Hydroponic fodder, Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

Hydroponic fodder, Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

ANZA KUFUGA KWA FAIDA SASA.

PUNGUZA GHARAMA ZA CHAKULA CHA MIFUGO KWA 70%-50% KWA KULISHIA CHAKULA CHA HYDROPONICS.

HYDROPONIC UGUNDUZI UNAOMUOKOA MFUGAJI: Hydroponic fodder Ni kizuri zaidi kwa sasa maana Ni nafuu kulinganisha na vyakula vingine
Hydroponic fodder Ni uoteshaji wa mbegu pasipo kutumia udongo kwa muda wa siku5- 7 tu kilo moja ya mbegu za ngano au mtama au shayiri au Mshindi zinaoteshwa kwa kumwagiliwa virutubisho maalum(NUTRIENTS) na kuongezeka kutoka kilo 1 hadi kilo 10 za chakula.
1.Ni nafuu sana kulinganisha na garama za CHAKULA cha madukani au viwandani
2.kina virutubisho na vitamini mara 3 zaidi ya CHAKULA cha kawaida cha Mifugo
3.Hupunguza magonjwa ya mfumo wa hewa kama vile mafua kwa mfugaji na Mifugo kwani hakina vumbi kabisa.
4.kina protein nishati nyingi zaidi mara 3 ya inayopatikana kwenye vyakula vya kawaida vya Mifugo kama kuku,
5.mifugo hukua haraka sana kutokana na wingi wa protein ambayo hufanya Kazi ya kujenga mwili na kukua
6.CHAKULA hiki Ni laini sana na kitam kwa kuku na Mifugo yote
7.mmeng'enyo wa chakula hiki huongezeka kutoka 30% kwa CHAKULA cha kawaida hadi 90% kwa CHAKULA cha hydroponics.
8.kinyesi hupungua na kuwa kati ya 5%-10% tu kwani CHAKULA kingi humeng'enywa na kutumiwa na mwili wa Mifugo
9.mazao kama mayai au maziwa huongezeka kwa 40% kulinganisha na chakula cha kawaida,
10.kiini cha yai la kuku anayelishwa hydroponic fodder huwa cha njano sana hata kama Ni kuku wa kisasa
Hupunguza garama za ufugaji kwenye manunuzi ya chakula kwa 50-75%
FANYA UFUGAJI WA KISASA WENYE GHARAMA NDOGO FAIDA KUBWA.

PIGA simu 0715 601 605

Agiza kitabu kinachofundisha hatua zote za kutayarisha chakula cha hydroponics.(10,000Tsh only)

Agiza Nutrients zakuoteshe fodder yako. Lita 1 ni sh 30,000 tu punguzo kwa zaidi ya lita mbili
 
Wakuu kuna watu walikuwa wanaulizia Shayri, kuna kiasi inapatiakana Arusha kilo ni Tsh 700/ hivyo sema unahitaji kiasi gani, inaweza safirishwa, Shyri ndo recomended kwa ajiri ya Hydroponic fodder kwa sababu ina virutubisho vyote na Kilo 2 ya hydroponic fodder ni sawa na Kilo 1 ya Chakula cha Dukani.

images
Mkuu nahitaji shayiri.
Naweza kupata?
 
@Chasa nimefurahi sana kuona hii technolojia. Nikuulize tu...
1. Je nitakapokuwa natumia chakula hiki, je upo umuhimu wa kutafuta chakula cha mchanganyiko kama ilivozooleka?
2. Hydroponics feeding ina vitamini kwa kiasi gani
3. Tofauti na kuepuka gharama, zipo faida zipi kwa ukuaji wa kuku

Wakuu kunasiku nilipost humu kuhusu Hydroponic techinology, Ila kama ilivyo kawaida yetu thread kama hizi huwa watu wanapotezea, Ila ukweli ni kwamba hii tekinolojia ni nzuri sana na inaweza kuwa ndo suluhisho pekee mpaka sasa la chakula cha mifugo.

Inaweza kukupunguzia gharama za chakula kwa 50% na kama tunavyo jua kwenye ufugaji hasa Kuku chakula kinabeba hadi asilimia 85 ya gharama zote za uendeshaji wa kuku.

110846c.jpg

Kanga wakiwa wanakula Hydroponic fodder.
DIY-Fodder4.jpg

Kuku wakila hydroponic fedder.

HYDROPONIC FODDER inaweza tumika kulishia aina zote za mifugo na hii ni njia rahisi sana na isiyo kuwa na gharama sana.
 
Mimi naomba kuelekezwa zaidi maana nimepitia makala mengi kuhusu hii tekniki lakini bado nina maswali kadhaa mfano,je nahitaji siku ngapi za kuandaa mpaka kulisha kuku wangu hizo fodder maana wengine wanasema siku nne wengine siku 7-9 ,pili je naweza kuwalisha kuku wa mayai(layers) hizi fodder bila kuongeza chakula kingine na wakataga kama wanavyotaga wakipewa kile chakula chao,ntashukuru nikipatiwa majibu.asante.
 
kimsing hakuna specific mda maana hyomimea ikiota unaangalia ukubwa wa majan unayotaka yakikaa mda mref ndo yanakua so chakulacwapata kingi,hii ni compliment ya chakula unachowapa haisubstute so unaeza wapa chakula cha kawaida asubuh jion ukawapa hayo màjan,kuwapa majan pekee kutawanyima virutubisho vngine n so utaathir ukuaj na utakaj
 
2-1-6 hii ni kwajili ya carrot na 2nitrogen,1phosphoric na6Mgnisium hii matumizi yake kwa mimea midogo ni kifuniko kimoja kwa lrt moja ya maji hapo sasa inategemeana na ukubwa wa shamba
Unapatikana wapi Mkuu? Mimi nipo Moshi
 
Wakuu kuna watu walikuwa wanaulizia Shayri, kuna kiasi inapatiakana Arusha kilo ni Tsh 700/ hivyo sema unahitaji kiasi gani, inaweza safirishwa, Shyri ndo recomended kwa ajiri ya Hydroponic fodder kwa sababu ina virutubisho vyote na Kilo 2 ya hydroponic fodder ni sawa na Kilo 1 ya Chakula cha Dukani.

images
mkuu nahitaji shayiri naomba contact zako
 
Let me start by sayn Ive practised hydroponics for more than 2years in Nairobi.Nimehamia Dar and kuna challenges one being hali ya hewa.kuna joto sana na pili nimekosa sehemu ya kununua shayiri(barley).
Hydroponics does well in cooler climates btwn 15°~25° when Dar iko kwenye 30s karibia kila siku.Higher temps inawezesha mould to grow haraka.
Barley is the best cz it grows fast and nutrient content is higher than nafaka mengine
Tried ngano na mtama and results show none is better than the other.
What Id suggest for Dar residents is to add a fan kwenye vyumba vya kuotesha.
Mimi hulisha vifaranga wangu from 2 weeks fodder ya soya hadi week 4..then barley sprouts.
Your comments most welcome.
mkuu ,..soya inaumuhimu gani kulishia vifaranga??
 
Waungwana naamini hamjambo!
Nitangulize shukrani za dhati kwenu wote mnaoutumia mda wenu vyema katika kuhakikisha yale mnayoyaelewa mnawaelekeza wengine.
Leo nataka niwajuze kile nilichokiona baada ya kupata maelezo mazuri kuhusu Hydroponic Fooder.

Kuna mjasiriamali mmoja alitoa maelekezo mazuri kuhusu namna ya kutengeneza chakula bora na kingi kwa mifugo kwa njia ya kisasa. Kweli nilinunua mahitaji na nikajaribu kutengeneza karibia mara mbili, nikawa nakwama.

Baadaye akajitokeza mjasiriamali mwingine akaelezea kwa kina na nashukuru sana kwa sababu alinilenga mimi binafsi kwa kunitumia PM. Nilipojaribu mara hii nilifanikiwa ila changamoto ikaja kwenye nutrients.

Nilifanikiwa kutafuta nutrients na bahati nzuri nikakutana na mtaalam ambaye kweli yeye aliwahi kutengeneza na ana uzoefu; tatizo kwake ni kwamba hana muda wa kufanya kazi hizo kwa sababu ametingwa na ajira. Alinipatia nutrients aina ya DI-Grow Green.

Bwana huyo pamoja na kwamba sikufahamiana naye kabla, alionesha nia ya kutaka kunifundisha na namshukuru Mungu yale aliyonifundisha niliyaelewa vyema.

Leo ni siku ya tatu tangu nimestawisha na naona maendeleo ni mazuri sana. Kwa kila hatua nitakayopitia nitawajuza ili wale wenye nia ya kuyafanyia kazi waweze kufanya huko waliko.

Angalizo: Kuna nutrients ambazo ukizitumia zinaweza zikasababisha madhara makubwa kwa mifugo yako na walaji pia.
Baada ya siku 9 nitakuja na full habari kuhusiana na kile nitakachokuwa nimekizalisha. Wenye nia msikose kuniuliza ili twende wote sambamba kwenye zoezi hili.

Updates 29 March 2017
Kuhusu nutrients
EM imeonesha matokeo chanya kwani inasaidia pia kupambana ma vimelea vinavyosababisha maradhi kwenye mifugo.

Kuhusu wafugaji wengine!
Nilichokiona kwenye field ni kwamba wafugaji wengi hawataki kubadirika toka kwenye hali waliyo nayo ya ufugaji. Unamkuta mfugaji anadai kuwa yeye mifugo yake imezoea chakula fulani hivyo haitaji kuwabadirishia.
Ukweli ni kwamba H-Fodder inasaidia sana kukata gharama za ulishaji. Soma mfano huo hapo chini:-
upload_2017-3-29_1-48-28.jpeg


UPDATES 5 APRIL 2017
Katika mwendelezo wa zoezi la Hydroponics, nimeona matokeo chanya baada ya kutumia nutrients aina ya EmO. Hii ni solutions yenye viumbe rafiki wanaosaidia kushambulia vijidudu vilivyoko kwenye maji na kuvibadirisha kuwa virutubisho kwa mmea. Ni technolojia ya wajapani.
.
 
Mkuu umetumia aina gani ya nafaka?

Natafuta try ni wapi nitazipata?
 
Kwanza nutrients ulo tumia inaitwa DI grow green na sio ID grow.

Zingatia tu hali ya hewa na joto ya mahali unapozalishia ndo jambo la msingi Sio lazima hutumie hyo unaweza tumia booster yoyote ya majan itasaidia kuyakimbiza yakue vyema mimi nastawisha na hata situmii hzo nutrients kutumia nutrients ni kujarbu kuzikimbiza tu ziwah kukua ndan ya muda mfupi ziwe kubwa.
Safi na hongera sana
 
nauza shayiri gunia mbili kwa anayehitaji
Uko wapi na una bei gani? mi nahitaji kwa sababu nimeanza kupata watu / wafugaji wanataka niwandalie chakula kwa ajili ya mifugo yao!
 
Back
Top Bottom