Plaintiff
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 307
- 216
Kwanza kabisa naomba msingi wa uzi huu uwe kwenye ukristo, maana tukiongea kwa misingi ya madhehebu yetu hatutafika lengo letu.
Karne ya kwanza ya 1, 2, 3 watu walipumzika na kuabudu siku ya Jumamosi mwanzoni mwa Karne ya nne watu fulani waliamua kubadili siku hii na kuhamia Jumapili. Je tunafuata maagizo ya wanadamu wenzetu au tunafuata Maagizo ya Mungu?
Kila aliyeuona uzi huu ninaamini ana access ya mtandao, unaweza kugoogle ibada ya jumapili imeanzishwa lini na mwanzilishi ni nani.
Tangu kuumbwa kwa dunia Mungu alishaweka wazi kwamba Sabato ni siku takatifu na aliitakasa. Na katika amri zote za Mungu hii ndio amri imeandikwa kwa maelezo marefu.
Pia wakati Musa yupo kule mlimani zile siku 40 Mungu alimgusia pia kuhusu sabato na akamuambia ni agano lake la milele.
Pia hata katika agano jipya bado watu waliendelea kuabudu siku ya sabato kuanzia Yesu mwenyewe mpaka mitume baada ya Yesu.
Mfano Luka 4:16 "Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome"
Luka 4:16 imeweka wazi kwamba ilikuwa ni desturi ya Yesu kuingia katika Sinagogi siku ya ya Sabato.
Mafungu ya sabato ni mengi na siwezi kuyaweka yote hapa, ila nataka kujibu hoja za baadhi ya watu kuhusu ibada ya J2.
1. Ibada ya J2 kama kusheherekea ufufuko wa Kristo.
Hili la kusheherekea ufufuko wa Kristo na kubadili mpaka siku aliyoweka Mungu kama siku ya ibada limeanza lini? Kwenye biblia limeandikwa wapi? Kwanini katika historia watu wameanza kutekeleza hili katika karne ya 4?
2. Yesu ndio Bwana wa Sabato, hivyo tukimfuata Yesu sabato haina haja.
Yeye mwenyewe ambaye alijiita kuwa ni Bwana wa Sabato alizishika Sabato, nimetoa mfano kwenye Luka 4:16. Lakini pia kwenye mathayo 5:18 akasema "Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie." Kwa maana hii sheria ya Mungu haibadiliki.
Na fungu la 5:19 akaonya juu ya wanaozivunja amri hizo "Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni."
3. Siku zote ni za Mungu,
Hakuna mtu aliyekukataza kuabudu siku yoyote, ila sabato ni siku ya kuacha kazi zako zote unazozifanya siku zile 6 za week na kupumzika na kuwa karibu na Mungu wako. Hata sisi wengine tunakuwa na ibada zetu kama kawaida siku zote za week ila sabato ya Bwana lazima tuitunze.
Swali langu kuu bado linabakia pale pale kwa wachangiaji wote.
Je, ni kwanini ibada ya J2 ianze karne ya nne baada ya watu kukaa na kuamua watu wapumzike na kuabudi jumapili? Je tunamfuata Mungu au tunawafuata Binadamu wenzetu kwa sababu tu wameamua mambo ambayo tumeyaona ni mema machoni petu?
Mungu atusaidie sana, Muwe na Sabato Njema.