I have been scammed 1,100$ through Forex

I have been scammed 1,100$ through Forex

Pole saana Bro. Hii kitu ya tuma pesa nitrade nikupe faida asilimia fulani baada ya muda fulani on top of your Capital , Huwa naiona ni approach mbovu kuliko zote kwenye game ya Forex.
Approach sahihi ni wewe mwenyewe kujifunza strategy mbali mbali mpaka upate inayokufaa na yenye kuleta faida kwako.
Na pia ukiangalia Forex kwa jicho la kamari bro , ni bora uiache tu ufanye mambo mengine kwasababu utapoteza pesa nyingi saaana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, hongera kwa kutupa somo kwa gharama zako, gharama uliyolipa ni kubwa kama ukijitazama peke yako ila ukifikiria wanaonufaika na elimu hii, ni wengi mno. Hakika hili somo utakuwa umeelewa vizuri na pengine hutakaa usahau. Pia nakupongeza kwa kutufundisha nasi tukapata somo kwa gharama nafuu zaidi ya kuwa na internet pekee.

Nikukumbushe tu kitu kimoja, chochote kinachokuja kirahisi, pia huondoka kirahisi. Halafu tamaa huwa inaondoa akili ya kuchanganua mambo. Hebu fikiria huu mfano uliopewa kwamba eti ukiweka $2000 baada ya mwezi utapata faida 500%, maana yake ni $2000 + (500/100*2000) = $12000, faida kwa mwezi ni $10,000. Hii faida kila mtu angeikimbilia, hata Warren Buffett. wakati mwingine tujifunze kwa waliokwisha kupata hela nyingi.

Hakuna pesa nyingi inayoweza kupatikana kwa njia za shotcut na njia za panya, zikawa na usalama ama zikadumu. hata matumizi yake huwa na njia kama zilizotumika kuzipata.

Pole sana ila kwa niaba ya wenzangu watakaopata somo hili na wakaelewa, tunashukuru mno.

Ubarikiwe sana.
 
Jamaa alivyo ambiwa kuwa akiweka $2000 ndani ya siku 14 atapa 500% nafikiri alianza na kuulizia bei za Range [emoji23][emoji23]

God save us
Anazani yeye ndo mjanja dunia hii, hao Wanaigeria na Waghana na Wakenya watawatapeli sana vijana.
 
Kila mtu na ujinga wake ndugu sema wengine hawaongei
Tatizo lako kubwa ni tamaa, una ndoto kubwa na uvivu wa kutumia njia ndefu ya uhakika kufikia malengo.
Forex sio tatizo, tatizo lako kutaka mtu watu wafanye trading kwa niaba yako.

Sikusemi vibaya ila ukiendelea na attitude hiyo ktk utafutaji utapoteza pesa nyingi sana na kuishia ktk umaskini.
 
Tatizo lako kubwa ni tamaa, una ndoto kubwa na uvivu wa kutumia njia ndefu ya uhakika kufikia malengo.
Forex sio tatizo, tatizo lako kutaka mtu watu wafanye trading kwa niaba yako.

Sikusemi vibaya ila ukiendelea na attitude hiyo ktk utafutaji utapoteza pesa nyingi sana na kuishia ktk umaskini.

IMG_6929.JPG
hii haina mjanja wala mjinga angalia jamaa kilichotokea no the same like me nisingetoa tahadhari kuna wengine yangewakumba humu na wangekaa kimya
 
Kwa maelezo yako inavyoonekana kwanza hauna knowledge ya FOREX wewe ni wale watu waliosikia au kuona mtu anapiga hela fx ukaamua na wewe kuanza trade bila kuwa na knowledge nzuri itakayokuwezesha wewe ku trade kwa profit kubwa na loss ndogo .

USHAURI.
FOREX ni nzuri na inalipa kama kwanza utawekeza muda wako kwanza kuisoma na kisha kufanya tradings ndogo ndogo ili ku grasp knowledge vizuri na pia kupata experience so fanya haya .

1).Soma kupata elimu yake na pia uwe mfuatiliaji mzuri wa matukio bali usiyategemee mno kwenye kila trade yako.(matukio ninayoyaongelea hapa ni taarifa za habari hasa zinazohusu uchumi wa nchi nyingi hasa zilizoendelea kwa kuwa ndiyo controllers wazuri wa market).

2).Tafuta strategy nzuri kati ya ulizosoma na ambayo unaona umeielewa vizuri kisha practice na hiyo strategy throughly ili kuielewa zaidi na kisha ifanye strategy yako ya kila siku.

3.Epuka kutumia bots,narudia tena epuka kutumia bots!!
Kama ulikuwa haujui zile ni codes zilizoandikwa na programmers,tu ambazo zinafuata kile ambacho zimeelekezwa na huyo programmer so hazina uhalisia na real time trendings.

4.Epuka kufungua orders nyingi kwa wakati mmoja jitahidi sana zisizidi tano na hata kama utaaamua kufungua nyingi hakikisha stratergy yako umei comfirm. Na una uhakika na unachokifanya.

5.Zingatia Risk Managents,hapa naongelea .

*Usitumie lotsize kubwa mno hapa unajiweka kwenye risk kubwa ya kuchoma hela yako.
*Zingatia Stop loss.

6.La mwisho USIMUAMINI MTU KWENYE HELA hao scammers wamekuibia kwa kuwa unapenda mteremko mkuu .

Mwisho kabisa nikutakie trading njema.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona namba +1 asilimia yote huwa ni scammer namba hii ni unknown code phone za kulipia.sio kwenye trader tu hata biashara za manunuzi ya vitu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom