Asante sana kwa elimu hii. Nimepitia uzi wote na kutafuta taarifa zingine. Hii kitu nimegundua unaweza ifanya kwa kutumia resources ulizonazo.
Ninafanya majaribio kwa kilo mbili hizi za ngano nione matokeo yake yakoje.
Process nayotumia
1. Kuloweka ngano kwa masaa 4 ili kutoa uchafu wa nafaka isiyofaa. Ukiloweka uchafu unaelea, unautoa.
2. Vundika kwa masaa 48-INCUBATION. Unapovundika hakikisha unatumia ndoo ya plastic ili kuepusha kutu. Na iwe na matundu juu kwa ajili ya kupitisha hewa, sababu process hii inahitaji hewa ya oxygen.
3. Baada ya masaa 48. Unaanza kuotesha.
Unatumia tray ya plastic au aluminium(kuepusha kutu). Unapojaza tray, mjazo wa mbegu usizidi nusu inch, na pia tray isizidi inchi 2. Eneo halipaswi kuwa giza na lisipate mwanga wa moja kwa moja. Unakuwa unazinyunyuzia maji kila baada ya masaa matatu, day time, ili kupata unyevunyevu. Tray iwe na matundu pembeni upande mmoja ili maji yatoke. Kuepusha fungus.
Mategemeo baada ya siku Nne unaweza anza wapa kuku.
Nitatoa mrejesho kadri navyoendelea.
Nililoweka jana saa 5 asubuhi na kuvundika saa 9 mchana. So kesho saa 9 mchana masaa 24 yatakuwa yamekamilika. Nategemea kuotesha.
View attachment 1783622View attachment 1783623View attachment 1783624