Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
IBRAHIM BABA WA IMANI ALIMWAMBIA ISHMAEL MWANAYE AMFUKUZE MKEWE KWA SABABU HANA HESHIMA NA ADABU. ISHMAEL AKAMTII BABAAKE AKAMFUKUZA MKEWE.
Anaandika, Robért Heriel
Mtibeli
Ukitaka ndoa na familia yako íwe Stable hata nyakati ñgumu na watoto wako wawe na nidhamu na wafaníkiwe basi Nakushauri Role model wako katika mahusiano awe Ibrahim. Tafuta kisa cha Ibrahim na familia yake. Visa kutoka vyanzo mbalimbali. Kisha jifunze.
Elewa, duniani hakuna jipya.
Baada ya miaka mingi kupita tangu Ibrahim alipomfukuza Hajri na Íshmael.
Hajri na Íshmael walienda kuishi jangwa la Beer-Sheba.
Huko wakaishi mpaka íshmael akafikia umri wa kuoa. Hajri mamaye akaenda Misri kumchukulia Mke. Kumbuka Hajri ni Mmisri na alikuwa mtoto wa Mfalme kutoka katika moja ya Masuria wa Mfalme wa Misri. Hii ni Stori nyingine.
Ishmael akamwoa mkewe kisha wakapata Watoto. Shughuli za Ishmael zilikuwa uwindani na kurusha upinde.
Miaka mingi ikapita pasipo ya Íshmael kumwona Babaake, Ibrahim.
Wakati huo Ibrahim alikuwa amehamia Nchi ya Wafilisti akiwa ametoka nchi ya Kanaani. Akakaa huko siku nyingi sana bila ya kumwona mwanaye, íshmael.
Siku moja Ibrahim akamuaga Sarah Mkewe Kuwa anataka kwenda jangwa la Beer-Sheba kumwona Ishmael kwani ni miaka mingi imepita hajamtia machoni. Nao uzee ulikuwa umechanganya.
Sarah akamruhusu Mumewe lakini kwa masharti.
Ibrahim akaondoka na ngamia mpaka huko jangwa la Beer-Sheba huko akakuta mahema mengi akiwa amefika majira ya mchana jua la utosini. Akauliza uliza Watu wa eneo lile. Akaonyeshwa hema la mwanaye íshmael.
Akafika kwenye hema la Ishmael akiwa juu ya ngamia.
Akabisha hodi akapokelewa na sauti ya Mwanamke mmoja ambaye alikuja kutambua ni mkwe wake(mke wa íshmael). Watoto humo ndani ya hema walikuwa wakilia sana.
Ibrahim akamwambia Mkwewe, Mumeo yupo wapi. Mkwewe akamjibu ametoka ameenda kwenye shughuli zake za kuwinda.
Ibrahim akamwambia naomba unipatíe maji ya kunywa ninywe.
Mkwewe akamjibu humu ndani hakuna maji wala mkate.
Ibrahim bado alikuwa juu ya ngamia kwani Sarah Mkewe alimpa sharti kuwa atakapofika Beer-Sheba asije akashuka juu ya ngamia. Ibrahim alilinda kiapo na ahadi aliyomuahidi Mkewe kuwa atafanya kama alivyopatana naye.
Yule mkwewe akawa anawachapa watoto huko ndani ya hema huku akiwanenea maneno mabaya ya laana. Tena akawa anamlaani Íshmael mumewe.
Hayo yote Ibrahim alikuwa akiyasikia.
Ibrahim alichukia sana hasira zikawaka kifuani pake.
Lakini hakuwa na chochote cha kufanya.
Ikabidi amuage.
Akamwita Yule Mwanamke ambaye ni Mkwewe ambaye mpaka muda huo hakumtambua Ibrahim kama ni Babake na Íshmael.
Yule Mwanamke akatoka hemani akaja kusimama mbele ya Ibrahim wakitazamana.
Ibrahim akamwambia, akija mumeo Íshmael mwambie alikúja mwanaume mzee mmoja kutoka nchi ya Kanaani ambaye hakuwa na mwonekano wa kuvutia na maskini. Nikamwambia hakuna maji wala mkate. Tena mwambie kuwa yule mzee amesema hilo Hema lako fito zake zimeharibika hivyo uzibadilishe.
Ibrahim aliposema hayo akaondoka. Jioni Íshmael akafika. Mkewe akamsimulia kila alichoambiwa na yule mwanaume mzee ambaye ni Ibrahim.
Ishmael akajua mzee yule alikuwa ni Babaake, Ibrahim. Alichukia sana na kumkasirikia Mkewe kwa sababu hakumheshimu Babaake.
Pia alielewa maana ya kubadilisha fito za lile hema kuwa zimeharibika, akamfukuza Mkewe kwa sababu hakumheshimu Babaake na alimpimishia kutokana na mwonekano wa Ibrahim ambaye alijivika mavazi ya kimaskini na alijitia unyonge kwa malengo aliyoyajua yeye mwenyewe.
Ishmael akaenda kuchukua mke Kanaani akamwoa.
Miaka mitatu ikapita. Ibrahim akafunga safari tena kwenda kumwona mwanaye, íshmael.
Akafika kwenye hema la Ishmael majira yaleyale ya mchana wa jua la utosini.
Akamkuta mkewe Íshmael.
Yule mkewe akamkaribisha, akamwambia, karibu Bwana wangu, nikuandalie mwanambuzi, shuka nikuoshe miguu yako niitoe vumbi.
Ibrahim akamwambia Mkwewe, hapana binti yangu. Mumeo yuko wapi nipate maji tuu kwa maana ninakiua.
Basi yule Mwanamke baada ya kumueleza Ibrahim kuwa mumewe Íshmael yupo kazini kwenye kuwinda akiwa kamletea Maji.
Ibrahim akamwambia Mkwewe, akija mumeo Íshmael mwambie alikúja mwanaume mmoja mzee sana. Nikampa maji na kutaka kumuandalia mwanambuzi na kumuosha miguu lakini alikataa. Akanywa maji. Tena umwambie kuwa Fito za hema hili ni nzuri na imara asiziondoe.
Ibrahim alipokwisha kusema hayo akaondoka.
Íshmael aliporudi akaambiwa yote na mkewe. Akatambua yule aliyekuja alikuwa Babaake, Ibrahim. Akafurahi kuona mkewe alimheshimu licha ya kuwa alikuja kimaskini ingawaje hakuwa Maskini.
Mkewe alishangaa kusikia kuwa aliyekuja alikuwa Baba mkwe.
Mungu akaibariki familia ya Ishmael.
Mwisho wa hiyo Stori.
Stori hii ni ya kifamilia.
Ukisoma stori hii utagundua kuwa Familia ni chanzo kikuu cha mafanikio ya mtu kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Mungu hubariki familia zenye utulivu, upendo na amani.
Ibrahim alimshauri mwanaye AMFUKUZE mkewe kwa sababu hakuwa na adabu na kama hakumheshimu asiyemjua bila shaka hawezi kumheshimu anayemjua.
Ibrahim aliona kuwa mafanikio na baraka za mwanaye zitakuwa kizuizini kwa sababu hakuwa na mke Sahihi.
Hivyo ili zile baraka za Mungu alizoahidiwa zitimie sharti AMFUKUZE mkewe.
Pia tunajifunza kuwa kumtii Baba kwa sababu wababa wengi hutoa ushauri usio na wivu tofauti na kinamama.
Mwisho kabisa, Mwanamke kama hakuheshimu wala hana adabu kwa wazazi wako wala adabu kwa Watu huyo fukuza
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam