Ibambangulu, nabii mtenda miujiza aliyetabiri kuzaliwa kwa Mwl Nyerere

Ibambangulu, nabii mtenda miujiza aliyetabiri kuzaliwa kwa Mwl Nyerere

Huo uwezo ulikuwa wa kawaida sana kama kifo chake kilisababishwa tu Na Kuku.Hivi Kuku tu asababishe mtu kwenye uwezo wa pekee age? Hebu leta ufafanuzi zaidi.



QUOTE="Michael Chairman, post: 19169503, member: 284116"]nabii huyu wa kiafrika alikuwa na maajabu mengi sana likiwa pamoja na hili
alikuwa akiingia kwenye chumba alikuwa na uwezo wa kujaa chumba kizima na hii ilipelekea mauti yake ambapo siku moja alijaa kwenye chumba na nje kulikuwa na kuku mmoja aliyekuwa anatembea kutafuta chakula aliona kitu kama nyama na akadonoa kumbe ulikuwa mwili wa nabii huyu na hapo hapo mauti yalimfika nabiii wa kiafrika akafa akiwa ameacha maajabu mengi[/QUOTE]
 
Wairaqw wa MBULU husimulia utabiri mbalimbali wa nabii aitwaye SAIGILO, huyo SAIGILO asili yake ni Barbaig kama sikosei. Alitabiri mambo mengi pia juu ya Mwl JK Nyerere na zama zake na tabiri zingine zilimulika hadi kizazi cha sasa. Mwenye tabiri za SAIGILO aziweke hapa.
 
mkuu nilibahatika kupata pia habari za Ng'wanamalundi,

Nabii huyu alikuja baada ya Ibambangulu,

Ng'wanamalundi alikuwa akitembea juu ya maji km Yesu, hadi wakoloni walikoma, alikuwa na uwezo wa kunyoosha kidole na mti unakauka papo hapo,
Huo haukuwa unabii ulikuwa uchawi wa kiwango cha democrasia. Kwetu tanga baba ananiambia alikuwa na mjomba wake anaweza kutembea kwenye mvua na akafika mkavu hata tone halimgusi akiulizwa imekuwaje anasema mvua inawanyeshea wanawake sio wanaume, pia alikuwa anaweza kunyoosha kidole likatoa mwanga kama tochi akatembea usiku mzima mwanha haupungui.

Manabii wa dizaini hii kwa Africa wanafika mamilioni, kila ukoo ulikuwa na manabii wao
 
Kung'atwa Na Nyoka inaleta mantiki kuliko Kuku.Huyo Kuku alikuwa Na sumu au?

Miiko baba yangu elewa watu wenye mambo makubwa always wana condition fulani zinazowafanya wawe tofauti na wengine eg. Yesu saa yangu haijafika, Nimeishiwa nguvu baad ya mwanamke kugusa nguo yake nk. Hakuna nguvu isiyo na masharti kokote juu au chini ya dunia.
 
Mkuu natumai uko salama..nilitamani zaidi kupata historia ya Nindwa..mana hili jina lipo katika ukoo wetu ila sina historia yake huyo nabii Nindwa.

#MaendeleoHayanaChama.
Kabla ya Ibambangulu na Mwanamalundi alikuwepo nabii Sitta. Huyu alitabili ujio was wakoloni na jinsi watakapotesa watu. Alitabiri pia kuzaliwa kwa mkombozi wetu JK Nyerere. Ukitaka historian yake fika Bariadi kijiji cha Kilulu (Gabu). Hapo kuna mlima au jiwe alilokuwa anapanda na kuongea na watu walio umbali was kilomita kumi na wakasilizana. Pia kuna picha ya mkewe kwenye jiwe. Picha hii haikubali kupigwa kwa kamera. Ukipiga litatoka jiwe tu bila picha. Kuna maajabu mengi tu ukifika Gabu. Huyu ndiye chanzo cha nabii Nindwa. Alikuwa na uwezo was kuunda jeshi kwa kutamka tu.
Ukweli yapo mengi.

Hakufa alipotea tu kwa hiyo hakuna anayejua kaburi lake.
Kuna wakati Wamasai huja kuhiji hapa sijajua uhusiano wa Sitta na wamasai. Kipindi cha vita ya wasukuma na wamasai walikuwa wakija wanasindikizwa na Polisi maana wasingerudi salama.
Kuna watu huwa anawatokea had I sasa japo siwezi kulithibitisha hili. Utalii huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyerere ni habari ingine wacha kabisa,huku MBULU Manyara Kuna nabii alijulikana kwa jina la Saigilo,kipindi Kama hicho Cha ibambangulu alitoa unabii uliotimia mwingi sana,ukiwemo wa mwalimu Nyerere
 
Heshima kwenu Mabibi na Mabwana, Poleni na heka heka za maisha

Km kichwa cha habari kinavyosomeka, Imbangulu ni Nabii mtenda miujiza km ilivyokuwa kwa manabii wengine enzi hizo, inasemekana katk karine ya 19, Nabii huyu aitwaye Imbangulu alipata kutabiri kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpigania uhuru mashuhuri wa Afrika aliyeleta changamoto kubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Kama ilivyokuwa kwa manabii wengine ambao dini hudai habari za kuzaliwa kwao zilitabiriwa na manabii au nabii, basi hata kuzaliwa kwa Mwokozi wa Afrika na Tanganyika yaani Mwalimu kulitabiriwa na nabii wa Mungu aitwaye Ibambangulu, Nabii Ibambangulu inasemekana alikuwa Nabii mtenda miujiza, miujiza mingine aliyoitenda Ibambangulu inasemekana hata Yesu hakuwahi kuitenda, Ibambangulu alikuwa msukuma, alikuwa anaishi Magu ktk mkoa wa Mwanza.

Inasemekana Nabii huyu alikuwa na desturi ya kupanda mlimani na kutazama mashariki wakati anapotabiri kama alivyokuwa akifanya Yesu na manabii wengine wa kidini, hatimaye ilipofika mwaka 1922, Butiama, Mkoani Mara, Mwalimu alipata kuzaliwa.

Km una lolote kuhusu nabii huyu Imbangulu Msukuma wa Magu mkoani Mwanza Karibu
siju kama alikuwa nabii ila jina lake lina maana ya muwamba mbingu nadhani alikuwa anawez kujaa ndani ya nyumba hadi inabomoka na kifo chake kilikuwa cha ajabu pia alijaa ndani ya nyumba na nsehemu ya ngozi yake ikatokeza kwenye ufa wa nyumba na kuku akamdonoa akafa
 
nabii huyu wa kiafrika alikuwa na maajabu mengi sana likiwa pamoja na hili
alikuwa akiingia kwenye chumba alikuwa na uwezo wa kujaa chumba kizima na hii ilipelekea mauti yake ambapo siku moja alijaa kwenye chumba na nje kulikuwa na kuku mmoja aliyekuwa anatembea kutafuta chakula aliona kitu kama nyama na akadonoa kumbe ulikuwa mwili wa nabii huyu na hapo hapo mauti yalimfika nabiii wa kiafrika akafa akiwa ameacha maajabu mengi
Wasukuma hawajambo kwa sayansi za miuzauza
 
Back
Top Bottom