IBM (Tanzania) kupunguza msongamano wa magari katika Barabara za DSM!

IBM (Tanzania) kupunguza msongamano wa magari katika Barabara za DSM!

Sasa traffic count itapunguzaje congestation . kama JAICA wanazo takwimu za road usage ya barabara za dar hii solution ya IBM ni duplicate ya kazi waliyofanya JICA ?

Au ni solition ya ku
monitor tu. Monitoring Road usage hitasaidi tunataka solution ya management . Ni sawa sawa na kumpima mgonjwa wa ukiwmi useme umetatua tatizo kwakugundua tu ana CD4 ngapi, Bila kumpatia dawa haisaidiii.

Nchi isiyokuwa na pesa inahitaji kufanya priority makini kwenye miradi yake. Kama JICA walifanya monitoring na kutoa takwimu kinachtakiwa na kinachofuata ni suluisho nini kifanyike kupungza congestion sio duplication ya ya kurecod tena msongamano wa magari . kazi ambayo JICA wameshafanya. Au mimi sijaelewa.

Kuna tofauti ya Solution finding a problem to solve and a problem finding a solution . Hii ya IBM ni Solution finding a problem to solve.

Traffic count ni takwimu tu ambazo hutumika kwenye 'traffic engineering & transport engineering" kwa ajili ya usanifu wa barabara na mambo mengine yahusuyo usafiri. Sanasana ni kujua idadi ya magari inayopita katika barabara husika kwa saa au kwa siku n.k. CCTV kwa ufahamu wangu na hasa kwenye nchi zenye mifumo ya kielectronic ya kwa ajili ya kusimamia mambo ya usafiri (Intelligent Transport Systems) zinatumika kwa ajili ya udhibiti na uangalizi kama vile mwendo kasi, kuweka kumbukumbu za matukio ya barabarani kama vile ajali, na wavunja sheria za barabarani.

Hivyo, utatuzi wa msongamano wa barabara Dar-es-Salaam ni hadi hapo serikali itakapotekeleza kwa 100% mapendekezo ya JICA kwenye hiyo 'master plan' , mojawapo ni kujenga barabara za pembezonni mwa jiji (ring roads), kufufua na kutengeneza access roads, na upanuzi wa barababar kuu ziingiazo katikati ya jiji, kujenga barabara za juu (elevated roads).
 
Sioni uhusiano wa IBM


  • na kupunguza foleni
  • sioni uhusiano wa CCTV na kupunguza foleni?
  • Je IBM wamafanya kazi hii wapi au Tanzania ndio Pilot site yao ya solution zao na congestation ???

But kwa serikali yetu ya Tazania ukmjumulisha na huyo jamaa mhhh any project is possible

Hawa jamaa wanataka kuuza CCTV systems kwa deal za kifisadi, Dar haina barabara zilizopo ni nyembamba mno na hakuna wide parking spaces, zote zimeuzwa kwa wezi!
 
Jamani solution ya foleni Dar sio kujenga barabara tu kama wengi tunavyofikiria. Kuna mambo mengi yanayopashwa kuendana na ujenzi huo wa barabara na hapa najua wengi wanazungumzia fylovers. Mojawapo ya suluhisho lingine la foleni ni kupanua mji na kuzitoa baadhi ya ofisi muhimu katikati ya mji ili watu badala ya wote kuamka asubuhi tukielekea Samora Avenue, tuwe tunaelekea mbagala, Tegeta au Mbezi!!!!

Tiba

Miaka ya nyuma mashirika makubwa yalikuwa na staff busses, lakini sasa yanaona ufahari kila staff ana usafiri wake hata wale wa ngazi za chini. Utaratibu wa zamani urudishwe kwa kutungiwa sheria.
 
Foleni za Dar husababishwa na makutano ya barabara sababu zingine huchangia kidogo sana. Kwahiyo kukiwa na flying over foleni kwisha. Hili la IBM laweza kuwa ni dili la watu fulani la kutaka kutafuna tu pesa za walipa kodi wa TZ
 
Tukiweza kufanya maamuzi baada ya utafiti tutafanikiwa. Kwa kukurupuka hatusongi mbele. Nitoke vipi! haha
Shirikisha wadai mheshimiwa.
 
Kinachozungumzwa hapa tayari kilishafanyiwa utafiti na JICA kwenye ule mradi uliojulikana "The Study on Dar es Salaam Transport Policy and System Development Master Plan". Na kimsingi DART ni sehemu ya utekelezaji wa mapendekezo ya hiyo master plan, pamoja na ujenzi wa "fly-overs/under-pass" kwenye jiji la DSM. Bahati mbaya report kama hizi haziwekwi hadharani, utadhani ni siri wakati siyo siri. Wanachopendekeza IBM tayari kilishafanyiwa utafiti na hao JICA, na naamini traffic count ni shehemu ya takwimu zilizo kusanywa. Kwa hiyo siyo kitu
kipya.

Na hiyo DART imelogwa? Mbona maendeleo ya maana hayaonekani?
 
wantafuta hela tu hao....
Njia ya kutatua foleni ni kupanua barabara zetu....
Na kuwa na barabara mbadala za kutosha.....
Mfano watu wa kimara wanaofanya kazi posta hizo CCTV cameras zitasaidia nini?
 
Miaka ya nyuma mashirika makubwa yalikuwa na staff busses, lakini sasa yanaona ufahari kila staff ana usafiri wake hata wale wa ngazi za chini. Utaratibu wa zamani urudishwe kwa kutungiwa sheria.


mkuu humalizi tatizo kwa kukimbia tatizo.....solution sio kubania watu umiliki wa usafiri la hasha...... Ni kupanua miundombinu, barabara toka enzi za nyerere zipo vilevile halafu utegemee cctv camera zisaidie nini?
 
Siamini kama kupanau barabara kutatua tatizo la foleni Dar kwa muda mrefu, tunachohitaji ni public transport nzuri pamoja na kuongeza gharama za kumiliki gari kwa kiasi ambacho itakuwa ni ngumu kwa majority kumiliki magari au kuyatumia kila wakati hii inaweza kufanywa kwa njia nyingi kodi ya gari/import/mafuta/tolls kuingia maeneo fulani etc.

Ila hilo la mwisho politically ni maamuzi magumu sana maana walalahoi ndo wataumia zaidi, na sidhani kama tuna kiongozi mwenye ubavu huo.
 
Nadhani wana CCTV za kuchezea.
Zitawekwa maeneo gani wajanja wasiondoke nazo?
Barabara zatakiwa kuboreshwa kwanaza kabla ya jambo lolote lile.
OTIS
 
Hawa jamaa wanataka kuuza CCTV systems kwa deal za kifisadi, Dar haina barabara zilizopo ni nyembamba mno na hakuna wide parking spaces, zote zimeuzwa kwa wezi!

hii inajionyesha dhahiri. naskia harufu ya wizi wizi hivi.
 
Hivi ulishawahi kujiuliza km madereva wt dar wanajua kuwa kwenye njia mbili ile ya ndani nii ya wanaoenda kasi? Unashangaa jamaa yupo 40km/hr hana ata wasiwasi, piga honi,washa taa wala haelewi, hangaika mwenyewe kumpita, af ni sheria kabisa trafiki polisi anaweza kukushtaki kwa hilo, asa cjui km polisi hawajui manake wanakamata makosa mengine tu, hz cctv wangapi watasikiliza matangazo yk badala ya mziki na vichekesho clouds
 
Back
Top Bottom