EvilSpirit
JF-Expert Member
- Jun 15, 2017
- 10,576
- 16,644
Wasaato tutaanza kuwachapa viboko sasa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaposema jumamosi- MojaHayo ni maagano ya Mungu kwa wayahudi kwenye agano la kale ambapo walikuwa na siku iitwayo sabato na sina uhakika kama ni hiyo Jumamosi unayoongelea hapo.
Vipi kuhusu agano jipya? Binafsi naamini Ijumaa ndio siku ya mwisho ya wiki.
Jumamosi - moja
Jumapili - mbili
Jumatatu - tatu
.
.
Kwa mtiririko huo. Ijumaa ndio siku ya saba ya wiki.
Pia kama kweli wewe ni mfuasi wa hizi imani ambazo tumeletewa na wazungu (ukristo) na waarabu (uislamu) nadhani kuna mambo ya msingi na muhimu zaidi ya kuzingatia katika kuishi maisha yenye kufuata misingi ya hizo dini lakini suala la siku gani ya kuabudu sio la msingi.
Ukienda nchi zenye mlengo wa dini ya kiislamu hata makanisa huwa yanaabudu na kufanya misa Ijumaa. Mfano Algeria
SI kweli Mungu hajawahi kuamrisha watu kusali Jumamosi, zile kanuni zilitungwa na watu na wala si Mungu. Ondoa huu ujinga kichwani mwako. Mungu hana dini na hawajawahi kutunga seria yeyote ya dini. Ndiyo maana mnaambiwa religion makes people stupid, thiis is it.Mungu aliagiza tuabudu siku ya kwanza ya juma ambayo ni jumamosi, hebu nenda kanisani muulize kiongozi wako wa dini, sabato ni juma ngapi?
Nimekuelewa sanaaaaNTAANDIKA KWA WINGI PENGINE KUTOKANA NA UZITO WA HOJA YANGU NA HUMU KUNA BAADHI YA UKWELI KWA UNACHOKIAMINI MAANA SIWEZI KUANDIKA VYOTE...
Naomba usome comments hii Ndugu yangu Najua italeta confusion kwako lakini ndo ukweli wenyewe ( Na japo utakuwa mchungu Lakini inabidi uukubali kwakuwa huna namna)
Kwanza naomba kudeclare kwamba nilikuwa SDA kama wewe Tena nikishika siku Takatifu Very strict na Kwa bahati nzuri nilipita katika njia zote salama ( Na kipindi hicho tulikuwa ni lazma upitie Mafunzo yote kutoka Adventurer mpaka master Guide kama unataka kutambilika kanisani na kupata uongozi angalau Hata wa Shule sabato ..Kwahyo ilikubidi uwe umepita MasterGuide na umesoma na kuweza kufanya refference angalau ya Roho ya unabii (Ellen G white) si chini ya vitabu 10 na kuendelea...Na nilifanikiwa kuwa miongoni mwao...
Natamani niandike vyote lakini Shortly Niliwahi kupita pale Arusha na kufanikiwa Kusoma Theology (Pastoral version Nazungmzia) kwahyo nilikuwa "kipastor" kijana nisiye na mtaa wala kuwekewa mikono (sikuwekewa mikono kwa kuwa kanuni kipind hicho haikuruhusu Pastor ambaye hajaoa kuwekewa mikono mpaka atakapo oa!...
Ok Sasa tuachane na Huko kwani hiyo ni Hadithi ndefu sana on how i became to be Like this (hivi nilivyo sasa),
kwa sababu niliwahi kuwa muslim na kusoma pia huko na nahisi kwa sasa ni bora kubaki nilivyo...
SO NIRUDI KWENYE MADA KUU ULIYOILETA
So actually bado Elimu yako kibiblia sio kubwa sana kuweza kujenga hoja na kupangua Hoja pinzani kuhusu Hoja hiyo uliyoileta japo umejaribu (Kwa sababu nimeona jinsi unavyojibu hoja za wapinzani)
kuna hoja nyingi Kama za mtume Paulo kuhusu Siku na miandamo ya mwezi hujaweza kuzijibu ipasavyo...
na kuna mmoja akatoa hoja kuhusu Mabadiliko ya Siku katika enzi mbalimbali nahisi ulimjibu kwa Mafungu ya Luka (Kuhusu maandalio mpaka ufufuo) umejibu vyema kwa imani yako..Japo bado kuna Mapungufu pia..
kuwa kuna Enzi (Era) nyingi kuna milele nyingi imepita (Najua unajua kuwa kuna milele zilizopita na milele zijazo) katika enzi hizo nani ajuaye kuwa Siku ziliwahi kubadilika? kuna mtu aliuliza swali Hili ila sijaona ukijibu...
SASA NIENDE KWENYE HOJA YANGU..
Warumi sio watu wajinga kama wengi mnavyodhani au mnavyowachukulia...
kama waliweza kufuta historia baadhi ya dunia, wewe unawaonaje walishindwa kufuta ulichofikiria?
halikuwa taifa lenye Nguvu tu pia lenye siri nyingi sana pengine kuliko taifa lolote duniani...
Wakati ule wa Religious and Political Revolution (Reformation) Ambao ndo unasifiwa kuwa wakati bora kwa makanisa ya kiprotestant na wasabato ndo ulikuwa wakati mbaya sana kihistoria na kidini japo bado watu wengi hawajui.. (The Time of prostestantic Reformation ilikuwa ni muda wa majonzi yaliyojificha)
Kipindi kina john wycliffe ,John huss, Martine luther na wengine wengi kama kina smith wanaanza harakari za kukomboa Kanisa yaani Church reformation from Evil hiki ndo kpindi ambacho Roman walifanya Reformation kubwa kidini na kipolitical..
najua hili litakuwa jipya ila nifatilie ...
Martine luther kama baba wa reformation hasa kwa Wasabato na anaaminika hivyo (Kasome The great controverse au Pambano kuu ...Ellen G White) sasa Martine luther alipoaza Harakati miaka ya 1517 ndo alitikisa Kanisa kuliko wote...
sasa roman wakakuna kichwa wakapata cha kufanya ni kubadiki majira na Time Sasa walibadili vipi endelea kusoma usichoke utajua ...
Sasa bila speculation Mama yangu Ellen G white pamoja na mme wake Mchungaji James white wao hawakufanya speculation wakajua hasa Sabato ni lini kulingana na tarehe ili waweze kuiabudu kulinganana muda uliobadilishwa..
HAPA nataka kuzungumzia nini Hasa?
Kutokana na Reformation kuzidi na kanisa kuanza kuzidiwa Ndipo papa Gregory XIII aliazimia kubadli majira nazungumzia kalenda na nyakati, Rasmi Mwaka 1582 alibadilisha kalenda kutoka julian kalenda kwenda gregorian kalenda..
Kama sio mchunguzi unaweza ukaona haikuwa na utofauti wowote katika siku eeh ?
Sasa endelea kunifatilia..
Kama nilivyosema mwanzoni kuwa katika watu wenye akili sana Roman wanaongoza na katika kubadili siku walicheza na akili za watu wote duniani..
kwanza akasema anapunguza ukubwa wa siku za mwaka kutokana na kuwa ni mkubwa sana kwahyo alipunguza siku z mwaka kutoka 365.25 za juliani na kuwa 365.2425 za gregory..
kalenda Rasmi ilitangazwa Tarehe 04 october 1582, siku ya alhamisi (Thursday) na ikatangazwa kwamba kalenda hiyo itaskip siku kumi ili kuifanya iwe na mabadiliko Muhimu waliotangaza hivyo kesho siku ya ijumaa itakuwa Tarehe 15 October 1582...
sasa ili wayahudi Waliokuwepo wasipinge kalenda hiyo Wakatangaza kwamba siku zitabaki sawa na kesho itakuwa ijumaa kama kawaida kwahiyo kesho yake ilikuwa Tarehe 15 october 1582 , siku ya ijumaa...
Unaweza ukaona its ok kwa haraka haraka eeh?
Lakini ukifikiri vizuri utajua ni mchezo..
Leo Tarehe 04 October, 1582, siku ya Alhamisi Umebadili kalenda halafu unatuambia ili siku ziwe sawa inabidi uskip siku 10 mbele ili kutoa mabadiliko ya Julian to gregorian na kesho iwe siku hiyo ya kumi lakini isibadilishwe siku ila iwe siku ya ijumaa Tarehe 15 October 1582, bado watu wanashangilia bila kujua wamepigwa bao
Na hapo ndipo papa huyo alipowatandika watu fimbo bila ya kujua alibadilisha Siku na majira bila wao kujua kama kabadilisha...
Hiyo mimi huwa napenda kuiita Day sight illusion kutokana na wao kutoona kilichofanyika hapo...
Sasa naomba tuangalia kitu hapa chini..
Tarehe ambavyo zingeendelea kuwa kama zisingebadilishwa Yaani kuskip siku Kumi mbele kutoka Tarehe 04 na Tarehe 05 ikawa tarehe Tarehe 15 October 1582 kama ingeendelea bila kuskip ingekuwa hivi...
- October 6, 1582: Saturday
- October 7, 1582: Sunday
- October 8, 1582: Monday
- October 9, 1582: Tuesday
- October 10, 1582: Wednesday
- October 11, 1582: Thursday
- October 12, 1582: Friday
- October 13, 1582: Saturday
- October 14, 1582: Sunday
- October 15, 1582: Monday
- October 16, 1582: Tuesday
- October 17, 1582: Wednesday
- October 18, 1582: Thursday
- October 19, 1582: Friday
- October 20, 1582: Saturday
Sasa umeona Tarehe 15 iliyopangwa kuwa ijumaa ni actually Jumatatu kwa hiyo jamaa alichange Jumatau kuwa ijumaa...
hiyo inakupa Picha gani?
Unajua matokeo yake?
Hata hiyo Jumamosi unayojitambia its actually not jumamosi ile walioabudu mitume kama ulivyotaja....
lets see jumamosi ya juzi tarehe 4 ilikuwa ni lini kama asingebadilisha..
November 4 Ni siku ya Jumapili..Kwa c
Kalenda kama isingebadilishwaa...
Yaani 04,November 2023 before skiping 10 days of gregory ni Siku ya Jumapili while ulienda kanisani ukiamini ni siku hiyo ni Jumamosi....
Na tarehe 3 ndo ilikuwa Saturday ya kweli..
Na nimeona umesema wewe ni mtu wa kugoogle so nakupa homework nenda kafanye reseaech zako zozote...
hata kama.utaweza unaweza tumia google uwezavyo...
Angalia uhalisia kuhusu nilichosema
Dan 7:25 SUV
Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.
CC:- Plaintiff Mega Mind Nyerere
Kabla ya Julian calender inasemekana kulikuwa na lunar calender, tafiti kuhusu hii na ndio iliyokuwa inatumika enzi za agano la kale mpaka jipya, Yaan siku zilikuwa determined signs of heavens/MweziOk Sawa japo nimeshalielezea ngoja ntakuelezea kitu ili unielewe zaidi...
Ngoja nitumie mfano hai kukuelekeza...
Lets say leo kasema kuwa Atabadilisha siku na keo ni 07/11/2023...siku ya Jumanne
Na akasema kesho iwe tarehe 17/11/2023
Ikumbukwe kwamba tarehe 17 ingekuwa Ijumaa kama isingesogezwa kesho..
Kwa hiyo alipoisogeza akaifanya kuwa Jumatano..
Kwahyo hiyo skipping days ikachange siky ya Ijumaaa kuwa junatano..
Its seems kuonekana sawa but hiyo sio sawa..
Kwa mfano sikukuu ya christmass ilikuwa tarehe 25/12/2023 siku ya jumatatu unafikiri itakuwa siku ya jumangapi baada ya hiyo displacement?
Huko ndo kubadili majira kusikoumiza wala kujulisha..
Kuna huwa ni magumu Mpaka utumie ufahamu mkubwa na ndo maana biblia kuna wakati inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa...
Na kuna wakati kwenye ile 666 biblia haisemi kila mtu atajua kuhusu hiyo kitu ila inasema...
"Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na ufahamu na ahesabu tarakimu za huyo mnyama, kwa maana ni tarakimu za kibinadamu. Tarakimu zake ni 666."
Anasema hapo ndipo penye hekima kwa lugha nyingine penye ujuzi na yeye aliye mwenye ujuzi..
Maana si rahisi kutambua vitu baadhi kutoka kwa mwovu
Julian ilianza kutumika Mwaka 45 BC au 783 AUC kabla ya hapo hakukuwa na kalendar Rasmi ya Pamoja kila mmoja alitumia calendar yake kulingana na matukio na sehemu aliopo and yes Wengi walitumia Lunar Calendar na sio zaman mpaka sasa China,Jews,Islam ,Hinduism na sehemu nyingine nyingi wanatumia Lunar calendar.....Kabla ya Julian calender inasemekana kulikuwa na lunar calender, tafiti kuhusu hii na ndio iliyokuwa inatumika enzi za agano la kale mpaka jipya, Yaan siku zilikuwa determined signs of heavens/Mwezi