Hydroponic fodder, Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

Pamoja na ushauri wa tuition ya ana kwa ana humu JF, nashauri watu waingie kwenye YOU TUBE andika chochote kama 'growing soilless wheatgrass' au 'fodders growing', yatakuja mengi.Ukijifunza hayo pamoja na haya humu mwetu JF, nina hakika utapata kitu. Kwa kweli ni process rahisi sana, haina gharama sana LAKINI faida zake kwa mifugo yetu ni KUBWA SANA. Changamkia mwana JF!
 
Sure brother. [emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
By the way hizi ni HYDROPONIC FODDERS na siyo FOODERS! Hii nikuweka record sawasawa in case unataka kuingia kwenye mtandao ingawa utasahihishwa tu ukiingiza wrong thing! Tuko pamoja.
 
Twende sambamba majibu ya maswali yako yatapatikana! Ila binafsi sijafuatilia sana aina za kuku.
 
Si vyema kumlisha fodder peke yake ila kwa kipindi ambacho vyakula vingine ni changamoto unaweza kuwapatia fodder tu!
Ratio iko hivi Fodder kwa layer mash - 2:1 Kilo mbili za fodder changanya na kilo moja ya mchanganyiko huo uliozoeleka.
 
Ahsante sana mkuu, naona wengine wanataka tuendelee kujibu yale yale!
 
inapendeza ila itakuwa na upungufu wa virutubisho kwenye mfugo wako! most of nutrients za H-Fodder ni booster pia kwenye mifugo.
Asante. Ni kwa vipi Naweza kapata barley nikiwa naishi Dar?
 
Asante. Ni kwa vipi Naweza kapata barley nikiwa naishi Dar?
Mi mwenyewe nimeitafuta nimekosa ... nimeshangaa ukiingia sokoni kuulizia shayili unapewa ngano .. hata wafanyabiashara wa nafaka hawaijui hiyo kitu....
Nasikia Arusha inapatikana ila sijapata mtu wa kunihakikishia ...
 
Shayiri kuipata ni shughuli kwa sababu inalimwa na wakulima baadhi kwa ubia na makampuni ya bia (tbl na sbl).. Kisha wanawauzia wao mzigo wote... Tutumie ngano na mtama tu.
 
Shayiri kuipata ni shughuli kwa sababu inalimwa na wakulima baadhi kwa ubia na makampuni ya bia (tbl na sbl).. Kisha wanawauzia wao mzigo wote... Tutumie ngano na mtama tu.
Ahsante kwa ushauri .... ulezi je? na kwa wafuatiliaji ...
Fuatilieni mbegu hizi zinatofautianaje kwenye fodder
Mtama mwekundu,
mtama mweupe
Uwele
Ngano.
 
Mkuu naomba Msada. Hydroponic yangu nilipanda ngano, baada ya siku 8 niliwapa kuku wa nyama wa wiki 2 ajabu waligoma kabisa kula. Inaweza kuwa sababu gani?
 
Mkuu naomba Msada. Hydroponic yangu nilipanda ngano, baada ya siku 8 niliwapa kuku wa nyama wa wiki 2 ajabu waligoma kabisa kula. Inaweza kuwa sababu gani?
Siku 8 kwa ngano inakuwa imeishakuwa ngumu sana ...
Kuku wapatiwe kuanzia siku nne hadi 6 mwisho ...
Nguruwe wapatiwe kuanzia siku 6 hadi 9.
Wanyama wengine ambao ni watumiaji wa nyasi .. hao hata wakipatia iliyokomaa wanakula tu!
Kuna swali jingine mkuu?
 
Mkuu, ngano ya siku 6 inakuwa fupi au kwa sababu situmii nutrition?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…