Iangaliwe namna bora ya kuwanusuru watoto na madhara ya kitabia migodini

Iangaliwe namna bora ya kuwanusuru watoto na madhara ya kitabia migodini

Trainee

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
2,660
Reaction score
3,501
Hivi mbona swali hili sijawahi kupata majibu yaliyonyooka?

Ni kwa nini watu hawa wanatukana sana katika baadhi ya mazingira yao ya kazi?
TANESCO (WAKIWA SITE)
WANAJESHI (KWENYE OPERATION NA MAZOEZINI)
WATU WA MADINI (MACHIMBONI)
WAJENZI (WANAPOKUWA SITE)
Na kadhalika na kadhalika, kiufupi kazi nyingi za kutumia nguvu za misuli ya mwili zinapokuwa zinahusisha kikundi cha watu basi matusi ni nyumbani mwake! Je ni lazima? Kwa nini?

Pia nimeuliza mara kadhaa bila kupata majibu kwamba je haiwezekani kuweka sheria na kanuni kali kuzuia haya mambo ya kutukana ovyo? Tufanye haiwezekani basi maana imekuwa hao ni watu wazima wanajiongoza kwa hiyo as long as hawagombani imekuwa ni sehemu ya lugha yao basi nawaendelee! Haya vipi kuhusu watoto ambao wanakulia katika mazingira hayo? Nao tuwaache? Hapana!

Leo nitajikita zaidi kwa watu wa migodini sitagusia hao wengine maana wengi wao kazi zao hazichanganyiki na watoto. Nitatoa mifano miwili tu katika watoto kadhaa niliowaona ili muone matendo ya ovyo na haya matusi yana athari gani kwa watoto wetu wadogo

Wamama katika harakati za kujitafutia wanakwenda kupiga kambi migodini wanakuwa wanafanya biashara ndogondogo hususani vyakula. Wengine wana vitoto vidogo ambavyo vinawasaidia shughuli ndogondogo mama zao (hasa kipindi cha likizo) huko migodini au hata kama siyo kusaidia kazi lakini kuna vitoto vingine hakuna budi kuwa na mama zao huko kutokana na udogo wao

Kuna mtoto nimempokea hapa shuleni (mimi ni mwalimu) naambiwa kimekulia huko machimboni. Huyo mtoto kuanzia ongea yake, cheza yake, angalia yake, tembea yake, kula yake na kila kitu ni mtihani tupu. Sina sababu ya kuandika mitusi yake humu lakini kiufupi ni kwamba kila anachofanya hawaendani na wenzake na kama unavyojua vitoto vya awali kwa kushitaki, kila muda kanashitakiwa kametukana, kamepiga, nk. Uzuri ni kwamba shule kila kitu kinawezekana, kanabadilika ghafla sana mpaka kwao wanashangaa

Siku moja jamaa mmoja tulikaa kwenye kioski chake (kijiweni) kukaja mshikaji mwingine ana katoto kake (nadhani walikuwa ndugu huyu mwenye kikosi na mwenye mtoto) basi kukapita muuza supu ya ndoo dogo akamkomandi baba yake anunue supu "baba nunua supu hiyo mimi nataka supu" baba akajibu saivi sina hela ebwana wee katoto kaliporomosha mitusi hiyo "wewe #$$# nini hebu nunua supu mimi ninywe usinizingue" huku kanamvuta nguo kumdrag kwenye ndoo ya supu. Jamaa anaulizwa anasema huyu mtoto alikuwa machimboni na mama yake huko sasa ni mtihani sana nimekuja nae hata bibi yake kashindwa kukaa nae ndiyo maana natembea nae mimi muda wote. Ni kadogo sana kiasi kwamba kanapakatwa wakati wa mazungumzo lakini hapo mdomoni sasa...

Imagine siku hizi kila kijiji tunaambiwa kumevumbuliwa madini na uchimbaji wake ni huu huu wa kienyeji ambapo watu wa hali ya chini wanakimbilia humo kama sehemu muhimu ya kujiingizia riziki sasa kitabia tutakuwa na kizazi cha aina gani.

Nyinyi mmekubuhu sawa na wengine mnajitahidi matusi yanaishia hukohuko site mkifika nyumbani/uraiani hamtukani kabisa sawa lakini vipi na hawa watoto je?
 
Naona umewasahau wavuvi

Hao kipindi wanavuta mitumbwi kutoka majini ili ifanyiwe ukarabati ni matusi kama yote na anayetukanwa ni Tajiri yao😂😂
 
Madereva wa Malori,

Hawa wakiwa parking zao hasa zinakua shell, na hapo kuna wamama wakiwa na watoto wao wadogo wakifanya biashara.

Jamani wana matusi hawa watu, tena makubwa makubwa, hadi unajiuliza wako timamu? Wanakera hatarii.
 
Back
Top Bottom