I am depressed. Naombeni ushauri

umemuelewa lakini?
 
Pole Dada,Depression sio kitu chepesi hivyo.Ni shida kubwa inayoweza kupelekea kujitoa Uhai!
Tafakari Hilo shimo unalotaka kujichimbia bila sababu!
Nakusihi ridhika na ulichonacho,usiyatafute makubwa.Kufosi lazima lakini usimpeleke puta sana huyo jamaa,yeye ndio atatangulia kupata depression.
Mwenzako yupo kwa Mama yake Hana wasiwasi,mtoto ni sehemu ya familia Yao.
Mshahara wako ukijipanga unaweza ukajenga Nyumba ya uwezo wako kwa ajili ya mwanao,kama mama mkwe wako alivyofanya kwa mwanaye.
Jamaa akiona umuhimu wa kujenga,atajenga tu!
Uliambiwa shule ya kanisa,zipo pia za bei nafuu sana!
Dada kupanga ni kuchagua,usimpe stress mtoto watu Wala na wewe usijipe stress.
Katoto kamoja tu kanawahangaisha watu mko above 40+!
Kingine kuishi nyumbani sio udhalili,watu wa nje wasiwape presha.

Nawatakia furaha na lastborn wako,huyo hahami hapo!..Tena kama ndio kina sisi wa Magomeni,kkoo na ilala ndo usahau kabisaa!
Furahia Maisha dada,depression kitu kibaya saana.
 
Yani mimi kila siku nasema ningekuwa mwanaume mke wangu marufuku kujiunga na magroup ya wamama......wanadanganyana sana na kupeana negative energy.
Wakati mwingine mtu anayeshauri hata ndoa hana.

Maisha ya sasa bila kusaidiana hamtoboi......na mara nyingine mke unaweza kukuta anabeba 70% ya majukumu ya familia ila anakausha tu na siku zinaenda.
 
Watoto wengi hapa bongo ni wale wa kwa bahati mbaya 😄
 

Ushauri ni mgumu sana, sidhani kama Mme wako ana shida kubwa, mwanaume ukiwa huna hela ya kueleweka na mke ana kipato kikubwa ni changamoto sana!

Tatizo lako sio kubwa kama unavyofikiri, tatizo lako lipo kwenye misingi ya kiuanawake na kiuanaume, Hakuna mwenye kosa hapo!

Kwa umri ulio nao upo matured enough na unaweza work around hayo mazingira, 2.5m ongeza laki 8 na Kodi hamlipi; Hakuna sababu ya kumsukuma huyo jamaa kwenye biashara, ni kwamba unataka uhuru na fedha zako.
 
umemuelewa lakini?
Nimemuelewa sana, uzuri anajua mume hana passion ya biashara kuanzia mwanzo, hawezi kumlazimisha.....dawa ni kutumia vipato walivyonavyo kufanya maendeleo ya kiwango chao.....from there mume anaweza kubadilika.
Sasa hivi mume hawezi kutafuta pesa kwa nguvu kwa sababu hana project ya kumuumiza kichwa inayohitaji pesa.....so mshahara unamtosha.

Mi ningemshauri yeye atake a lead indirectly.....like amshauri mume wangu unaonaje tukisave kila mtu laki na nusu kwa mwezi halafu mwisho wa mwaka tununue kiwanja.....akikubali yeye mke anaongeza kiasi cha kusave baada ya miezi lets say 6 anamwambia mume wangu pesa hii, tukatafute kiwanja.....(Muda huo ana options za maeneo anayoyataka)
Kuanzia hapo mume anaweza kuanza kuchangamsha kichwa....

Ila sio anamwambia ooh wanaume wenzio wananunua viwanja wanajenga wee upo tu🤣🤣🤣🤣 atajua hajui.
 
Nimesema machache tu mkuu. Mshahara wangu ndo unalisha wazazi wangu , kulipa bills zao na ninakatwa bima yao na ya mkwe pia kwahiyo kinabaki kiasi kidogo cha fedha ambacho ndo tunatumia kwa pamoja na yake kwa familia.

Acha ndoa kakae na wazazi wako, wewe una Matatizo makubwa sana, na unakatisha tamaa watu kuoa, jamaa wa watu anateseka kuliko wewe!
 
Ila wanawake wanajitoa sana kwenye majukumu aisee.

Sasa anamkomalia mwamba ndo afungue biashara yake na sio waongeze nguvu kwenye hiyo yake kama yeye ana idea hizo za biashara basi watumie akili ya mke.

Kuna familia mume hayupo kabisa kwenye mambo ya biashara yeye ni kilimo tu, mambo ya kuzurula kwenye biashara kamuachia mkewe.
 
Ni mapungufu tu mkuu, sio kila mwanaume anawaza kua kama Bakhresa. Akizidi kumlazimisha ndo mwanzo wa malumbano ilhali mke anaweza kufanya yake, taratibu tu jamaa akiona progress atatia mkono wake.

Wanaume hasa wenye mapungufu fulani hawapendi ukweli na hawapendi kuambiwa fanya hivi. Japo ni ushauri ila yeye ataona kama dharau na amri.
 
Nimesema machache tu mkuu. Mshahara wangu ndo unalisha wazazi wangu , kulipa bills zao na ninakatwa bima yao na ya mkwe pia kwahiyo kinabaki kiasi kidogo cha fedha ambacho ndo tunatumia kwa pamoja na yake kwa familia.
Si umesema kipato chako yaani take home ni 2.3m? Kwa hiyo pesa ni ndogo sana?
Mmeo laki 8 + 2.3 m = 3.1 m
Halafu unaleta gazeti? Relax
 
Tena mkipatana watu mnaoweka mipango pamoja kutoboa ni chapchap , lakini mkianza ubinafsi na uchoyo shida huanzia hapo,
 
Depression? Mishahara laki8+m ara m 2.3? Mtaji wa biashara mnataka utoke nje ya familia,Tena kwa kuazima...wanawake mnakuwaga wabinafsi sana,sasa usiombe huyo mumeo awe kashagundua huo ubinafsi na kuukatia tamaa kuwa kwa ubinafsi huu hatutofika popote...anasubiri tu useme tuachane,akujibu kwa kifupi tu 'sawa'...halafu baadaye uje kugundua kuwa mwamba alishatega mitego yake vizuri tu, na alijiandaa vizuri kuishi bill wewe.
 
ajira za connection hizo 😂😂 mimi sina ajira rasmi lakini huenda nikawa nawazidi maendeleo
 
Nimehisi hivo maana mwanaume akishagundua mke ni mbinafsi , basi hajitumi kwa lolote ana relax kabisa , na angegundua wapo pamoja basi jamaa angechacharika hata kidogo , Mamy K amelielezea vizuri , kwanza kashangaa bibie anatoa mawazo halafu anashauri mwenzake akakope kwao , mtoto wanae mmoja kipato 2.3M +800k wanashindwa kujipanga na kiwanja hawana,
 
unanikandamiza kwa kuwa nimesema kipato changu mkuu? nimejibu hapo juu shule ni ya kanisa na alishauri yeye mtoto aende shule ya kanisa. hapo tatizo ni mimi kivipi?
Mkuu sema tu ukweli,
2.3+0.8=3.1 mnaiweka mezani na kuipanglia?
 
Umesema ni last born!! Aah dada pole tu kwakweli. Hapo huna namna zaidi ya kushikilia tu usukani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…