Mangi Pole sana!
Hebu tafuta fedha kwanza aisee mambo ya huyo kwanza yaweke pembeni! Yaani miaka minne keshakusahau! Shukuru Mungu sana kajionyesha mapema maana ungekuwa uashaoa huyo binti afu mkatenganishwa ungekuta nusu ya watoto sio wako! Kaz buti Mangi ongeza kipato then atatokea mmoja utakayempenda kwa dhati naye atakupenda kwa ampenzi ya ukweli. Kumbuka Mke mwema utapewa na Mungu nami naamini Mungu hakuchukii hivyo mwombe naye atakupa mke mwema!
Kwa wale vijana wa zamani jee yupo aliyewahi kusoma kitabu "great expectations' cha Charles Dickens? Kuna kibibi kimoja ilikuwa kiolewe na mjamaa basi kikaachwa solemba siku ya harusi. Tangu siku hiyo aliamua kubaki na veli lake, akasimamisha mkono wa saa usitembee tena na akabakisha kila kitu kama kilivyokuwa siku na saa ile ambayo alitakiwa aolewe. Nimemsahau jina maana nimekisoma miaka mingi sana nyuma.
Sasa wewe kama unataka kubaki umeganda kwenye muda kama kile kibibi endelea tu.
Pole sana kaka, hayo mambo yapo sana tu, mimi mwenyewe niliwahi kuathirika kama wewe. sikutamani kupenda tena wala sikujua kama anaweza kutokea wa kumpenda. lakini Mungu ni mwema alinipatia yule aliyenichagulia na si mimi niliyemchagua. hakuwa riziki yako mkabidhi MUngu muda ukifika atakupatia yule aliye sawa na wewe.