You are right dada angu. But one thing - ni lazima wazo litangulie kabla ya mtaji.
Reginald Mengi alishawahi kulizungumzia hili:
Kwa habari kamili, soma
hapa
Ni kweli kuwa kwa sasa hivi huna mtaji, ila kujiajiri kunaanza na
spirit ya tafuta uhuru wa kiuchumi (financial freedom) na sio mtaji. Kwa sasa unachotakiwa kujenga ni
spirit ya kujiajiri na kutafuta
mawazo mazuri ya kibiashara, alafu ndio
unatafuta mtaji.
Mtaji haujawahi kuwa tatizo hata siku moja kwa mtu mwenye nia ya dhati. Wanaokwambia kuwa hawana mtaji ndio maana hawawezi kujiajiri, wawekee question mark. Wahenga walisema "
penye nia pana njia" na hili mimi naliunga mkono 100%.
Ukitaka kujua kuwa capital is not everything, ngoja nikupe mfano halisia wa rafiki yangu anayefanya kazi CRDB.
Huyu jamaa nimesoma nae toka Form I - IV, tumesoma nae darasa moja, course moja hapa UDSM miaka mitatu. Na pia tulikua tuna-share kitanda kimoja tangu tupo form I - ni mtu wangu wa karibu sana.
Tulipomaliza chuo, mimi nikapata offer kufanya kazi CRDB, lakini kwa vile sikupenda kuajiriwa, nikampigia pande ile nafasi, akaipata. Analipwa gross ya 1M.
Hapo alipo, anauwezo wa kuchukua mkopo wa 30M+, kwa riba ya 6%. So akichukua 30,000,000 atarudisha na riba ya Tsh 1.8M - which is a nothing for a 3+ years loan.
Hivi wangapi leo wakiwa na nafasi ya kuchukua mkopo kama huu - watakubali ? na ni wangapi watakataa?
Lakini nakuambia, ni miaka nenda rudi, huyu jamaa hachukui mkopo, na tena anataka kuhama hapo, amepata post nyingine watampa 1.2M Gross.
To me, he is just as stupid as other stupids. Tatizo ni kwamba, huyu jamaa hana
spirit wala
wazo la biashara - na wala hataki
kuthubutu kufanya hivyo.
Matokeo yake, wanaopata mikopo wanaishia kununua magari na wakati hawana chanzo kingine cha fedha zaidi ya mshahara ambao unakatwa kila mwezi kulipia mkopo!
Kwanini usiwekeze alafu faida ndio uitumie kununulia gari?
Kama ni kweli Carmel unataka kujiajiri siku za usoni, basi mtaji usiuone kama tatizo. Asikudanganye mtu,
unapokuwa na wazo zuri, hela inakuja yenyewe bila hata hodi!
Mimi wakati naanza kujiajiri nilikuwa sina hata Tsh 10. Ushauri niliokupa hapo juu, hata mimi nilipewa na watu wazima waliofanikiwa kibiashara. Nakumbuka kuna mzee mmoja entrepreneur aliniambia "
Money has never been a problem" - and now I see this is very true!
Aliniambia "
tafuta wazo, kama litakuwa ni zuri, hela itakufuata"
Then nikaanzia hapo, nikatafuta wazo - I thought of writing a software for hospitals, kwa sababu nyingi zilikua haziko computerized.
Next month, nikakutana na mkurugenzi mkuu (Jina la hospitali naliweka kapuni kwa sasa), ilikua ni kama bahati tu maana huyu jamaa ni mtu adimu sana. Nikampa wazo langu, ila nikamwambia kuwa "mimi ni kijana nimemaliza chuo, sina mtaji ila nina uwezo wa kufanya kazi na nina mawazo mazuri ya kibiashara kwenye software development."
I am telling you, it took him only 10 minutes, yule mzee akaniambia - "Nataka tuwe patners, niambie gharama za kutafuta ofice na kila kitu" - tukabadilishana namba za simu.
Kwa vile nilikua mwoga sikutaka nipoteze ile chance, nikambambia kuwa 10M ingetosha kufanya project ya miezi minne pamoja na gharama nyingine za internet, office n.k.
He wrote me a 5M cheque the next monday kwa kuanzia, na nyingine niipitie after 2 weeks. Nilipokwenda after two weeks, nikakuta tayari ameshatafuta office na kila kitu - akaniambia hiyo 10M ilikua ni yangu kwa ajili ya kufanya kazi na kununua vitu kama computers n.k. I was supprised!
That's how a started a business to this day. Nilianza kujiajiri kwa staili hiyo. Nauhakika, kama ningekuwa nasema siwezi kujiajiri sababu sina mtaji, nisingefika hapa nilipo hii leo.
And today, I am sharing the very same thing I learned:
"Money has never been a problem in this world. If you are determined and full of innovative ideas, money will follow you always"
GOD bless you.