jameshyela
JF-Expert Member
- Oct 13, 2022
- 2,037
- 15,839
Banda lina umuhimu gani?
Gharama za kutengeneza chakula cha mifungo hautaji kuanza na vitu vya gharama kubwa, muhimu ni kutenga eneo, kisha jenga banda kama la kuku, juu funika kwa plastic pembeni pia funika kwa plastic. Tengeneza vichanja vya miti vya kushikilia tray za bati au plastic. Kichanja kimoja kinaweza kuwa na row tatu, nne, sita au kumi itategemea urefu wa banda lako.
Zipo mbegu na virutubisho vingine unachanganya pamoja kisha unamwaga juu ya tray na kumwagilia maji, baada siku mbili mbegu huchipua na baada ya siku nane tayari unakuwa na malisho kwa mifungo yako. Kumbuka kilimo hiki hakihitaji udongo kuoteshea mbegu.
Ukiwa na banda la futi 20 kwa 10 linatosha kuotesha nyasi za kulisha ng'ombe 50 wakubwa, au kulishia mbuzi zaidi ya 150 kwa mwaka mzima.
Kumbe mkojo wa sungura ni bidha😀Naomba kujua kuhusu soko la mkojo wa sungura.
Sasa hivyo vifaa kama shelf ni special au manmade nyumbani!!?nataka kujuaMkuu hii ni kilimo kizuri sana hasa sehemu zenye shida ya maji, ukivuna maji yako ya mvua yanakutosha musimu mzima,
Eleza vitu kama umeenda shule. Elezea technolojia yenyewe ni nini, inafanyaje kazi na ni vipi inapunguza gharama za kufuga.Wakuu Hydroponic si kwamba ni zao, ni sayansi ya kuotesha mazao kwa kutumia maji na nutrients zingine, yaani hutumii udongo kamwe, na unaweza otesha hata Mboga za kula kwa hii sayansi,
Na mara nyingi inatumika kuotesha vyakula vya mifugo, kuotesha, nyanya, mboga za majani, na baadhi ya matunda.
HYDROPONIC FODDER-Ni kulima/kuotesha chakula cha Mifugo kama vile, Kuku, Mbuzi, Cow, kondoo na kazalika, ila kama ni mboga inaweza itwa hydrponic tomatoes na kazalika,
Hapa jamaa kaotesha mboga zake na anaweza uza bila tatizo
majani ya mifugo
Chakula kama hiki wanaweza kula kuku, Ng'ombe, mbuzi na hata kondoo
HYDROPONIC FODDER, Mara nyingi inapendelewa ioteshwe ngano ya bia au Barley hii ndo ina nutrients zote kiasi kwamba utapata energy, protein, vitamini na kazalika, ingawa hata oats inaweza oteshwa ao hata wheat.