Sasa traffic count itapunguzaje congestation . kama JAICA wanazo takwimu za road usage ya barabara za dar hii solution ya IBM ni duplicate ya kazi waliyofanya JICA ?
Au ni solition ya ku monitor tu. Monitoring Road usage hitasaidi tunataka solution ya management . Ni sawa sawa na kumpima mgonjwa wa ukiwmi useme umetatua tatizo kwakugundua tu ana CD4 ngapi, Bila kumpatia dawa haisaidiii.
Nchi isiyokuwa na pesa inahitaji kufanya priority makini kwenye miradi yake. Kama JICA walifanya monitoring na kutoa takwimu kinachtakiwa na kinachofuata ni suluisho nini kifanyike kupungza congestion sio duplication ya ya kurecod tena msongamano wa magari . kazi ambayo JICA wameshafanya. Au mimi sijaelewa.
Kuna tofauti ya Solution finding a problem to solve and a problem finding a solution . Hii ya IBM ni Solution finding a problem to solve.
Traffic count ni takwimu tu ambazo hutumika kwenye 'traffic engineering & transport engineering" kwa ajili ya usanifu wa barabara na mambo mengine yahusuyo usafiri. Sanasana ni kujua idadi ya magari inayopita katika barabara husika kwa saa au kwa siku n.k. CCTV kwa ufahamu wangu na hasa kwenye nchi zenye mifumo ya kielectronic ya kwa ajili ya kusimamia mambo ya usafiri (Intelligent Transport Systems) zinatumika kwa ajili ya udhibiti na uangalizi kama vile mwendo kasi, kuweka kumbukumbu za matukio ya barabarani kama vile ajali, na wavunja sheria za barabarani.
Hivyo, utatuzi wa msongamano wa barabara Dar-es-Salaam ni hadi hapo serikali itakapotekeleza kwa 100% mapendekezo ya JICA kwenye hiyo 'master plan' , mojawapo ni kujenga barabara za pembezonni mwa jiji (ring roads), kufufua na kutengeneza access roads, na upanuzi wa barababar kuu ziingiazo katikati ya jiji, kujenga barabara za juu (elevated roads).