Hydroponic fodder, Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

Hydroponic fodder, Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

Mkuu kutengengeneza Nutrients si ishu ya kitoto kabisa, ni ngumu sana na ni gharama sana kutengeneza nutrients kwa sababu kuna vitu vingi sana vya kuchanganya, ni lazima uwe na capital kubwa sana kuweza kuchanganya nutrients mwenyewe, uko wapi?

Gharama sana?? Mie nipo Mbeya kwa sasa, wanaposema ni nafuu wanamaanisha nini tena?? Anyway mie kabla sijaona makala yako na kupanua wigo wa ufahamu zaidi niliwahi tu kutengeneza locally kwa kuloweka ulezi mpaka ukachanua na kuku waliushambulia sana. So nikawa narudia na kurudia kwa kutumia biology ya secondary niliyosoma kuwa mbegu kama mbegu hujiwekea chakula chake cha siku saba wakati mimi nawapa kuku baada ya siku tano.

Pia kuna Doctor mmoja wa mifugo nilikutana nae yeye aliniongezea maarifa ya kuongeza ukuaji wa haraka wa hizi foda kwa kuweka nutrients fulani hivi zinaitwa DI Grow au Super Gro ambazo zenyewe hazina madhara kwa mimea, mifugo na binadamu. Nayo ilisaidia ulezi kukua kwa haraka ndani ya siku tatu nawapa kuku

Na mwisho alinifundisha kuepuka fangasi basi niwe naziosha mbegu kwa maji ya malimao ni hayo tu. Hii makala yako imenifungua mengi hasa baada ya kusoma kwenye mitandao zaidi ugomvi ni hizo nutrients, ina maana huwezi kutuwekea hapa formula yake tukasoma tukaelewa!! Ndiyo maana ya mitandao mkuu ni kurahisisha mambo ikiwemo muda na gharama
 
Habari wakuu,

Nimenza kutoa elimu ya uzalishaji wa chakula cha Kuku, Mbuzi, Nguruwe na Ng'ombe kwa kutumia Hydroponic, na nilisha wahi kuielezea hapo nyuma.

Hydroponic fodder inaweza kukupunguzia gharama za Chakula cha kuku wa asilimia zaidi 60% kitu ambacho ni cha kipekee kabisa, na Nguruwe kwa zaidi ya asilimia 40% Ng'ombe asilimia 50%.

Kwa sasa anaye hitaji kufundishwa kwa vitendo itambidi awekeapoint ment na kuna gharama za kulipia na vilevile naweza kukufanyia instalation huko uliko kwa gharama za maelewano, na vilevile utapata vifuatavyo.

1. Nutrients ambazo zinapatikana

2. Trays

3. Barley Seeds

NB: Huu mfumo hata kama unataka kulima Mboga za Majani pia unakaribishwa. na Kuna Business plan yake pia.

Nitafute 0783-69-10-72
 
mkuu. Chasha ungeboresha huu uzi kwa kuweka zile picha maana kuna wengine bado hawaelewi hii kitu
 
Last edited by a moderator:
pia ungetuwekea na gharama za mafunzo na vifaa,mi nipo mwanza

Mkuu gharama zina tofautiana na kuhusu vifaa naweza kukufdundisha ukatumia vifaa vinavyo patikana huko kwenu Mwanza, but labda mbegu ya bare na Nutrients ndo pekee unaweza pata kwangu kama huko hazipatikani.
 
Mkuu unaweza itumia hii Hydropodic folders peke yake kuwalisha nguruwe bila bila suppliments nyingine kama pumba na wakakua fresh? Ni kweli unaweza tumia eneo la ekari moja kulisha ng'ombe zaidi ya 300?
 
ya mkuu huhitaji kuwapa chakula kingine labda tu uamuwe mwenyewe kufanya hivyo, hata kwa Kuku huhitaji kuwapatia msosi mwingine
 
Habari wakuu,

Nimenza kutoa elimu ya uzalishaji wa chakula cha Kuku, Mbuzi, Nguruwe na Ng'ombe kwa kutumia Hydroponic, na nilisha wahi kuielezea hapo nyuma.

Hydroponic fodder inaweza kukupunguzia gharama za Chakula cha kuku wa asilimia zaidi 60% kitu ambacho ni cha kipekee kabisa, na Nguruwe kwa zaidi ya asilimia 40% Ng'ombe asilimia 50%.

Kwa sasa anaye hitaji kufundishwa kwa vitendo itambidi awekeapoint ment na kuna gharama za kulipia na vilevile naweza kukufanyia instalation huko uliko kwa gharama za maelewano, na vilevile utapata vifuatavyo.

1. Nutrients ambazo zinapatikana

2. Trays

3. Barley Seeds

NB: Huu mfumo hata kama unataka kulima Mboga za Majani pia unakaribishwa. na Kuna Business plan yake pia.

Nitafute 0783-69-10-72

Duuh mkuu nimeipenda hii inabidi nikutafute tuone unatusaidia vipi kwa sisi ambao tupo mbali na Arusha.
 
weka zile picha kuna mtu nataka nimuomyeshe
 
Pls chasha ungeweka na bei ingekuwa Pouwah sana kwa sababu mtu anaweza toka mbali kuja. Huko ulipo halafu kumbe kaja na hela kidogo nje ya kiwango chako so ungerahicsha kwa kututajia baadhi ya gharama ....
 
Kiasi cha "crude protein" kwenye hiki chakula, ni asilimia ngapi?
 
Back
Top Bottom