Waungwana naamini hamjambo!
Nitangulize shukrani za dhati kwenu wote mnaoutumia mda wenu vyema katika kuhakikisha yale mnayoyaelewa mnawaelekeza wengine.
Leo nataka niwajuze kile nilichokiona baada ya kupata maelezo mazuri kuhusu Hydroponic Fooder.
Kuna mjasiriamali mmoja alitoa maelekezo mazuri kuhusu namna ya kutengeneza chakula bora na kingi kwa mifugo kwa njia ya kisasa. Kweli nilinunua mahitaji na nikajaribu kutengeneza karibia mara mbili, nikawa nakwama.
Baadaye akajitokeza mjasiriamali mwingine akaelezea kwa kina na nashukuru sana kwa sababu alinilenga mimi binafsi kwa kunitumia PM. Nilipojaribu mara hii nilifanikiwa ila changamoto ikaja kwenye nutrients.
Nilifanikiwa kutafuta nutrients na bahati nzuri nikakutana na mtaalam ambaye kweli yeye aliwahi kutengeneza na ana uzoefu; tatizo kwake ni kwamba hana muda wa kufanya kazi hizo kwa sababu ametingwa na ajira. Alinipatia nutrients aina ya
DI-Grow Green.
Bwana huyo pamoja na kwamba sikufahamiana naye kabla, alionesha nia ya kutaka kunifundisha na namshukuru Mungu yale aliyonifundisha niliyaelewa vyema.
Leo ni siku ya tatu tangu nimestawisha na naona maendeleo ni mazuri sana. Kwa kila hatua nitakayopitia nitawajuza ili wale wenye nia ya kuyafanyia kazi waweze kufanya huko waliko.
Angalizo: Kuna nutrients ambazo ukizitumia zinaweza zikasababisha madhara makubwa kwa mifugo yako na walaji pia.
Baada ya siku 9 nitakuja na full habari kuhusiana na kile nitakachokuwa nimekizalisha. Wenye nia msikose kuniuliza ili twende wote sambamba kwenye zoezi hili.
Updates 29 March 2017
Kuhusu nutrients
EM imeonesha matokeo chanya kwani inasaidia pia kupambana ma vimelea vinavyosababisha maradhi kwenye mifugo.
Kuhusu wafugaji wengine!
Nilichokiona kwenye field ni kwamba wafugaji wengi hawataki kubadirika toka kwenye hali waliyo nayo ya ufugaji. Unamkuta mfugaji anadai kuwa yeye mifugo yake imezoea chakula fulani hivyo haitaji kuwabadirishia.
Ukweli ni kwamba H-Fodder inasaidia sana kukata gharama za ulishaji. Soma mfano huo hapo chini:-
UPDATES 5 APRIL 2017
Katika mwendelezo wa zoezi la Hydroponics, nimeona matokeo chanya baada ya kutumia nutrients aina ya EmO. Hii ni solutions yenye viumbe rafiki wanaosaidia kushambulia vijidudu vilivyoko kwenye maji na kuvibadirisha kuwa virutubisho kwa mmea. Ni technolojia ya wajapani.
.