Ibambangulu, nabii mtenda miujiza aliyetabiri kuzaliwa kwa Mwl Nyerere

Huo uwezo ulikuwa wa kawaida sana kama kifo chake kilisababishwa tu Na Kuku.Hivi Kuku tu asababishe mtu kwenye uwezo wa pekee age? Hebu leta ufafanuzi zaidi.



QUOTE="Michael Chairman, post: 19169503, member: 284116"]nabii huyu wa kiafrika alikuwa na maajabu mengi sana likiwa pamoja na hili
alikuwa akiingia kwenye chumba alikuwa na uwezo wa kujaa chumba kizima na hii ilipelekea mauti yake ambapo siku moja alijaa kwenye chumba na nje kulikuwa na kuku mmoja aliyekuwa anatembea kutafuta chakula aliona kitu kama nyama na akadonoa kumbe ulikuwa mwili wa nabii huyu na hapo hapo mauti yalimfika nabiii wa kiafrika akafa akiwa ameacha maajabu mengi[/QUOTE]
 
Wairaqw wa MBULU husimulia utabiri mbalimbali wa nabii aitwaye SAIGILO, huyo SAIGILO asili yake ni Barbaig kama sikosei. Alitabiri mambo mengi pia juu ya Mwl JK Nyerere na zama zake na tabiri zingine zilimulika hadi kizazi cha sasa. Mwenye tabiri za SAIGILO aziweke hapa.
 
mkuu nilibahatika kupata pia habari za Ng'wanamalundi,

Nabii huyu alikuja baada ya Ibambangulu,

Ng'wanamalundi alikuwa akitembea juu ya maji km Yesu, hadi wakoloni walikoma, alikuwa na uwezo wa kunyoosha kidole na mti unakauka papo hapo,
Huo haukuwa unabii ulikuwa uchawi wa kiwango cha democrasia. Kwetu tanga baba ananiambia alikuwa na mjomba wake anaweza kutembea kwenye mvua na akafika mkavu hata tone halimgusi akiulizwa imekuwaje anasema mvua inawanyeshea wanawake sio wanaume, pia alikuwa anaweza kunyoosha kidole likatoa mwanga kama tochi akatembea usiku mzima mwanha haupungui.

Manabii wa dizaini hii kwa Africa wanafika mamilioni, kila ukoo ulikuwa na manabii wao
 
Kung'atwa Na Nyoka inaleta mantiki kuliko Kuku.Huyo Kuku alikuwa Na sumu au?

Miiko baba yangu elewa watu wenye mambo makubwa always wana condition fulani zinazowafanya wawe tofauti na wengine eg. Yesu saa yangu haijafika, Nimeishiwa nguvu baad ya mwanamke kugusa nguo yake nk. Hakuna nguvu isiyo na masharti kokote juu au chini ya dunia.
 
Mkuu natumai uko salama..nilitamani zaidi kupata historia ya Nindwa..mana hili jina lipo katika ukoo wetu ila sina historia yake huyo nabii Nindwa.

#MaendeleoHayanaChama.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyerere ni habari ingine wacha kabisa,huku MBULU Manyara Kuna nabii alijulikana kwa jina la Saigilo,kipindi Kama hicho Cha ibambangulu alitoa unabii uliotimia mwingi sana,ukiwemo wa mwalimu Nyerere
 
siju kama alikuwa nabii ila jina lake lina maana ya muwamba mbingu nadhani alikuwa anawez kujaa ndani ya nyumba hadi inabomoka na kifo chake kilikuwa cha ajabu pia alijaa ndani ya nyumba na nsehemu ya ngozi yake ikatokeza kwenye ufa wa nyumba na kuku akamdonoa akafa
 
Wasukuma hawajambo kwa sayansi za miuzauza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…