Chumvi yao
JF-Expert Member
- Feb 27, 2010
- 2,580
- 5,563
Nakuja hapa jukwaani nikiwa na huzuni kubwa baada ya kupata taarifa za msiba kutoka kwa jamaa yangu, aliyepoteza binti yake wa kwanza aliyekuwa anakaribia kufanya mtihani wa NECTA. Binti huyo mwenye umri wa miaka 17 alifariki dunia baada ya kupitia changamoto nyingi za kiafya.
Awali, alikuwa na tatizo la kuganda damu, kisha akafanyiwa upasuaji wa utumbo. Baada ya miezi miwili, alifanyiwa tena upasuaji wa pili, ambao ndio ulisababisha kifo chake. Mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani.
Baada ya msiba huo, kama ilivyo kawaida, hospitali ya Muhimbili ilitoa bili ya zaidi ya milioni 4, huku familia ikiwa tayari imeshalipa karibu milioni 3. Baba wa marehemu ni dereva wa daladala, maisha yao ni ya kubangua hapa na pale. Uongozi wa hospitali ukawaambia wafiwa walete kitu kisichohamishika kama dhamana ili waweze kupewa mwili wa binti yao. Baada ya majadiliano, hati ya nyumba ikatolewa, na wakakubaliana kuwa kiasi kilichobaki kitalipwa ndani ya muda waliopangiwa.
Hapo haikuwa tatizo kubwa. Tatizo lilianza walipoondoka hospitali kuelekea nyumbani kwa ajili ya maziko. Wakiwa njiani, gari yao ilizuiwa na trafiki, licha ya kuwa maiti ilikuwa ndani ya gari. Polisi wakadai kuwa hati za kusafirisha mwili hazijatimia, wakidai kuwa siku hizi maiti zinaibwa.
Wafiwa wakapiga simu hospitalini ili polisi wapate uthibitisho, lakini hata baada ya maelezo hayo, polisi waliendelea kushikilia gari kwa zaidi ya masaa matatu. Inasikitisha sana—katika wakati mgumu wa majonzi, badala ya kusaidia wafiwa, polisi waliongeza machungu kwao.
Swali langu ni hili: Kuna ubinadamu kweli hapa? Je, ni halali kuwachelewesha wafiwa kwa muda mrefu namna hii? Mbona hata nyinyi polisi ni binadamu na pia mnapoteza wapendwa wenu?
Kwa Resma na Ramadhani – polisi wote mlioshikilia mwili wa marehemu kwa masaa matatu – mwaka huu mtaula kwa shida sana