I want to die a judge

I want to die a judge

STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA MIA MOJA (FINAL EPISODE)

TULIPO ISHIA SEHEMU YA TISINI NA TISA.............

“Fungua milango yote ya nyumba hii” aliamuriwa hakuwa na namna ya kufanya alienda pembeni ambapo palikuwa na kibox kidogo kuna namba aliziingiza milango yote ikafunguka, Jamal alimtanguliza makamu wa raisi mbele huku yeye akiwa anafuata nyuma kwa umakini, wakati wanafika nje kuna kifaa kidogo alikirushia ndani ambacho kilikuwa na nguvu kubwa mno kililipuka kwa sauti na kufanya umeme kuzima humo ndani shoti ilianza kutokea wakati huo alikuwa amemlaza chini makamu wa raisi baada ya kukikata kichwa chake na shoka ambayo aliikuta hapo nje mwanaume alitoka na kupanda kwenye gari yake kisha akaanza kutoka hapo kwa spidi huku nyuma mjengo huo wa pesa nyingi sana ukilipuka kwa ile shoti kubwa iliyopiga hakuna kitu hata kimoja ambacho kiliweza kubaki kikiwa salama pale.

Sasa alikuwa anaenda kukutana na master mind wa mchezo Nicolous Philemone waweza kumuita mwanasheria mkuu wa nchi ya Tanzania au Makubiri Yanick mzee wa karata tatu maeneo ambayo mtu huyo alikuwa anapatikana alikuwa anayajua vizuri sana baada ya kupewa taarifa za kujitosheleza kabisa na Alexander, usiku huo wa manane majira ya saa 9 alikuwa anatoka Chanika kuweza kuwahi Buguruni sokoni alihitaji usiku wa leo uwe ni usiku ambao hauta sahaulika kabisa kwenye vichwa vya wananchi wa taifa hili.

FINAL.....................................

Mrembo wetu Catherine alikuwa ameshaingia ndani ya ardhi ya nchi ya Tanzania tayari mpaka muda huo hakujua atampatia wapi mwanaume wake huyo na ambaye ndiyo ilikuwa sababu ya yeye kuingia ndani ya nchi hii japo alijipa imani kwamba lazima angempata tu, alijipa imani baada ya kuingia Tanzania na kuweza kuiona ile taarifa ambayo raisi aliye jiuzulu akitangaza wazi kwamba mtu huyo alikuwa amerudi rasmi na hakufa kama watu wengi walivyokuwa wanafikiri. Alikuwa ametulia kwenye Bar moja maeneo ya nje kabisa ya airport ambapo alikuwa ameshuka kwenye ndege tangu aianze safari siku ya jana yake. Alikuwa anaucheza mchezo wa kubahatisha baada ya kuja Tanzania kwa mara ya kwanza Rashid alimpatia namba ambayo Jamal huwa anaitumia hapa nchini kwa siri sana ni watu wachache mno ambao alikuwa akiwapa hiyo namba, hiyo namba ni kweli alikuwa nayo alijaribu kupiga mara kadhaa alitaka mtu huyo apokee ili aweze kujua yuko wapi kwa huo muda ila mwenye simu hakufanya kama ilivyokuwa imetegemewa na mwanamke huyo alipiga mara nyingi sana lakini simu haikupokelewa kabisa.

Mwanaume alikuwa yupo njiani akiwa kwenye kasi sana alisikia simu yake inaita ndipo alipokumbuka kwamba tangu ampigie Alexander wakati anaenda kwake alikuwa ameisahau humo humo kwenye gari, namba ilikuwa ngeni na hakuwa na imani sana kama ilikuwa ni namba ya Tanzania kwani zilikuwa ni code za nje kabisa, aliangalia alikuta hiyo namba imempigia mara nyingi sana basi akapokea simu yake hiyo.

“Jamal” alisikia sauti ya kike upande wa pili hakutaka kujishughulisha nayo aliikata simu yake na kuiweka mfukoni kwani alihisi huenda ni mtu anahitaji msaada wa haraka ndiyo maana aliikata alivyo ona alicho kihisi kilikuwa tofauti, baada ya kuona ameitwa tu jina lake alihitaji kuimaliza kwanza kazi yake hizo simu angezishughulikia baadaye alikuwa na vita nzito sana mbele yake ambapo alikuwa anaenda kukutana na mtu aliye ambiwa ndiye mwanadamu hatari zaidi kwenye nchi hii. Upande wa pili Catherine alibaki anaongea pekeyake lakini alimshukuru MUNGU baada ya mtu huyo kuweza kuipokea ni kitendo cha dakika moja tu aliweza kuona sehemu ambayo simu hiyo ilikuwepo kwa uelekeo ambao ilikuwa inamuonyesha baada ya kuweza kuihaki, cha ajabu ilionekana kuwa karibu sana na eneo ambalo yeye alikuwepo aliangalia barabarani aliona kuna gari moja tu nyeusi ilikuwa inapita ikiwa kwa kasi sana alijua yes simu ilikuwa kwenye ile gari alisubiri kuona kama gari hiyo inakimbizwa lakini haikuwa hivyo ilikuwa yenyewe tu japo mwenye hiyo gari alionekana kuwa mtu mwenye haraka kupitiliza.

Hakutaka kuzubaa tena hapo alilipa na kutaka kuondoka majira hayo ya usiku wa manane alishangaa anazuiliwa mbele na wanaume kama sita hivi, alikuwa ni mwanamke mrembo sana kumuona peke yake majira hayo ya usiku ilikuwa ni lazima mtu rijali udenda umtoke ndicho kilicho wapata wanaume hao walihitaji kumchukua iwe ni kwa kumlipa au kwa nguvu mwanamke huyo aende kuwaridhisha nafsi zao. Kilicho wakuta kilifanya kila aliyekuwa ndani ya hiyo club akimbie na kuitafuta njia yake alibadilika macho yake yakawa yanawaka kama moto aliwaua kikatili sana watu hao akachukua pikipiki ambayo hata hakujua ni ya nani aliondoka nayo kwa kasi sana na alama ya hiyo simu ilipokuwepo ilionekana kumuacha mbali kidogo lakini alikuwa na uhakika wa kuipata kwa sababu ilikuwa bado inaonekana kwenye kioo cha simu yake.

Jamal alienda kulisimamisha gari lake maeneo ya Buguruni sokoni ikiwa ilikuwa ni saa 11 kasoro za asubuhi alikuwa na hamu kubwa sana ya kuonana na huyo mwanaume ambaye ndiye alikuwa chanzo cha kila kitu kibaya ambacho kilikuwa kinaendelea nchini, alitembea huku na huku kweli aliweza kuona neno GANGSTER EMPIRE likiwa limeandikwa kwa herufi kubwa alisogea na kubonyeza hiyo switch baada ya dakika moja alitoka mwanaume moja mwenye suti ambaye hata hakumuuliza aliishika shingo yake na kuinyonga akawa anamburuza ili amuelekeze sehemu ambayo bosi wao alikuwepo, baada ya kuingia ndani kabisa taa ziliwaka ni kama alikuwa anasubiriwa kwa muda mrefu sana kufika hapo, aliimalizia shingo ya yule mlinzi ambaye alikuwa amekuja kumfungulia. Hapo ndani kulikuwa na wanaume wa shoka wasio pungua 50 wote wakiwa kwenye suti nyeusi ila mbele ya hapo alipokuwa amesimama yeye kulikuwa na meza kubwa sana ya kifahari na kiti chake ambacho kilikaliwa na mtu aliyekuwa amempa mgongo, aliangaza juu alipokuwa ameambiwa ni kweli aliona kuna kibox cha kioo cha bei ghali sana ndani kulikuwa na fuvu la mtu alizikunja sana ngumi zake mwanaume huku akiwa anauma meno kwa hasira sana leo asingeruhusu mtu atoke humo ndani japokuwa milango iliachwa wazi kwa mara ya kwanza kwenye jengo hili.

Mwanaume aliyekuwa amempa mgongo alimgeukia na sura hiyo alikuwa ameiona mara moja tu pekee ile siku ambayo alienda Colombia na mtu huyo akamuonyesha sura tatu ambapo nyingine alikuwa anaijua Alexander na Julius Makasi tu ila hii ya kuwa na karata ndiyo ilikuwa sura yake halisia umri ulikuwa umeenda hakuwa mnyonge kwenye kuyaishi maisha marefu huyu kiumbe.

“Nashukuru sana kwa kuniletea huo mkufu ambao nimeutafuta kwa muda mrefu sana bila mafanikio na nimeua watu wengi sana ili tu niupate huo sasa naenda kuitawala dunia na kuwa mtu mwenye pesa sana hahahaahhahahahaahhahahahh” alicheka sana mzee huyu akiwa anazichezesha karata zake za hatari sana kwenye mkono wake wakati mwenzake alikuwa ana machungu na majonzi ambayo yasingeweza kusimuliwa, michezo ya huyu mtu ndiyo ilimfanya aweze kuikosa familia yake lakini pia aliwakosa karibia watu wake wote wa karibu mpaka ndugu yake wa ukubwani Rashid alikuwa ameuawa vibaya mno Jamal alikirusha kisu chake kimoja kwa nguvu sana kuelekea kwa mzee huyo kilidakwa kwa dharau sana tena kwa vidole viwili tu.

“Stooooooooooop” ni sauti ya mamlaka ambayo ilisikika kutoka kwa mzee huyo akiwapa onyo vijana wake wote humo ndani ambao walikuwa ni hatari sana hakuhitaji yeyote amguse Jamal.

“Nilikuwa namsubiri leo nataka nimuonyeshe namna watoto wadogo wanavyotakiwa kuwaheshimu wakubwa zao kwenye haya maisha” aliongea akiruka kwenye meza na kusogea mbele kidogo alikuwa akitumia karata zake kujipepea na alihitaji yeye mwenyewe kwa mkono wake amfunze Jamal.

“Ulijua kama nakuja hapa?” Jamal aliuliza kwa gadhabu

“Tangu unaingia kule Chanika nakuona wale wajinga hakuna kitu walikuwa wanakifanya mimi nisijue kwahiyo ile nyumba yote nilikuwa naiona kila muda ndio maana haujakaa sana nje kijana alikuja kukuchukua kwa sababu nilijua utakuja leo” alielezewa kitu ambacho kilimshangaza alijua amefika kibabe sana kumbe alikuwa anasubiriwa ndiyo maana amepata bahati ya kuongea na kiongozi huyo kiwepesi sana namna hiyo.

Jamal alikuwa mwenye uchungu sana alijirusha kwa mateke yenye spidi za hatari kama matano alipiga hewa alijizungusha double kick na ngumi nzito sana alipiga hewa akaishia kushushia teke lake kwenye meza ambayo ilipasuka, Jamal alishangaa mtu ambaye alikuwa anpambana naye alikuwa hana uwezo wa kumfikia pale alipo hakuwa wa kawaida kama alivyokuwa anafikiria yeye alifumba macho na kutoka kwa spidi kubwa sana alimzunguka mtu huyo na kumgusa kwa nguvu na vidole vyake ili ampoozeshe alishangaa yupo vile vile hakuna kinacho badilika alijirusha samba soti ambayo alifanikiwa kuzamisha teke moja ambalo lilionekana kumwingia mtu huyo wakati huo ilifuatiwa na urushaji wa sindano ndogo ambazo zilikuwa na sumu kali sana pia alishtuka kwa mtu huyo zilikuwa hazifanyi kazi alichoka na kuogopa mno.

“Bwana mdogo hapa umekuja kufa mwili wangu una nguvu za ziada ambazo mimi sitakiwa kupigana na mwanadamu wa kawaida kabisa kama wewe ni mtu mmoja tu pekee ambaye anaweza kunipiga mimi kwenye huu ulimwengu” baada ya kumaliza kuongea mzee huyo alijirusha kwa nguvu na kupotea alivyokuja kutokezea mbele Jamal alikuwa amechanwa na karata sana kwenye mikono yake na miguu yake ambayo ilikuwa inamuwasha vibaya mno aliukaza mwili wake na kwenda kwa mwanaume huyo alidondokea ukutani baada ya kukutana na karata tatu kwenye uso wake ni wazi alikuwa ameelemewa sana.

Alinyanyuka huku akitema damu kwenye mdomo wake mkono wake mmoja ulikuwa chini akiwa anamwangalia mzee huyo kwa uchungu mkubwa alikuja akiwa anajiviringisha na kisu chake mkononi huku akiwa anaongeza kasi kila alivyokuwa akisogea alikutana na ngumi za shingo zilizomfanya akatoa sauti ya maumivu mkono wake uliteguliwa vibaya mno alishindiliwa mateke na ngumi tano kwenye kifua chake alikuwa akitapika damu Jamal hali yake ilikuwa mbaya sana alijitahidi kunyanyuka na kujaribu hahati yake kwa mara ya mwisho alizungukwa kwa kupigwa ngumi nyingi sana kisha alichomekwa visu viwili kifuani na kubetuliwa kwa mtama mkali, alikuwa yupo chini akiwa anaona kwa mbali hakuwa hata na uwezo wa kuendelea kujitetea mwanaume alikutana na mwanadamu ambaye alikuwa ana uwezo wa nguvu za kurithi kutoka huko Japan.

Makubiri Yanick alijirusha akiwa anamuonyesha Jamal kilipo kichwa cha baba yake alikitoa kidani kwenye shingo ya Jamal na kukiangalia sana akiwa mwenye kicheko dakika kadhaa tu zilimuwezesha kuishika hiyo hazina kubwa sana ya nchi, alichomoa upanga wake ili kuitenganisha shingo ya kijana huyo na kiwili wili chake ili akakiongeze hicho kichwa ile sehemu ambayo kilikuwepo kichwa cha baba yake Jamal mzee Jonson Malisaba ambaye alikuwa marehemu mpaka muda huo. Upanga ulishushwa kwa nguvu ila kabla haujatua kwenye hiyo shingo walisikia kelele kali sana ambayo ilimfanya Makubiri Yanick mwenyewe adondokee mbali, alishtuka sana baada ya kuiona hiyo sura hapo mbele yake huyo hakuwahi kukutana naye ila picha zake alikuwa akizijua muda mrefu sana ndiye binadamu pekee ambaye alikuwa anamuogopa na ndiye mwanadamu ambaye alikuwa ana uwezo wa kumfanya kitu chochote kile.

Catherine alikuwa ameingia hapo ndani, simu ambayo Jamal alikuwa anayo mfukoni ndiyo iliyo muwezesha kujua kwamba yeye yuko wapi alienda kupiga magoti alipokuwa amelala mwanaume wa ndoto zake alimkumbatia mwanaume akiwa anatoa damu nyingi sana kwenye mwili wake hakuwa akijitambua kwa lolote lile wakati huo, mrembo Catherine alitoa machozi ya uchungu sana alikuwa akimpenda mno mwanaume huyo alipiga makelele ya kutisha humo ndani kila mtu alirudi nyuma macho yake yalikuwa yanawaka moto aliuokota upanga ambao alichomwa nao Jamal na kuushika kwenye mkono wake kwa nguvu. Alikuwa anapotea na kuonekana kila baada ya sekunde moja wanaume wote 50 waliokuwepo humo ndani licha ya kuwa wapiganaji wakubwa sana hakuna ambaye alipata hata nafasi ya kuweza kurusha hata ngumi walijikuta anadondoka mmoja mmoja kila mtu alitamani sana aweze kupata nafasi ya kukimbia mauaji yaliyokuwa yanafanywa na mwanamke huyo yalikuwa yakitisha mno, kuna watu walikuwa wanakufa vichwa vyao vikiwa vimetenganishwa na mwili, kuna wengine vichwa vilipasuliwa kati kati wengine viungo yao hawakuwa navyo kwenye miili yao mpaka muda huo.

Makubiri Yanick alijishangaa baada ya kugundua kwamba alikuwa amebaki mwenyewe alimeza mate kwa nguvu na kuijaribu bahati yake kama anaweza kupata nafasi ya kukimbia humo ndani mkufu alikuwa nao mkononi tayari hakutaka kuzubaa alikuwa anazijua vizuri sifa za kiumbe ambacho kilikuwa mbele yake. Aliufanya mwili wake kuwa na joto kali ambalo kama akikugusa basi ungehisi kwamba anakutengenezea shoti kwenye mwili wako alijirusha kuelekea alipokuwepo Catherine hakubahatika hata kufika alipigwa mapigo sita kwenye sehemu tofauti tofauti za mwili wake alianza kutetemeka sana mwili wake ulikuwa na baridi kali mno ule moto ulikuwa umepotea akiwa anatetemeka alihisi kuna kitu kinapenya kwenye mwili wake panga lile lile ambalo alilizamisha kwenye mwili wa Jamal lilizama pia kwenye kifua chake alitaka kuongea neno macho yake yalimuua mno kuangaliana na macho ya Catherine lilikuwa ni kosa yalikuwa yanaumiza sana na haikutakiwa kuangaliana naye machoni ilikuwa ni sawa na mtu anaye chomelewa kwa gesi alipiga kelele sana alishtukia mkono wa Catherine umezamishwa kwenye kifua chake moyo ulitolewa na kukanyagwa chini mpaka ukapasuka, alikufa akiwa nashuhudia moyo wake haupo kwenye mwili wake.

Catherine aliuchukua ule mkufu na kuweza kuwahi pale alipokuwa amelala nyonga mkalia ini wake toa mfupa weka mnofu aliinama pale chini akamvalisha ule mkufu na kutoa vitu kama cheche kwenye vidole vyake alimbinya navyo Jamal kifuani na shingoni kwa nguvu zaidi ya dakika mbili akiwa anatoa machozi hakuwa na imani na alichokuwa anakifanya hapo, alitabasamu baada ya kelele ya maumivu kusikika kutoka kwa Jamal alizinduka akiwa kwenye maumivu makali mno alikuwa ametolewa kwenye hatari ila alihitajika kwenda hospitali, alimkumbatia Catherine huku wote wakiwa wanalia sana ni wazi hisia zao zilikuwa zinazungumza kwa macho yao walipendana sana na ndiyo maana mwanamke huyo alijitoa kutoka ndani ya nchi ya Cuba na kuja kwenye nchi ya Tanzania kwa ajili ya kumsaidia mumewe mtarajiwa na kweli alilifanikisha hilo.

Baada ya kuangaliana tu macho yake yalirudi kwenye hali yake ya kawaida na Jamal alikuwa amesha zipata hizo taarifa juu ya hilo hivyo hakuhitaji sana kumsumbua mwanamke huyo kumuuliza tena, alimsaidia Jamal kunyanyuka ambaye alionyesha ishara juu ya kioo kilichokuwa ukutani Catherine alikirukia na kumpatia mwanaume huyo ambaye akikipasua kwa ngumi yake kwa mara ya kwanza tangu alipokuwa na miaka 14 leo alikuwa anakipata kichwa cha baba yake mzazi mr Jonson Malisaba alikikumbatia na kulia sana hakujali damu ambazo zilikuwa zinamtoka kwenye mwili wake kulingana na namna alivyokuwa amecharangwa na visu pamoja na zile karata tatu.

Hakuwa kwenye hali nzuri ila hakuwa mwanaume mlaini kabisa, kwa msaada wa Catherine wakawa wanatoka nje huku akiwa amekishika kichwa cha baba yake kwenye kile kibox kilicho tengenezwa kwa muundo wa kioo wakati huo ilikuwa imetimu alfajiri sana na mapema, walivyotoka nje walishangaa kuna umati mkubwa wa watu, kulikuwa na wanajeshi wengi sana ambao wote walikuwa wamepiga saluti wakati komando huyo anatoka tu hapo nje, alishangaa wamejua vipi kama yuko hapo na kama haitoshi pembeni alimuona mwanamke ambaye alimpenda kuliko hata nafsi yake aliletwa na Mr Jimen pamoja na Jackie the Hunter baada ya raisi kutangaza kila kitu siku ile anayo jiuzulu aliweka uwazi kwa kusema kwamba kijana huyo hakuwa na hatia yoyote ile hivyo walimweleza ukweli wote wa maisha ya mwanaume huyo kwamba ni pacha wake wa damu kabisa na historia nzima ya maisha yao bibie aliweza kupewa, alilia sana na kutamka kwa sauti “kaka” huku akiwa anamkimbilia pacha wake huyo hata waziri mkuu alikuwepo hapo naye alikuwa amepiga saluti ya heshima kumpa pongezi komando ambaye alikuwa ameitetea nchi kuingia kwenye mikono ya watu wabaya ule mkufu alikuwa nao shingoni tena baada ya Catherine kuurudisha, dada yake alimkumbatia huku akiw analia sana, upande wa pili The SPY waweza kumwita Ismail Mwandepo alienda na kumkumbatia Catherine naye pia alikuwepo.

Mtaani watu wote ambao walihisiwa kuhusika na hayo mambo walikamatwa kampuni zote ambazo zilikuwa hazieleweki vizuri zilifungiwa swali lilibaki kwa Jamal akiwa anajiuliza ni nani aliyekuwa amefanya mpaka wakajua kwamba alikuwepo hapo. Kuna gari ilisimama karibu na hapo alishuka mr Deus akiwa kwenye pingu alienda na kumkumbatia Jamal kwa furaha hapo ndipo Jamal alipo elewa huyu ndiye aliye wafanya mpaka wakajua kwamba wapo hii sehemu alimtambulisha dada yake kwa wifi yake Catherine walikumbatiana kwa furaha sana kidogo familia iliyokuwepo iliungana tena kwa mara nyingine. Jamal alimkabidhi dada yake kichwa cha baba yao mzazi na kupiga kelele.

“Dadiiiiiiiiiiiiiiiiiiii” huku akitoka machozi kisha taratibu mwanaume akawa anashuka chini na kudondoka kabisa alitulia kimya, walianza kuhangaika sana kuweza kumpandisha kwenye gari ili wamuwahishe hospitali dada yake na mkewe mtarajiwa walikuwa kwenye majonzi mno dada yake akiwa ameshika box la kioo lenye kichwa cha baba yao leo ndiyo kwa mara ya kwanza alikuwa ametamka neno kaka alichanganyikiwa mwanaume huyo kuwa kwenye hiyo hali na aliogopa sana alipandishwa haraka sana kumuwahisha hospitalini kuona kama wanaweza kuokoa hali yake akiwa ameiacha nchi kwenye hali ya amani na usalama wa kutosha.

Naam ulikuwa nami kwenye kigongo hiki tangu naanza sehemu ya kwanza mpaka namaliza sehemu ya 100, niseme asante sana kwa kuwa na moyo wa uvumilivu pamoja na support yako ya dhati mpaka leo tupo pamoja siwezi kukulipa ila nakuombea MUNGU azidi kukupa maisha marefu zaidi upate kuzisoma hadithi zangu nyingi.

Mpaka hapa niseme sina la ziada nakusanya kila kilicho changu rasmi natoka ndani ya chumba kilichokuwa kinaitwa I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU), nimefika mwisho.

GOODBYE

Bux the story teller.

MWISHO.
 
Asanteni sana, nawashukuru wote kwa kila aliye comment, kutia like, ushauri, kukosoa na hata wale ambao walipita kimya kimya nawashukuru sana.

Shukrani zingine za dhati ziende wa wale ambao walitoa chochote kutoa support yao kubwa, nawapenda sana.

Leo nafika mwisho wa simulizi hii tukutane ndani ya simulizi zingine.

1. ULIMWENGU WA WATU WABAYA
2. I WANT TO DIE JUDGE
3. GEREZA LA HAZWA
4. INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
5. HATIMA YA UJINGA WAKE

Wasalaam

Bux the storyteller
FB_IMG_16772242584975055.jpg
 
what a story from GURU Babuya
 
Hello wanafamilia wa Story za Bux na mwandishi Febiani Babuya.

Leo nimewaletea andiko lingine fupi.

Kwa wale ambao wanapenda sana simulizi za misuko suko ya maisha pamoja na maisha halisi ya mtaani haswa, basi simulizi ya MIMI NAITWA GAMA ipo kwa ajili yenu.

Simulizi inamhusu jamaa mmoja ambaye alizaliwa kwenye maisha magumu sana tena zaidi ya sana, ukitaka kujua nini maana ya maisha magumu basi wewe lisome jina lake tu hali ambayo inampelekea kuwa muokota makopo mtaani. Ugumu wa maisha yake unamfanya kumtupia lawama zote baba yake mzazi huku akimshuhudia mama yake akifa kikatili mbele ya macho yake mawili.

Anaahaidi kumuua baba yake kwa mkono wake mwenyewe, hasira zake zinampelekea kuishia gerezani kisha kuwa muuaji baada ya kutoka huko.

Maisha ambayo aliyachagua yanamfanya kuishia kuokota makopo na kula jalalani. Mwanaume huyo anafanikiwa kuishi mwaka mmoja tu wa furaha huku mwaka huo ukiacha majonzi makubwa sana kwa familia.

Ni bonge la simulizi hii usiikose kabisa ili uyasome maisha halisi ya mtanzania wa mtaani.

Hadithi inaitwa MIMI NAITWA GAMA na nimeiandika yote mpaka mwisho ila hii haitapatikana huku Facebook,instagram au Jf mpaka ulipie ndo utaweza kusioma.

Unaipata kwa shilingi 1500 tu, yaani elfu moja na miatano tu pekee, yote.

Lipia kupitia namba

0621567672
0745982347

Jina FEBIANI BABUYA

ILI UIFURAHIE WIKIENDI YAKO KWA KUYASOMA MAISHA YA MTANZANIA HALISI WA MTAANI HASWA.

Wasalaam.
Screenshot_20230528-070958_WhatsAppBusiness.jpg
Screenshot_20230528-070933_WPS%20Office.jpg
 
Habarini ndugu zangu? Hope mko poa.

Jambo jema ni kwamba mwezi wa 9 tutakuwa na hardcopy/ nakala ngumu ya kitabu cha GEREZA LA HAZWA.

NITATOA TAARIFA MAPEMA KABISA.

Nawatakieni asubuhi njema.
FB_IMG_1693195898337.jpg

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SAKATA LA UCHAGUZI-PESA KWENYE DAMU (ELECTION SAGA-MONEY IN BLOOD)
INTRO...
Miaka mingi sana iliyokuwa imepita ikiwa ni miaka miwili kabla ya uchaguzi, serikali ya nchi ya Tanzania ilipokea taarifa mbaya kutoka kwa magaidi nchini Kongo kwamba raia wa Tanzania waishio huko wametekwa na ili kuwaachia serikali ilitakiwa kupeleka madini ya kutosha.

Sababu hiyo inamuibua waziri wa ulinzi ambaye anagoma kuhusu kupeleka madini hayo, ndipo anakutana na mkuu wa majeshi na wanakubaliana kukituma kikosi cha makomando SITA ambacho kiliitwa 6.0 (SIX POINT ZERO (hiyo zero iliwekwa kwa sababu maalumu, mwanzo ilikuwa ni 7.0). Makomando hao wanafika Kongo na kufanikiwa kuwaokoa mateka wote, wakawapandisha kwenye ndege huku wao wakiwa karibu na ziwa Tanganyika kusubiri usafiri kwani walikuwa wanafuatwa kupewa msaada ili kutoweka haraka kabla hawajashtukiwa.

Lakini huko Kongo kuna mizigo ambayo waliiokoa pamoja na mateka bila kujua ni mizigo ipi, baadae walikuja kugundua kwamba ni madini.Wakiwa wanajiuliza inakuwaje wanarudi na madini tena? Ndipo wanashangazwa na kinacho tokea.

Ndege ya raia wa Tanzania inatunguliwa ikiwa angani na kulipuka yote.....makomando hao wanashangazwa sana na hilo tukio na ndipo wanashtuka kwamba huenda huko walitumwa kufanya oparesheni nyingine na sio kuokoa watu, hapo wanayakumbuka madini ambayo walisisitizwa warudi nayo na kupewa onyo kwamba wasije wakaangalia ni mzigo gani. Wakiwa kwenye mshangao wa raia wao kulipuliwa wote ndipo msaada ambao ulikuwa umewafuata unafika walipo.

Wanaume ambao waliwafuata hapo hawakuwa kwa ajili ya kuwachukua bali kuwaua. Makomando hao wanakuja kushtuka ikiwa ni TOO LATE hivyo wanapigwa risasi vibaya sana miili yao ikibaki inaelea ziwani tu. Wauaji baada ya kuhakikiki kwamba wamemaliza kazi wanayabeba madini na kutoweka kuyapeleka kwa waheshimiwa walio toa amri ya kazi. Waheshimiwa wanatoa taarifa kwamba MAKOMANDO wamelidhalilisha taifa kwani badala ya kuokoa watu wao wameenda kuua raia wote wa Tanzania kisha wametoroka na madini hivyo wanatakiwa kusakwa popote pale duniani (WANAUME WANAUZIWA MSALA)

Kwa bahati mbaya sana mtoto mmoja wa kishua alikuwa ndani ya nchi ya Kongo kufanya utalii.....anafanikiwa kuuona mwili wa mtu ukielea majini hivyo akatoa amri walinzi wake wautoe na ndipo anagundua kwamba mtu huyo kwa mbali bado anahema, anaamua kuondoka naye na kwenda kwao UGIRIKI na mwili wa huyo komando mmoja ambaye anaitumia miaka miwili kitandani na baada ya kuja kuamka MATATIZO YANAANZIA HAPA. Wakubwa wakijua waliua wote lakini kwa bahati mbaya kuna kiumbe kiliishi. UMWAGAJI WA DAMU NDANI YA TAIFA LA TANZANIA UNAANZIA HAPA bila kujali kwamba ni damu za wenye hatia au wasio na hatia, nchi inachafuka na kuna mambo mabaya sana yanakuja kutokea. Hapa ndipo tunaanza kuzifunua kurasa hizi rasmi;

Baada ya miaka kumi na miwili kupita, Tanzania inapitia kwenye kipindi cha uchaguzi ambapo vigogo watatu wanaanza kuiwania nafasi hiyo kwa udi na Uvumba, wa kwanza alikuwa ni raisi mwenyewe (Huyu hakuna mtu aliyekuwa anamjua sura yake hata wananchi ambao alikuwa anawaongoza) utakuwa unajiuliza inakuwaje raisi aliye ongoza miaka 10 wananchi hawamjui?[emoji848]RELAX, wa pili alikuwa ni wa chama kimoja na raisi ambaye alitaka kumchallenge bosi wake na kutaka atoke Ikulu kwa lazima (huyu alikuja kususiwa IKULU, na alipokuja kugundua sababu ya kususiwa IKULU! Alikuwa amechelewa (TOO LATE).

Wa tatu alikuwa ndiye kipenzi cha Watanzania...huyu wananchi wote walihitaji aingie IKULU kwani walimpenda sana lakini siku chache kabla ya uchaguzi huyu anaye pendwa sana, mwanae mdogo anatekwa. Akiwa amepaniki asubuhi anapatiwa maiti ya mwanae ikiwa haina kichwa. ANACHANGANYIKIWA sana ila kabla hajapoa vizuri jioni mwanae mkubwa wa kike naye anapotea kwenye mazingira ya kutatanisha, anapagawa na kuamua kuibeba bastola yake kisha akaondoka nyumbani.

Alihitaji kwenda kuwabana wapinzani wake kwa kuhisi kwamba ndio ambao walihusika lakini aliishia kupigwa risasi nyingi sana na kupata koma na hapo ndipo simu inapigwa mpaka kwenye ardhi ya MALIKIA. Huko alikuwa anasoma mtoto wa kiume wa mzee huyo, lengo la kumpigia ilikuwa ni kumpa taarifa na kumtaka awe karibu na familia asije kuuawa.

Lakini kurudi kwake kunaibua mambo ya kutisha nchini, alidaiwa kuwa moja kati ya watu hatari sana na alikuwa na makubaliano ya kifo na shirika la kijasusi la MI6 Kwa siri sana ambapo alidaiwa kuhusika kukitengeneza kirusi kimoja hatari sana ambacho kiliishia kwenye mikono ya magaidi ikiwa ni siri ambayo aliishi nayo yeye tu maana familia ilimjua kama mtoto wa mama na hata vyombo vya usalama hivyo ujio wake unakuwa mwanzo mpya wa Tanzania nyingine ya kutisha kwa siri sana.

Unataka kujua kwamba kuna nini humu ndani? Basi ungana nami kwenye andiko hili la SAKATA LA UCHAGUZI-PESA KWENYE DAMU.

Simulizi hii ipo yote mpaka mwisho na unaweza kuipata kwa mfumo wa softcopy kwa bei ya shilingi 5000 tu za kitanzania.

5000 yako tu unapata burudani kubwa sana ya kusoma andiko bora sana hili la kipelelezi likiwa limejikita zaidi kwenye kuichambua SIASA na mambo yake ambayo yapo ndani.

Unaweza kufanya malipo kwa namba hizi.

0621567672
0745982347

Zote jina FEBIANI BABUYA.

Kwenye kalamu ni mimi FEBIANI BABUYA.

Chao

5cd1902acb2b45298e1a59afea1a415c.jpg

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
JIJI LA KAMALI ( GAMBLING CITY)

INTRO...........
Usiku wa kiza kinene ambacho kilikuwa kinasindikizwa na mvua ambazo hazikuwa na mpaka wa kuweza kuzielezea vyema, alionekana mwanaume mmoja akiwa ndani ya nguo zake nyeusi tii na begi jeusi usiku huo huku mwili wake ukiwa umefunikwa na koti kubwa jeusi pia ambalo lilikuwa refu kiasi kwamba lilivuka mpaka magotini.

Mikono yake ilifunikwa na gloves nzito nyeusi pia ambapo mkono wake wa kulia ndio ambao alikuwa ameutumia kuweza kushika begi lake mkononi akiwa anatembea kwa mwendo wa haraka sana huku akiwa makini mno kuonyesha wazi kwamba alikuwa anatakiwa kulifikisha begi hilo salama kabisa sehemu ambapo lilikuwa linahitajika kuweza kufika.

Akiwa kwenye mwendo wake huo wa haraka, wakati amefika katikati ya barabara ndogo ambayo ilikuwa imezungukwa na majengo marefu sana na pembeni yake kukiwa na vichochoro vingi, alihisi kwamba eneo hilo ni kama lilikuwa na mtu au watu wengine ukiacha yeye hivyo alizidisha hali ya umakini sana kwa hapo ambapo alikuwa amesimama.

Masikio yake yalimtekenya vizuri mithili ya funguo zinapokuwa zinazamishwa kwenye kufuli na kumpa taarifa hiyo, alikuwa ni mtu wa kuutumia sana mlango wake wa sita wa fahamu huo wa hisia hivyo alikuwa na uhakika kwamba hisia zake zisingeweza kumsaliti kamwe kwani alikuwa akijiamini sana kwenye jambo hilo hivyo akawa na uhakika kwamba kulikuwa na ugeni ndani ya hilo eneo.

Alisimama na kutulia ili kuweza kujua kwamba huyo mgeni alikuwa anatokea upande upi huku akiwa ameyafumba macho yake kuweza kujipa hali ya utulivu zaidi kwenye masikio yake. Akiwa bado amesimama hapo alihisi kama kuna kitu kilikuwa kinakuja kwa kasi sana sehemu ambayo alikuwa amesimama hivyo aliinama kwa kasi mno mithili ya radi ya mvua.

Wakati anainama alipishana na shoka ambalo lilienda kukita kwenye ukuta mmoja wa jengo la pembeni. Aligeuka haraka sana ila wakati anageuka alitumia muda mrefu ambao ulimpa nafasi mtu ambaye alikuwa ameingia hapo kufanya kile ambacho alikuwa anakitaka.

Alihisi kifua kinamuwasha mithili ya mtu aliye tafuna pilipili kichaa maana spidi ambayo mvamizi aliitumia kumkita hapo kifuani haikuwa ya binadamu mwenye mifupa ya kawaida bali alikuwa ni mashine haswa kama namna umeme unavyo safari kwenye zile njia zake. Alipokea mishindo ya haraka na mabuti makali na kumfanya begi kumtoka mkononi huku ikionekana wazi kwamba mabuti hayo yalitokea kwa mtu ambaye alidhamiria kabisa kumuua ndiyo maana hakumpa hata nafasi ya kuweza kumtazama maana mvamizi huyo uso wake ulifunikwa kwa kitambaa cheusi na hata mvamiwaji hakupata hiyo nafasi ya kumtazama kwa ukaribu.

Mwanaume huyo licha ya kurushwa mbali na mabuti hayo hali ambayo ingemfanya auvunje mgongo wake kwa kujibamiza kwenye kuta za mawe mazito za majengo ambayo yalikuwa pembeni, hakuwa fala kufa kijinga namna hiyo. Mkono wake ndio ambao aliutumia kukita kwenye kuta hizo na sio mgongo ambao ulitua ukutani kwa nguvu sana.

Kasi ambayo alitua nayo kwa mkono wake ililifanya koti lake kujivuta kidogo na kwenye mkono wake ikaonekana alama ya tatoo (tatuu) ambayo ilisomeka kama 001. Baada ya kujichomoa hapo ndipo aligeuka na kumuangalia mtu ambaye alionekana alihitaji kumuua, mtu huyo alikuwa kwenye mavazi meusi kama yeye na koti kama lake, yaani kiufupi wote walikuwa wamevaa sawa ila utofauti wao ni kwamba mvamiwaji alivaa kofia aina ya pama kichwani ila mvamiaji alikuwa amejifunika tu kitambaa kwenye uso wake hivyo sura yake haikuwa ikionekana kabisa.

Baada ya hapo ulipigwa mkono wa hatari mno mpaka umeme ulipo katika ghafla sana ndipo mvamiwaji alitulia akiwa makini sana maana hakuwa akimuona mtu ambaye alitakiwa kumshambulia huku akiwa amepigwa vibaya sana na umeme huo kukatika alishukuru sana japo ilikuwa ni hatari maana angeweza kuuawa bila kujua mhusika yuko wapi ila aliamini kwamba angepata dakika chache za kupumzika maana bila hivyo ni lazima angekufa.

Akiwa anaangaza kwa umakini huku na huko umeme ulirudi tena ghafla sana na ndipo alipo gundua kwamba ndani ya eneo hilo hapakuwa na mtu mwingine zaidi yake, mvamizi alikuwa ameondoka muda mrefu sana ila chini palikuwa na karatasi nyeupe ambayo ilikuwa imesainiwa kwa damu huku ikiendelea kunyeshewa na mvua.

Aligeuka na kuangalia pale ambapo begi lilikuwa limedondokea ili kujua usalama wake ila kwa bahati mbaya sana begi halikuwepo kabisa eneo hilo, alishtuka sana akionyesha hofu ya wazi moyoni na kwenye uso wake hivyo hakuwa na namna zaidi ya kuisogelea ile karatasi ili aweze kusoma kile ambacho kilikuwa kimeandikwa.

“KAMALI YANGU YA MWISHO, NDIYO KAMALI YAKO YA KWANZA” hayo ndiyo maneno ambayo yalikuwa yameandikwa hapo. Aliogopa sana baada ya kuisoma huku akionekana wazi kwamba mikono yake ilikuwa inatetemeka wakati huo. Hiyo ilikuwa ni kauli ambayo alikuwa anaitumia mwanaume mmoja ambaye alimuua yeye mwenyewe kwa mkono wake miaka kadhaa ambayo ilikuwa imepita huko nyuma, huku begi ambalo lilionekana kuwa na nyaraka mhimu mno likiwa limepotea kizembe sana.

Inawezekanaje mwanaume ambaye alimuua kwa mkono wake mwenyewe bado awe hai? Hilo begi lina nini mpaka mtu ambaye alisemekana kwamba alikufa aweze kupotea nalo? Nini maana halisi ya JIJI LA KAMALI na jiji hilo lina mambo yapi na siri zipi labda?

Unategemea kukutana na nini humu ndani? Mimi nashika kalamu yangu sasa nakaa mezani, kazi yako wewe ni kuhakikisha unaenda nayo nukta kwa nukta ili uweze kuifunua kila kurasa kuweza kuzisoma serikali tatu kwa wakati mmoja ndani ya JIJI LA KAMALI.

Simulizi hii inasomwa kwenye group la WhatsApp tu pekee na haitapostiwa mahali pengine popote hivyo nicheki haraka nikuunge kwenye group langu la WhatsApp uanze kusoma simulizi hatari sana ya watu wenye jiji lao la KAMALI (ni hatari sana).

Kujiunga bei yake ni shilingi 3000 tu, yaani ukilipia 3000 nakuunga kwenye group haraka sana.

Usikae kinyonge wakati naingia kujifungia ili ufurahi na kwenda kuisherehekea vyema likizo yako ndefu. Maandishi yapo yanakusubiri wewe tu, usijibane ukataka kukosa simulizi hii bora ya kusisimua eti kisa 3000 tu.

Lipia kupitia namba

0621567672 ( WhatsApp)

0745982347

Zote FEBIANI BABUYA

Nataka watu 30 tu wa mwanzo nianze nao haraka sana, unaweza kuwahi kabla nafasi hazijajaa ili usije ukaikosa[emoji996]

Niwatakieni asubuhi njema.

Kalamu ni yangu mwenyewe;

FEBIANI BABUYA.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)-Simulizi mpya na bora sana ya kipelelezi/kijasusi imetoka rasmi kwa mfumo wa softcopy (nakala laini)

Hii ni moja kati ya movie bora sana iliyopo kwenye maandishi ambayo utaisoma mwaka huu....Kuna mwanaume alipigwa zaidi ya risasi sita kwenye mwili wake kisha akaenda kuzikwa akiwa hai.......Alizikwa porini ambako hakukuwa na binadamu yeyote yule anayeishi LAKINI cha kushangaza mwanaume huyo alikutwa anaishi na yupo hai miaka kumi na mbili iliyo fuatia baadae.....Walichanganyikiwa na ndipo alitumwa BEAST mmoja kwenda kumtafuta ili kujua mtu aliyezikwa anakutwa vipi mtaani! Ni bonge moja la simulizi[emoji119][emoji119][emoji119] NICHEKI UJIPATIE NAKALA YAKO LAINI uendelee kufurahi..... [emoji996][emoji91]

Softcopy yake inapatikana kwa shilingi 5000 tu.

Nicheki WhatsApp kwa namba 0621567672 uweze kuipata yako.

Kama unalipia namba za malipo ni hizi hapa[emoji116]

0621567672

0745982347

FEBIANI BABUYA.

Karibu tuyafurahie maandishi, ndipo chanzo kikubwa cha akili na maarifa kilipo jificha[emoji996].
FB_IMG_1701864748679.jpg

Back
Top Bottom