binafsi atakapoona kwamba amekuwa the best he/she can be kwa kipofu kushiriki mbio za mita mia na kuwa wa mwisho au kuwa disqualified huenda akawa na furaha ya hali ya juu kuliko Hussein Bolt kushinda Olympic ila bila kuvunja rekodi.....
 
Sometimes huwa nawwza nasema kama mungu ananipa pesa nyingi saaana za kunua chochote ninachotaka nahisi maisha yatakuwa boring tu.

Kwa sababu nikishakuwa na pesa ya kila kitu everything kitakuwa ni kawaida kwangu.

Kama magari nitakuwa ninayo ya kutosha hivyo hakutakuwa na jambo jipya la kunipa excitement.

Kama nyumba ni za kutosha,kama vyakula vizuri ni kawaida,sasa ni kipi kitakachonipa furaha tena ?

Hapo ndio nagundua kwamba furaha ni kuamua kufurahia ulichonacho sasa hata iwe nyasi ukiamua kuzifurahia utakuwa na furaha
 
Naam lakini baada ya kupata basic needs huwezi kufarahi wakati tumbo halina kitu au haujui kama ukifumba macho jirani yako hatakuchoma kisu na kuchukua figo yako ili akauze......

Ndio maana nikasema inawezekana kuwa na jamii yenye furaha kwa kuweka misingi ya kuhakikisha watu wanapata basic needs hayo mengine inategemea mtu na mtu...., Mother Theresa huenda kwake kuona watu wengi amewasaidia kutokuwa ombaomba kwake ndio furaha...., Obama pamoja na kuwa Rais huenda leo hana furaha kwa kuona ObamaCare haikufanikiwa..., Mizimu ya Nyerere kama kweli kuna Mizimu huenda leo hii pamoja na watu kumuona kama Baba wa Taifa lakini kwa kuona misingi ya Self - Reliance tumegeuka kuwa Dependent na sio Independent tena huenda akaona all was time wasting..... Hence Ukishapata zile basic needs hapo ndio watu can become the best they can be....

1701003411161.png
 
Furaha ipo ndani ya Tranquilty ya roho, na hiyo unaipata kwa DHIKR' LLAH (Kumbukumbuka Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma, na kuwa conscious nae all the time)
Mimi nina mawazo tofauti kidogo na hii.

Kwa mtu ambaye amefundishwa kuhusu mwenyeziMungu na akafundishwa kumshukuru na akafundishwa umuhimu wa Mungu basi huyo ataipata furaha.

TOkea kuumbwa dunia kuna jamii ambazo kimsingi hawakufikiwa na habari ya Mungu hata kidogo,hivyo sidhani kama walikuwa hawana furaha katika maisha yao.

Sina lengo la kupinga comment yako mkuu ila nakusudia tu kuchagia utofauti wa point
 
Naam lakini baada ya kupata basic needs huwezi kufarahi wakati tumbo halina kitu au haujui kama ukifumba macho jirani yako hatakuchoma kisu na kuchukua figo yako ili akauze......

Ndio maana nikasema inawezekana kuwa na jamii yenye furaha kwa kuweka misingi ya kuhakikisha watu wanapata basic needs hayo mengine inategemea mtu na mtu...., Mother Theresa huenda kwake kuona watu wengi amewasaidia kutokuwa ombaomba kwake ndio furaha...., Obama pamoja na kuwa Rais huenda leo hana furaha kwa kuona ObamaCare haikufanikiwa..., Mizimu ya Nyerere kama kweli kuna Mizimu huenda leo hii pamoja na watu kumuona kama Baba wa Taifa lakini kwa kuona misingi ya Self - Reliance tumegeuka kuwa Dependent na sio Independent tena huenda akaona all was time wasting..... Hence Ukishapata zile basic needs hapo ndio watu can become the best they can be....

View attachment 2825732
Yes mkuu nakubali maneno yako yaaani lazima kuwe na mazingira bora ama mazingira salama,iwe kila kitu kinapatikana.

Kama nimekuelewa unamaanisha kwamba mtu akishapata mahutaji muhimu,usalama wake uko uhakika basi mtu huyo hatakiwi kujifanya ana stress katika mambo mengine wakati mambo ya msingi kabisa anayapata katika mazingira yanayomzunguka
 
Ili mtu kama huyo asiwe bored atahitaji a purpose..., kama ni kusaidia watu, kujielimisha au kufanya utafiti , au jambo lolote.., tatizo wengi wanachase an illusion (wanatafuta kitu ambacho wanadhani ndio wanataka ila wakishakipata wanaona sio hence wanaendelea kuhangaika)

Mfano mtu kama wito wake ni Ualimu na anapenda kufundisha basi furaha yake ni wanafunzi wake ambao walikuwa hawajui A wala B leo hii wanaweza kushuka nondo (na sio kiasi gani cha mshahara wamepata) Daktari ni jinsi gani ameweza kutibu wagonjwa au kugundua njia bora ya kutibu watu (na sio kwanini mwanasiasa anapata pesa kuliko mimi au kwanini sipati overtime)... Nashangaa unasikia msanii analalamika eti anaacha kuimba sababu mziki haulipi (sasa najiuliza hivi huyu hata bila kupewa senti moja asingeimba)?!!!!

Hapa ninakuacha na other wise words....; serenity to accept the things you cannot change, the courage to change the things you can, and the wisdom to know the difference.
 
Pamoja na mambo yoooooote, hakuna zawadi kubwa kutoa na kupewa kama UPENDO

UPENDO unabeba vyote, watu wenye FURAHA haijalishi tajiri au masiki ndani yao kuna UPENDO

Kuna watu wana UPENDO kupitiliza kiasi kwamba akikusaidia mpaka unapata FURAHA ambayo ndani yake unaambatana na UPENDO

Ukitaka kuenjoy maisha, kila kitu chukulia katika sura ya UPENDO
 
Upendo ni nini mkuu ?
 
Sometimes huwa nawwza nasema kama mungu ananipa pesa nyingi saaana za kunua chochote ninachotaka nahisi maisha yatakuwa boring tu.

Kwa sababu nikishakuwa na pesa ya kila kitu everything kitakuwa ni kawaida kwangu.

Kama magari nitakuwa ninayo ya kutosha hivyo hakutakuwa na jambo jipya la kunipa excitement.

Kama nyumba ni za kutosha,kama vyakula vizuri ni kawaida,sasa ni kipi kitakachonipa furaha tena ?

Hapo ndio nagundua kwamba furaha ni kuamua kufurahia ulichonacho sasa hata iwe nyasi ukiamua kuzifurahia utakuwa na furaha
Utakuwa unabadili editions tu
 
Huyo mtu atakuwa na shida basi, yani niamke kwenye account kuna yangu salio linasoma billion 13. Hivi naanzaje kuwa na makasiriko na huzuni?

Internet ipo ya kutosha, naishi comfortable. Siwazi ada za watoto wala kodi ya nyumba. Siumwi chochote mwili wangu uko sawa.
ni kwamba,licha ya kuwa nayo hiyo hela,wasiwasi unakuja kwa vitu viwili,1. utafanyaje huo mpunga ulionao uuendeleze hvo unajikuta unawaza namna gan ufanye ili mpunga wako uendelee kuwa don,unajikuta una stress za namna hyo. 2. ukiwa na mpunga hofu ya kutekwa kuvamiwa na kuuliwa inakuwa ugonjwa wako hvo unakuwa na huzuni kuwa ufanyeje ili uwe safe
 
Basi tumeumbwa tofauti sana yani, mimi kuna mambo nayataka maishani nikifanikiwa hayo wala sitohangaika tena. Ni kula bata hadi uzee tu na kubwa kuliko ni "Mpunga" au "Pesa" ya uhakika hilo ndio la muhimu.

Hayo mengineyo yatakuja yenyewe tu as long as grassess are greener.

Unahitaji pesa au mpunga kiasi Gani ili uwe nafuraha Mkuu?
 
utafanyaje huo mpunga ulionao uuendeleze hvo unajikuta unawaza namna gan ufanye ili mpunga wako uendelee kuwa don,unajikuta una stress za namna hyo.
kwa mtu ambaye hajioneshi utajiri wake hana haja ya stress hizi,ataishi maisha ya kawaida tuu na kufanya kazi za kawaida za kumuingizia kipato.
 
Kama kweli furaha inatokana na kitu fulani ambacho unakihitaji jee kwa nini baada ya kupata kitu hiko bado kuna vitu vingine vitakukosesha furaha na kukutia stress ?

Yaani utajikuta umepata mtoto tayari,lakini kodi ya nyumba inakunyima raha

,je ni ipi faida ya furaha ya mtoto kama furaha hiyo haiwezi kuondoa hata huzuni ya kudaiwa kodi ya nyumba ?

Ni ipi faida ya furaha ya kuwa na gari kama furaha hiyo haiwezi kuondoa huzuni ya kazi nyingi ofisini ?

Ni ipi faida ya kuwa na furaha ya kupata nyumba kama furaha hiyo haiwezi kuondoa huzuni ya kipato kidogo ?

katika haya maisha hicho unachodhani ukikipata kitakupa furaha sio kweli.

FURAHA YA KWELI NI ILE AMBAYO INAKUONDOLEA HUZUNI UNAYOIPATA KATIKA VITU VINGINE.

furaha unayo mwenyewe na wala haipo kwenye vitu unavyovihitaji Kama vile watoto,pesa,nyumba n.k.

Unaweza kutamani gari,ukalinunua na siku za mwanzo ukawa na furaha sana na upya wake.

lakini masiku yakikatika unaliona gari la kawaida hivyo halikupi tena furaha kama ile ya mwanzo,imeenda wapi furaha ile ?

vitu ambavyo tunategemea vitatupa furaha tukishavimiliki tu baada ya masiku kadhaa tunaviona vya kawaida na havitupi tena furaha.

Nilitamani sana kuoa na siku ya kuoa nilikuwa na furaha sana,lakini leo hii sijui furaha ile imeenda wapi na ndoa bado ninayo.

Nilitamani kuwa na mtoto,nilipopata mtoto nilikuwa na furaha sana.

leo mtoto ninaye lakini sijui ile furaha ya mwanzo ya kuwa na mtoto siioni tena na mtoto bado yupo.

Hakuna kitu chochote ambacho ni chanzo cha furaha kwenye maisha yetu isipokuwa sisi wenyewe.

SULUHISHO.

FURAHA TUNATAKIWA KUZITENGENEZA KAMA AMBAVYO TUNATENGENEZA CHAKULA,MAGARI AU NYUMBA.

KUITENGENEZA FURAHA.

furaha tunaitengeneza kwa KUSHUKURU na kutafakari faida ya kitu hicho.

Utakapotafakari faida unazopata kwa kitu fulani na kushukuru basi hapo ndipo furaha utaiona.

Ukiamka asubuhi unaenda kazini kwa daladala sawa hauna gari jee umeshawahi kutafakari kwa uchache umuhimu wa daladala kwako na ukasema asante Mungu..?

Umeshawahi kutafakari kwa uchache umuhimu wa macho yako kwa namna unavyotumia na ukasema asante ?

Je miguu,masikio,pua,mdomo umeshawahi kutakarai kwa ucahche umuhimu wa hivyo vitu kwako kwa namna unavyovitumia ?

Bila kuwa na utaratibu huo utajikuta unaamka kila siku uko bored,hauna mood,hauoni kitu kipya katika dunia na utaanza kudhani kwamba furaha yako kuna sehemu imejificha.

Ukweli mchungu ni kwamba hapa duniani kila kitu sisi ndio tuntengeneza,hata furaha tunatakiwa tuitengeneze wenyewe.
Safi Sana boss kwa elimu tosha!
 
Back
Top Bottom