"Wananchi ndiyo msingi wa Mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yote kutoka kwa wanachi".
Tumieni haki hiyo na wajibu tuliopewa kama raia kumkosoa na kumshauri Rais na Serikali yake.
Tusiwe watu wa kuimba mapambio tuuuu, wakati ndani tunaumia kutokana na baadhi ya mambo, huo ni unafiki. Na mnafiki ni bora kuliko mchawi.
Tuache kimbelembele na kiherehere cha kujbu hoja au ushauri unaotolewa na wananchi kwa Serikali na badala yake Serikali ndiyo ijibu. Wakati mwingine Serikali inakalia kimya hoja mbalimbali zinazotolewa na wananchi kutokana na machawa na wanafiki kujitanguliza mbele kujibu kama vile wao ndio viongozi wa Serikali.
Kwa upande mwingine Serikali inaponyamazia mambo haya na kuwaachia machawa na wanafiki kujibu, inaanza kujengeka picha miongoni mwa watu kuwa machawa na wanafiki hawa nao ni sehemu ya watu wanaokula Kodi tunazolipa.
Watu wenye mapenzi mema na Taifa hili waendeleo kutumia haki yao ya Kikatiba kutoa maoni, kushauri na kukosoa Serikali ilimradi wasivunje Sheria.
Ikitokea mwananchi katika kutoa ushauri, maoni, kukosoa, akateleza kwa namna moja au nyingine, Serikali iache kutafuta jinai badala yake waangalie maudhui na malengo ya mtoa hoja.
Sote tumeumbwa kukosea, ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Tusipomkosoa na kumshauri Rais tunamkufuru Mungu.