I am depressed. Naombeni ushauri

I am depressed. Naombeni ushauri

Yan unajua kbsa umemzid mumeo mshahara then unakuja na matakwa kibao...unajichagulia the easy way out...lipa ada mm ntalipa usafiri na uniform!!

Hv unajua akili zetu wanaume zinavyofanya kazi kwel!?

Swal moja naomba kukuuliza...hyo shule ni nani aliye suggest!?
 
hakuna mwanamke duniani ataweza kuishi na mwanamme ambaye amemzid kipato ivyo kosa kubwa sana yeye kukwambia mshahara wake ushauri hapo hakuna ndoa kwa kuwa mwanamke anahitaji atawaliwe sio kutawala bila Mungu kuwa ndan yenu basi no love no ndoa
 
Habari great thinkers.

Nimekuwa msomaji kwa muda mrefu sana humu, ila imenilazimu nijiunge ili nitoe nilichonacho maana ninahisi kuzidiwa moyoni sipati kulala usiku. Nahitaji ushauri.

Mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miaka 6, nimeolewa miaka 8 iliyopita, nyumba tunayoishi tumepewa na mama mkwe kwa hiyo hatujajenga na wala hatulipi kodi. Najua unajiuliza hizi information za nini leta hoja, sawa nakuja na hoja.

Ni hivi mume wangu ana kipato cha kawaida tu kwa mwezi labda laki 8 take home. Binafsi nina kipato kwa mwezi kama 2.3m take home. baada tu ya kufunga ndo mume wangu alipoteza kazi kwahiyo alikaa nyumbani kuanzia 2017 akaja kupata kazi 2021 lakini tuliiishi bila shida.

Yeye kwao ni last born ana kaka na dada. Mimi kwetu ni wa pili kuzaliwa ila nahudumia wazazi pia. Kipindi yupo nyumbani ni kamwambia aongee na kaka yake amuazime mtaji wa kufanya biashara lakini mwenzangu alikuwa akikaa kimya, so miaka ikaenda mpaka alivyokuja kupata kazi.

Mwaka jana mwishoni nikagusia tena na kumpa idea ya biashara na alionekana kuipenda sana akasema sawa, na hiyo mwaka jana nilimwambia kwa kuwa mtoto anaingia darasa la kwanza hatuwezi kutegemea mshahara pekee. Ingawa mimi nimefungua biashara ila bado changa na pia ninafanyaga tender za kuprint, kufunga zawadi na kadhalika.

Mtoto tumemtafutia shule kwa pamoja na ada alikuwa anaijua tangu Novemba, nikamwmabia ngoja nikupunguzie mzigo nitalipia usafiri na uniform akasema sawa.

Nikawa namkumbusha kulipa ada anasema anakumbuka. juzi jumapili anasema hiyo ada kubwa sana hatoweza hiyo shule, imagine bado wiki shule zifunguliwe.

Baadae nikamuuliza kuhusu ile idea ya biashara vipi? mana haijalishi mtoto anasoma wapi jinsi anavyozidi kukua madarasa ndivyo gharama zinazidi, akasema mi mambo ya biashara siyawezi wala sijawahi kuyawaza, duuh nikabaki nimetoa macho, nikamuuliza mbona ile idea uliipenda na ukasema utaifanya utamuazima kaka yako mtaji akasema mi siwezi hayo mambo.

Haa, moyo wangu uliinama sana tangu hiyo siku nina mawazo sipati usingizi. Najiuliza niongee na kaka yake au dada yake wamshauri kama hawezi kutegemea kukua kimaendeleo kwa mshahara tu au nibaki nalo? na nikibaki nalo nifanyeje?

Hawazi kujenga, hawazi kununua kiwanja, 2024 january nilimwambia tuweke kiasi cha fedha kwa ajili ya kununua kiwanja akaweka mwezi wa kwanza nadhani kwa kuwa nilimkalia kooni.

Baada ya hapo akawa hawezi kuna siku nikamuuliza akasema mi niache tu na hayo mambo. Nikaacha nikaendelea mwenyewe, ila peke yangu nguvu ni ndogo.

Naombeni ushauri jamani mimi ni mtu mzima nina 40+ nashindwa kuomba ushauri wa rafiki zangu mana ndo yataenezwa.

Nadhani ninaweza pata depression kama ningebaki navyo moyoni kichwa kinauma kwa kuwaza.

Naombeni ushauri tafadhali.
Kama una miaka 40+ mbona changamoto ndogo ndogo zinawasumbua unazani biashara ni ya kila mtu MSHUKURU MUNGU amekwambia mapema mwingine Anaweza kulima, kuchunga n'gombe kusimamia shughuli Fulani na vingine binafsi naomba jambo la kawaida sio vyema
 
Nunua kiwanja kwa sababu mshahara wako unaruhusu. Kama mwenzako hajaamka utasubiri aamke, anaweza kuja kukumbuka shuka kumeshakucha

Fanya hivi kwa ajili ya mwanao. Life goes on, mwache aishi anavyotaka yeye.

Ila vitu unavyonunua andikisha majina yako na mtoto wako, kisha weka hati ummya kiwanja mbali huyu kifaza kisije kuuza

Unakaaje nyumbani 40+, hapo ndipo tatuzo linaanza
Ukiufuata ushauri huu unakaribisha changamoto nyingine ........hauna Afya ya ndoa yako.
 
Duuuuh. Pole Mama.

Usipate presha wala stress.

Kama wewe unaweza kufanya biashara, wewe fanya. Kama anaweza kukusapoti na hakuzuii.
Muhimu zingatia upendo kutoka kwake na wewe Muheshimu hivyo hivyo alivyo. Hayo ndio mapungufu yake.

Mfano.
Kuna familia moja Baba mwenye nyumba hafanyi Kazi yoyote na sio kwamba hana nguvu hapana yupo vyema Kabisa. Yeye ni mitungi muda wote. Mama ndio anapambana, ila huwezi amini ukiwakuta wanavyoishi, Mama humwambii kitu kuhusu Mzee na Mzee humwambii kitu kuhusu Mke wake.

Na familia yao imebarikiwa.

Asante
 
Ukiufuata ushauri huu unakaribisha changamoto nyingine ........hauna Afya ya ndoa yako.
Sasa unataka nimshauri nini? Wew unaona myu yulo 40+ bado wako nyumbaji

Pili bado mshahara 2.3 na hana maisha ya kutengeneza ya baadae

Tatu kashazungumza sana na mume wake

Sijamshauri aachane na mume wake, nimemshauri atengeneze maisha ya mwanane...afya gani ya ndoa walati ndoa yenyew hapo ilipo haina afya
 
Pole.
Mimi naona hamna haja yeye kuanza kuzunguka kwa kaka yake kuomba mtaji. Nyie wawili kama mke na mume ndio mlitakiwa msaidiane kwa kila hali. Mngetafuta namna ya kutumia mshahara wako na wake mpate ya biashara na msiwe na biashara ya mke au ya mume kuweni na biashara ya familia.
😊😊😊 una akili mno.
 
Mshahara wako 2.3m
Mshahara wa mume 800k
Ada alipe mume wewe ulipe nauli na uniform.
Umri 40+
Kitendo Cha kumzidi mume mshahara tu kila atakalofanya mwanaume kwako halina maana kiufupi lazima ulazimishe mwanaume afanye unavotaka wewe.
Lazima uwe na stress kwa sababu shida Wala sio hizi ulizoeleza shida ni mwanaume amegoma kuendeshwa ni kwamba Kuna namna unataka mwanaume afanye kwa mawazo yako, Kama unabisha inaingiaje akilini watu wenye 40+ washindwe kuelewana ndani ya nyumba mpaka uandike kuomba msaada online!
Jibu ni kuwa wote mnajiona kichwa wa familia.
Hebu kuwa mke wa familia Kama utapata stress.
 
Pole.
Mimi naona hamna haja yeye kuanza kuzunguka kwa kaka yake kuomba mtaji. Nyie wawili kama mke na mume ndio mlitakiwa msaidiane kwa kila hali. Mngetafuta namna ya kutumia mshahara wako na wake mpate ya biashara na msiwe na biashara ya mke au ya mume kuweni na biashara ya familia.
Nahisi hili yeye halitaki anataka kila mmoja aingize cha kwake sio kutegemeana kwenye kitu kimoja, mimi ningemshauri tu hamvumilie jamaa labda kuna mambo anayaweka sawa bila kujitangaza tangaza ikifika muda atamwambia tu
 
Nadhani mnaishi ki vampire hasa wewe yawezekana ndo una sauti kuliko yeye(sina hakika)
Mwanaume mwingine anaweza kujifanya anakuunga mkono ili kuondoa kero zako ambazo akikupinga inakuwa wimbo ili kuepusha hayo anakukubali without any Action na muda mwingine anasahau kabisa kwamba mmewahi jadiri kitu flani.


Kaa nae vizuri ongea nae vzr mpe utawala wake kama mme muulize yeye anapenda kitu gani na usikurupuke jifanye kama huna habari na yote haya.

Kuhusu mtoto Msikilize yeye anataka shule ya kiwango gani cha ada na yeye ana ngapi na muafikiane shule ipi nzuri mkubaliane kwa pamoja. Wanawake wengi mnapenda kuiga kila kitu hapa ndo kuna tofauti sana na wanaume wewe unaweza kuvutiwa na watoto wa shost yako tu kisa wanasoma sehemu fln ukataka nawewe wa kwako waende hapo bila kujari hali ya uchumi mlio nao wewe na mmeo.

Usiombe hela kwa kaka zake. hata yeye ana akili usimuendeshe unavyotaka wewe bali kaaeni kama mme na mke myajenge.Hakuna mtu wa ku solve matatizo yenu isipokuwa ninyi wenyew
 
Sasa unataka nimshauri nini? Wew unaona myu yulo 40+ bado wako nyumbaji

Pili bado mshahara 2.3 na hana maisha ya kutengeneza ya baadae

Tatu kashazungumza sana na mume wake

Sijamshauri aachane na mume wake, nimemshauri atengeneze maisha ya mwanane...afya gani ya ndoa walati ndoa yenyew hapo ilipo haina afya
sawa
 
Back
Top Bottom