Mathew mambo,
Nikisema hakuna mwanaume ambaye ameshaniumiza moyo ntakuwa muongo. Sitasema ukweli wangu wote hapa ila kuna huyu mmoja alishanitenda baada ya kumaliza chuo........sababu sikuwahi kufikiri kuwa alinichukulia kama kiburudisho na sio mchumba.... kwa wakati ule niko mschana niliumia sijapata ona. Wanasemaga hakuna maumivu makali kama kuzaa, sijawahi pitia hicho kikombe siweze bisha ila maumivu ya kutendwa ninayajua na Mungu wangu, nilitoa hadi chozi lenye upinde wa mvua maana yake ilifika wakati nalia ila machozi hayatoki, yalikauka.......
Nashukuru Mungu nilipata rafiki wa kike alinipa maneno ya Mungu ya kunifariji na kuniambia songa mbele Kasie msahau wala usihangaike nae...... hadi kesho hata nikikutana nae namuona kama abiria wengine tuu tunaokutana nao kwenye treni ya kwenda kwetu Tabora kila mtu anashuka kituo chake hatujuani kila mtu na lake. Tangu hapo, nikayasemesha mapenzi na kuyaambia, watu wanakuja na kuondoka, wema kwa wabaya; akija mwema mwenye mapenzi ya kweli nambwagia moyo wangu, akija heart-breaker nitasikitika badala ya kuumia na kuachana nae na kwenda au kukaa mbali nae.... ntajishughulisha na mambo yangu yananonipa furaha na kugeukia marafiki hata wa salamu tuu maana wapo wengi till Mr. wema comes again. Nilishaacha kubembeleza mapenzi ati mtu haeleweki anapendwa mara aone yeye hotcake mara yuko busy.....mara hapokei simu, mara hajibu meseji hakwambii tatizo nini anakaa kimya tuu, namuacha aendelee na yake atapata wa kubembelezana nae huko mbele. Mahaba nayajua sana ila.... mapicha picha ya kitoto toto siyawezi.
Na ikitokea huyo mwanaume aka niumiza moyo au kunivunja moyo, wala siwezi leta hisia hapa, kwanza huwa sitaki zikae, nahakikisha nimezipeperusha na mziki, kucheza, kuimba, safari, kupika nakuwa fresh maisha yanaanza upya wala sisemeshani na mtu. Dooh, hivi nilisema sitasema ukweli wangu hapa eeehh huu mwingine naubakisha kwa Muembe Dodo wa Kasie.
Mathew, Kasie sio mschana ni kigagulaa nasubiria pensheni mwenzio. Mapenzi kwangu ni jina tuu ila ukinitajia Mahaba..... hayo nayatandikia mkeka, nakaa kitako, nachukua ungo na kuweka nafaka ndani yake naanza kuchambua na kupepeta.... Mahaba siyaachi hadi ntaporudisha namba ila mapenzi nawaachia nyie vijana.
To be honest am another creature, watu niliokutana nao na tukawa na ukaribu kila mtu alisema lake kuhusu Kasie, wengi wananiambiaga hutazeeka wewe kwa staili ya hivyo ulivyo, mie nabaki natabasamu tuu eehehheee.
Sina jibu direct who really Kasie is... but she is Matata the K'.
Ciao.