Wakuu kunasiku nilipost humu kuhusu Hydroponic techinology, Ila kama ilivyo kawaida yetu thread kama hizi huwa watu wanapotezea, Ila ukweli ni kwamba hii tekinolojia ni nzuri sana na inaweza kuwa ndo suluhisho pekee mpaka sasa la chakula cha mifugo.
Inaweza kukupunguzia gharama za chakula kwa 50% na kama tunavyo jua kwenye ufugaji hasa Kuku chakula kinabeba hadi asilimia 85 ya gharama zote za uendeshaji wa kuku.
Kanga wakiwa wanakula Hydroponic fodder.
Kuku wakila hydroponic fedder.
HYDROPONIC FODDER inaweza tumika kulishia aina zote za mifugo na hii ni njia rahisi sana na isiyo kuwa na gharama sana.