I am depressed. Naombeni ushauri

UBINAFSI WA MWANMKE ULIANZIA HAPA!!!!
Kulikua na mantiki gani yeye kumpa wazo mumewe wakati mshahara wake kwa saving hata ya miezi 6 wangepata wakunza biashara?
Halafu sina imani na mwandishi kama kweli mwanmke!!
 
Hivi mil 2.3 + laki nane kwa mwezi mnapata sh. ngapi?, huyo mtoto mmemtafutia shule ya milion ngapi, huko kwenu wewe mwanamke unasaidia kila siku? hamlipi kodi mnakaa bure, bado asumbuke kwenda kuomba mtaj kwa kaka zake? wewe mchango wako ni kutoa huo ushauri? ulimkalia kooni kuhusu kiwanja akatunza hela mwezi mmoja wewe ulitunza sh. ngapi kwa huo mwezi kama na wewe kweli uko serious kupata kiwanja, hivi unajua hiyo nyumba unayokaa na mume na mumeo sio yako? siku akidondoka utafukuzwa maana mumeo haikujenga Amka tumia akili, kwenu huwezi kumaliza kusaidia tengeneza future ya watoto wako, usiseme sijakuambia, hiyo depression unajitafutia mwenyewe
 
Kibongo bongo hili ni gumu sana ~ kupanga kabla ya kuoana huku kwetu ni jambo ambalo limekaa mbali mno na upeo wetu wa kufikiri
Ni mpangilio tu mkuu hata kibongo inawezekana
 
Tunakwenda kwa kutegemea kudra kudra tu.
Ni kama hatujui maisha ni nini, na nadhani hili linachangiwa sana na wazazi . Ujue mzazi wa kiafrika anaweza kuwa anamlipia mwanae ada kubwa sana shuleni lakini hajui hata ni kwanini mwanae huyo anasoma!

Nakumbuka miaka ya ujana wangu wakati naoa, fikra yangu kubwa sana ilikuwa ni mwanamke anizalie watoto halafu baas 😆. Undani wa majukumu hasa ya baba na mama katika kuijenga familia sikuwa nawazia saana Wala kudadavua akilini hadi nimekuja kupata mtoto wa pili keshakuwa tunataraji kuongezea watatu, majukumu ya shule yanadai ada, uniforms na mengineyo ndio akili inakaa sawa.

Mzazi ambaye hawezi hata kukagua ni nini mwanae anaandika katika madaftari yanayogharimu pesa nyingi. Mzazi asiyeuliza mwaswali kwa mwanae, kama vile unasoma ili iweje? Unatamani uje kuwa nani?
 
Kuna rafiki yangu Mtanzania anaishi Australia aliniambia yeye hata kuoa alijiuliza sana kwa nini aoe? Mpaka akajiridhisha.

Baadaye akajiuliza sana kama anataka mtoto, kwa nini azalishe mtoto, kuzalisha mtoto katika dunia ya leo ni kitu sahihi ama la, alifikiria saana mambo hayo kabla ya kuamua kuwa na mtoto.

Bongo watu wengi hawafikirii mambo haya, yanatokea by default tu.
 
shule alisuggest yeye kwa kuwa alikuwa anataka shule iliyo chini ya kanisa.
 


Ushauri upi unataka, hujasema unataka nn..!!
 
Asante kwa ushauri. Kukopa bank hataki na hata kukopa kazini kwao hataki anasema hataki kujiingiza kwenye mikopo. sijaomba ushauri kwa yoyote nahisi nitadhalilisha familia.
 
Shida naiona kwako Na Sio Kwa mumeo unamforce mumeo aishi Maisha ambayo Hana uwezo nayo na hayaendan Na kipato chake,pia umemnyang'anya mumeo nafasi yake kwenye nyumba......wewe ndo umekua mwanaume uko ndani Na unataka mumeo akutio weeewe Na kufanya kila unachotaka ....badilika mrudishie mumeo nafasi yake alafu Uwe Na utulivuu ....kuwa mwanamke acha mumeo awe mwanaume....ukiendelea ivi ndoa inaweza vunjika
 
Una mshahara wa 2.3 m, yeye ana mshahara wa laki 8. - ndio na kama umesoma kuna sehemu nimemmjibu mtu kuwa mshahara wangu ninakatwa

Umefungua biashara yako bado changa.

Umempeleka mtoto shule ya gharama ila wewe utachangia usafiri na uniform.

Umempa wazo afungue biashara ila mtaji akaazime kwao.

Ushauri wangu mpende mume wako kwani mpo pamoja ila sio wamoja.

ndio ila kama umesoma kuna mtu nimemjibu kuwa mshahara wangu ninahudumia wazazi wangu pia ninakatwa bima ya wazazi na mkwe kinachobaki ndo kinawekwa mezani kama familia. Pili biashara nilichukua mkopo kazini ambapo pia nakatwa na nilimshirikisha. nimempa wazo la biashara ila mtaji akaazime kwa kuwa kinachobaki hakitoshi kufungua hiyo biashara kwahiyo ili kitoshe inabidi kuazima au kukopa ambapo yeye hataki kukopa.
 
Hapa unakosea mkuu. sijawahi mforce kufanya kitu tunafanya kwa uwezo wake na sio uwezo wangu. hata hiyo shule alichagua yeye na sio mimi. kwa kifupi nyumba imetawaliwa na mume wangu mimi nipo chini yake sijawahi kujikweza hata siku moja.
 
ndio kwetu mimi ndo tegemezi tupo wanne lakini mimi ndo tegemezi. kuhusu mchango tulifungua UTT account mimi nilichanga miezi yote 12 ya mwaka 2024 kulingana na kiwango tulichokubaliana lakini yeye aliweka mwezi mmoja nikimkumbusha anasema niachane na hayo mambo.
 
UBINAFSI WA MWANMKE ULIANZIA HAPA!!!!
Kulikua na mantiki gani yeye kumpa wazo mumewe wakati mshahara wake kwa saving hata ya miezi 6 wangepata wakunza biashara?
Halafu sina imani na mwandishi kama kweli mwanmke!!
rejea majibu niliyotoa. kuhusu jinsia mimi ni mwanamke.
 
Mgogoro upo katika kuvutana, he is not motivated.. Hajalelewa hivyo. Soon atakuona una gubu.

Fanya hivi, lea mshahara wako, lea biashara yako.. Save kidogo kidogo nunua kiwanja uanze kujenga mdogo mdogo. You are on your own… Labda atakujoin baadae.

Ulishawahi sikia single mother ndani ya ndoa? ndio wewe. Kama unampenda na hayuko violent ishi nae hivyo hivyo, utavikwa taji 😀
 
Tatizo la wanawake wengi ni wabinafsi sana sasa mama unashindwa nn kumpa mmeo mtaji mbona huo mshahara wako ni mkubwa sana tu.Kopa apo benki milioni kumi ndani ya miaka miwili umemaliza maarejesho mpe mmeo maji ndo maisha yenyewe hayo punguzeni ubinafsi wanawake.Yani ni mwanaume tu ndo anaweza ishi na mwanamke asiyekuwa na pesa ila mwanamke akiwa na pesa ni masimango na manyanyaso kwa mwanaume.Wanaume tutafute pesa kwa udi na uvumbi.
 
Wewe umeshajua uhalisia
Tatizo sio haya aliyotuandikia tatizo ni yeye kuwa juu ya maamuzi Kama ulivoandika nimeandika pia
 
Pole umeolewa na bomu aisee..mimi na shida zangu za kiafya lakini nimekataa kubaki home tu kusubiri huruma ya ndugu na hata nikioa siwezi kukubali kukaa home mke wangu ahangaike hilo halipo asee.. nipo napambana na maisha na mdogo wangu namsaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…